Sintofahamu kuhusu mradi wa TASAF

jongo

Member
Aug 15, 2012
26
1
Kitendo cha serikali kufumbia macho fedha za mradi wa kunusuru kaya maskini (TASAF) zinazoliwa na watendaji wa vijiji na mitaa hakikubaliki, kufuatia kile kinachoitwa mradi huo kwenda kinyume na malengo ya kunusuru kaya maskini sasa unanusuru kaya tajiri na watendaji wa vijiji na mitaa, hasa katika maeneo ya mijini, asilimia kubwa ya wanaopokea fedha hizo si walengwa wa mradi.

Lakini pia kuna baadhi ya watu waliojiandikisha kisha wakati wa ugawaji hawapo kutokana na kukosekana wanapoishi fedha hizo hubaki kuwa mali ya mratibu wa mradi, mwenyekit, mtendaji na wajumbe teule wa mradi huo, serikali ya rais John Magufuli bado haijaliona hili na kuacha fedha za watanzania zikiwanufaisha wachache.

Kuna ulazima wa mradi huu kupitiwa upya na waliofuja fedha hizo kuchukuliwa hatua haraka.
 
Namna bora ya kumsaidia mwenye njaa ni kumwezesha aweze kuzalisha chakula mwenyewe. Kwa mfano badala ya kumpa maskini samaki, MPE nyavu atavua kila siku. Na kwa mtaji huo utaona kuwa TASSAFu lengo lake ni kununua kura za RAIA maskini wa vijijini!
 
Back
Top Bottom