Abuu Said
JF-Expert Member
- Jul 5, 2015
- 4,010
- 4,761
Wazee wa MMU habari zenu, kuna kautafiti kadogo nimekafanya baina ya Watu waliokua kwenye mahusiano na wale ambao hawako kwenye chain ya mahusiano ya kimapenzi.
Ambao hawako kwenye mahusiano ya kimapenzi
Ambao hawako kwenye mahusiano ya kimapenzi
- Kama ni mwanafunzi anakua ni kipanga, kama ni mfanya kazi anakua mtendaji mzuri wa kazi. Hii inatokana na kwamba mtu wa carrier hii hapotezi muda wake kufikiria masuala ya kimapenzi, kupigapiga simu hovyo kwa mpenzi wake na kuuliza masuala ya kijinga like hello baby umeshakula, unafanya nini na mengine mengi.
- Hawachagui mavazi. Kwa kuwa kichwa chake muda wote kinafikiria maisha huwa hawaangalii leo nitokeje ili mpenzi wangu anione nilivyopendeza au workmate/classmate wanione jinsi nilivyopendeza kwa kuwa yeye ajishughulishi na mambo ya kimapenzi hajali katokaje kwa hiyo anaokoa muda wake na fedha zake kufanya shopping na kujichungulia kwenye kioo.
- Pesa yake inatumika mambo ya msingi. Hawa watu mara nyingi pesa zao zinatumika kwa maswala ya msingi tu sio kulipia Gest/lodge au kumtoa mpenzi wake sehemu za starehe, au kumnunulia mavazi ya gharama, au kununua Vocha kila mara kuongea na baby wake.
- Wanakwenda na wakati hawana muda wa kupoteza. Utakuta watu walio kwenye mahusiano anaweza akakesha usiku kwa kuongea mambo ya kipuuzi na mpenzi wake bila kujali muda huo anatakiwa awe amelala na kutuliza kichwa, kuna wengine waliokua kwenye mahusiano wanaweza hata wakaiba muda wa kazini ili aende akakutane na mpenzi wake na hapo anapunguza ufanisi wa kazi. Ni hayo tu machache kwa sisi watu tuliokua Single tunajivunia kama kuna mengine ongezeeni. Nikija kua kiongozi nitaweka sheria kali juu ya jambo hili la mahusiano nitalipiga vita km haya mapambano ya Madawa ya kulevya. NAWASILISHA