Hakuna gari ya moja kwa moja toka singida to masasi njia nzuri ni kupitia dsm.
Fika dsm,kisha nenda temeke sudani au mbagala rangi tatu ndio gari za kusini zinakopatikana gari nzuri ni buti la zugu,maning nice,warda,baraka classic nauli ni elfu 40 toka dsm to masasi mjini,safari ni ya masaa9.
Maisha ya masasi sio ya gharama sana kwa sababu ni mji wa kibiashara hivyo vyumba vinapatikana kwa bei rahisi pia chumba single self 50k,chumba sebule self 80 hadi laki kutegema pia na eneo.
Karibu masasi usisahau kuja na mafuta ya alizet na vitunguu pia usisahau kula samaki ukifika nagurukuru kilwa.
Utawapa hii wala bata wa Kibo Lounge,Adamu viazi,center yao ya kibiashara inaitwa Mkuti.
Mitaa mizuri ya kuishi isiyo na uswahili ni Mtandi,maliasili mpya,mkomaindo,maendeleo.