singida.utumwa warejea kwa kasi ya kutisha. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

singida.utumwa warejea kwa kasi ya kutisha.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mwanakidagu, Apr 9, 2012.

 1. m

  mwanakidagu JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 208
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni dhahiri sasa zile kazi za ndanina nje.(house boy ,house girl, bar maids.na bila kusahau zile kazi za umanamba kwenye mashamba ya tumbaku na katani mkoa wa tabora na huko tanga.).zimebatizwa kwa majina kama hayo hapo juu.mkoa huu umegeuka kuwa soko muhimu kwa kazi kama hzo.watoto wadogo wakike kwa wakiume wamekuwa wakisombwa kila mwaka kwenda kufanya kazi za kitumwa hasa katika majiji ya nch hii na baadhi ya mikoa hapa tz.wana wema wa jf.hebu changieni maoni yenu. Hapa.niliwasikia kina mama fulani jijini mbeya waliokuwa na mradi wa kufungua bar.mmoja akasema.inabidi twende singida kuchukua mabinti wa kufanya kazi bar,mwingine kaunga hoja kuwa ni kweli kwani ni weupe.nk wakaendelea hvyo.elimu mkoani humu inashuka.kila mwaka.nini kifanyike.juhudi gn zichukulwe kuinusuru jamii yangu?.changia mawazo yako.hapa tafadhali .nitayafanyia kazi.
   
 2. u

  ureni JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Kweli hawa nafikiri walichokosa ni elimu,inabidi serikali iangalie kwa karibu hii mikoa ambayo iko chini kimaendeleo na kielimu manake siwezi kusema wanatatizo la kifedha,kwa sababu wanamazao yao kama mtama na alizeti ambayo yanawaingizia kipato,kitu ambacho kinaweza kuwatoa ni kuinvest kwenye elimu na shule zijengwe za kutosha na serikali itoe upendeleo katika mikoa kama hiyo.

  Naweza kutoa mfano kama mkoa kilimanjaro,wao hawana zao la kuwaingizia fedha kwa sasa hivi manake kahawa waliyokua wanaitegemea hamna tena imekufa lakini waliweza toka mwanzo kuelewa umuhimu wa elimu wakainvest vizuri,sasa hivi uchumi wao mkubwa unategemea elimu waliyoinvest.
   
 3. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,349
  Trophy Points: 280
  Wana mwamwedi intapraisi wao. Akiona wamezidiwa huwa anawapanga foleni na kuwagawaia unga.....(Nimeandika hayo kwa uchungu sana kwa sababu watu kama hao hakuna anayewakumbuka tena na wao hawajui cha kufanya ili kujikomboa...
   
 4. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,738
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kama unaweza, chapisha makala kuhusu ubaya au hatari zinazohusiana na kazi hizo. Jitahidi utoe matamko kutoka kwa waathirika. Pia ukipata nafasi ya kuongea iwe vijiweni, kwenye mihadhara n.k ufanye hivyo, labda itasaidia. WAFANYAKAZI WA NDANI, BAA, GUEST HOUSE WANATESWA HUKU MIJINI, JITAHIDI KUPUNGUZA MADHARA
   
Loading...