Sinema za Tanzania utazijua tu

Sinema za Tanzania utazijua tu

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Zinavyoanza na zinavyoishia.Wahusika wake na waandaaji wa sinema husika. Wanaouambia umma juu ya uwepo wa sinema hizo ni wale wale. Hazina tofauti kabisa. Kweli ni sinema za Tanzania. Made in Tanzania. Ili nieleweke,nitatoa mfano wa sinema mbili maarufu Tanzania: EPA na Escrow.

Kwanza, waanzilishi wa sinema hizo ni wapinzani. Zilipopamba moto, kila mtanzania alikuwa akizizungumzia kwelikweli huku akiapa kuidhibu CCM na Serikali yake hivi au vile. Halafu hakuna la maana na maisha huendelea.Wahusika wa sinema hizi ni viongozi wa kisiasa na kiserikai pamoja na wafanyabiashara wakubwa. Kwa majina siwajui!

Mwisho wa sinema hizo ni wakwapua/wachota pesa hutakiwa kuzirejesha.Na kwakuwa ni sirini (baina ya wakwapuaji na Serikali) upeo na macho ya umma hugota hapo na pazia hushushwa kuashiria mwisho wa sinema husika. Sitaki kuzungumzia sinema za Operesheni Tokomeza, Richmondna nyingnezo kwa leo. Kubwa ni kuwa jinsi ya uchezwaji na hata scenes hufanana. Sinema za Tanzania.

Punde tutawashiwa sinema nyingine!


Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Na hata watazamaji ni wale wale na wanatabirika...

Sinema hata iwe mbaya vipi lazima watainunua tu...
 
Uandishi wako wenyewe wa kisinemasinema, huna jipya Anodi Shoziniga
 
Na hata watazamaji ni wale wale na wanatabirika...

Sinema hata iwe mbaya vipi lazima watainunua tu...
Wengine hununuliwa sinema hizo hata kama hawazitaki wanalazimishwa kuziangalia
 
na hata stering huwa ni yule yule ila huonekana kwa majina tofauti
 
Sinema za Tanzania ni sawa na waigizaji wake. Si unawaona kina Wema, Johari, na wengine waliopo pale kwa ajili ya kujiuza badala ya kuelimisha jamii.
 
Back
Top Bottom