Mlenge
R I P
- Oct 31, 2006
- 2,125
- 2,318
Mabasi ya mikoani yaonyeshe sinema ambazo zinafaa kuangaliwa na familia. Sinema yoyote yenye kuhitaji maamuzi ya mzazi (PG) au zaidi ya hapo, zisionyeshwe kwenye mabasi kwa vile mzazi hana uwezo wa kumzuia mwanae kuangalia. Ruksa ya kuweka video yoyote ni pale tu basi linapokuwa na skrini kwa kila abiria kujichagulia anachotaka kuangalia. Si mabasi mengi yana skrini za hivyo.
Video zinazoonyeshwa sana kwenye mabasi mengi ni:
1. Video za Bongo Muvi, ambazo lugha na maudhui yanayotumika hayafai kwa watoto. Wapo wazazi wasiotaka watoto wao waangalie Bongo Muvi kwa sababu hizo.
2. Video za vita na mapigano, ambapo watu huchinjwa, kuuliwa na ambazo ni wazi si za kuangaliwa na watoto wadogo.
3. Video za miziki. Hizi huwa na wachezaji waliovaa nguo ambazo kwenye ofisi za umma haziruhusiwi, na ambao hucheza kwa mitindo ambayo hadhira yake si watoto wadogo. Ukiongezea lugha na maudhui ya nyimbo hizo, ni hatari tupu kwa utazamaji wa watoto wadogo.
Zipo video nyingi zinazoweza kuonyeshwa kwenye mabasi ya safari za mkoa kwa mkoa. Mf., 300 Family Movies - How many have you seen? . Ni wakati sasa Bongo Muvi wakaanza kutengeneza senema za kuweza kutazamwa na familia nzima. Wawaige Ubongo Kids Videos – UBONGO KIDS