Sina imani tena na tigo-pesa!

Aputwike

Senior Member
Aug 9, 2016
170
250
Nimekuwa nikitumia sana account ya m-pesa kuhamisha salio kwenda kwenye wallet account ya m bet ili nibetie kwa jero jero, na salio limekuwa likifanikiwa kuhama, hata likichelewa kama kuna tatizo la mtandao, basi haichukui dakika nyingi sana. Na ukiwapigia wahudumu wa voda, watakupa ufafanuzi na kukuelekeza usubiri baada ya muda mfupi mtandao utengamae, na kweli inakuwa hivyo.

Sasa hawa tigo naona wameanza utapeli. Tangu nifungue wallet account ya m bet kwa tigo, wamenitapeli. Hii ni mara ya pili wananifanyia hivi. Siku moja nilikuwa nahamisha salio kutoka tigo pesa kwenda wallet, message hawajanirudishia kuwa salio limehama na hata kwenye account ya wallet salio halijafika. Basi ikawa ntolee. Kwakuwa ilikuwa pesa ndogo nikapotezea. Juzi juzi tena nimehamisha salio mambo yakawa vilevile, nikaona ngoja niwapigie, wakaniambia pesa bado ipo hewani kutokana na tatizo la mtandao. Baada ya siku tatu nikawapigia tena, majibu yakawa yale yale, wiki imepita nimewapigia, bado majibu yaleyale. Ukipiga huduma kwa wateja kwanza wanachelewa kupokea kama vile hili kampuni linajitolea bure, kumbe linakomba pesa zetu. Hivyo nimeamua kuwazilia hiyo hela na nimeapa kutotumia tena huduma ya tigo-pesa, nimeona ni wababaishaji tu wasiokuwa na malengo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom