#SimuliziZa116 - Watoto walelewe na baba au babu?

#SimuliziZa116 - Watoto walelewe na baba au babu?

Sema Tanzania

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2016
Posts
251
Reaction score
466
Mnamo tarehe 22 Oktoba 2019 tulipokea simu toka kwa Ndugu Sudi wa Tandahimba ambaye alitoa taarifa kuwa mzazi mwemzie (mama wa watoto wake) amewatelekeza watoto wao watatu Adam mwenye umri wa miaka 12, Selemani miaka 9 na Ahmad mwenye umri wa miaka 6. Alisema mama huyu ambaye sasa ameolewa na mume mwingine amewaacha watoto hao kwa babu yao ambaye hana uwezo wa kuwapatia malezi stahiki.

Ingawa Ndugu Sudi hutoa pesa za matunzo kwa watoto, alisema ana hakika hawaambulii lolote katika pesa hizo. Tayari alikwisha washirikisha wakwe zake nia yake ya kuwachukua wanawe - wakamkatalia. Alituomba ushauri afanyeje?

Tulimweleze utaratibu wa kufuata ikiwa ni pamoja na kumshirikisha Afisa Ustawi wa Jamii ambaye atafanya uchunguzi ili kubaini ukweli wa mambo kabla ya kutoa maamuzi ya hatma ya watoto.

Tulipekeka taarifa hizi kwa Afisa Ustawi wa Jamii Tandahimba kama rufaa. Tulimpigia baada ya mwezi mmoja Ndugu Sudi ambaye alitueleza kuwa baada ya uchunguzi wa Afisa Ustawi wa Jamii wakwe zake pamoja na mkewe waliitwa ofisi za Ustawi wa Jamii ambako iliamriwa kuwa kwa ajili ya maslahi bora kwa mtoto baba ndiye atawalea watoto.

Ndugu Sudi sasa analo jukumu la kuhakikisha watoto wake wanapata malezi bora.

Kila unapokwama juu ya hatma ya watoto wako. Tupigie namba 116 nasi kwa pamoja tutafikia muafaka. It's possible|Inawezekana.
 
Naam.. Watoto ni taifa la leo.
Tuwalee katika maadili wakue kimwili na kiakili..tuwapatie Mlo bora wa chakula na Maarifa. Huku tukiwatia moyo kua wao ni wathamani na wamezaliwa kuja kufanya mambo makubwa ulimwenguni
 
Naam.. Watoto ni taifa la leo.
Tuwalee katika maadili wakue kimwili na kiakili..tuwapatie Mlo bora wa chakula na Maarifa. Huku tukiwatia moyo kua wao ni wathamani na wamezaliwa kuja kufanya mambo makubwa ulimwenguni
Habari mdau wetu. Tunakushukuru mno kwa maoni mujarabu
 
Back
Top Bottom