Simulizi za sasa

Japhet Lufungulo

New Member
Joined
Sep 2, 2025
Posts
4
Reaction score
3
SIMULIZI-JAYLAN
MTUNZI-JAPHET LUFUNGULO
SEHEMU-02
TULIPOISHIA

Ni pale ambapo binti ambae mpaka sasa bado hatujamjua jina vizuri alisimama na kuanza kupungia magari yaliyokua mbele yake bila ya kujua watu watu wale Walikua ni wale waliomteka mda mfupi uliopita na yote ilikua ni sababu ya giza pamoja na ile mianga mikali iliyomfanya ashindwe kuona vizuri mbele.

"Shenzi sana kumbe alipona bila hata ya jeraha sasa mmalizeni haraka sana" ilisikika sauti ya mkuu yule ambae sasa alifahamika kwa jina la STEVEN

Mda huo mwanajeshi mmoja aliekua mbele ya dereva akichomoza kichwa nje huku akiwa na bunduki aina ya M4 carbine ambayo aliielekeza mbele ya yule binti,.mda huo huo wengine nao pia waliokua magari ya nyuma nao walilenga shabaha kuelekea pale alipokua binti yule ambae sasa licha ya kuona mwanga ulikua umeanza kuzoea macho yake ndipo alipoona rangi halisi ya magari yale, pia aligundua hali ya hatari baada ya kuona midomo ya bunduki zile zikiwa zimemuelekezea yeye.

Moja kwa moja sasa alifahamu fika hakua kwenye mikono salama tena kama alivyofikiria,lakini iliku ni kasi ya ajabu binti yule aliitumia kukwepa risasi moja iliyokua inakuja uelekeo wa kifua chake na kujirushia pembeni kwenye kichaka kilichokua kimeambatana na msitu uliokua pembeni kuelekea chini.

"Fanya haraka anakimbia huyo" ilisikika sauti ya steven ikiamuru na huku kundi kubwa la wanajeshi walishuka huku wakimimina risasi uelekeo aliokua ameelekea binti yule ambae katika kukimbia kwake bahati mbaya risasi moja ilimpata usawa wa bega lake la kushoto

Na kumfanya aanze kuvuja damu japo hakutaka kupunguza kasi zaidi alijali tu kukimbia mbele kwenye giza lile la msitu ule.

UPANDE WA PILI

Yule kijana ambae mda uliopita tulimuona akitoka supermarket akiwa njiani ndipo aliona mtu akiibukia pale barabarani toka msituni huku mkono mmoja ukiwa bega lake la kushoto lililokua likivuja damu mda huo huku mkono mwingine wa kushoto ukiwa na bastola yaani gunshot aliunyoosha kuelekea alipoku kijana huyo ambae nae alikua kwenye gari lake na kumfanya sasa kusimamisha gari lile kwa ghafla sana.

"Mungu wangu kitu gani tena hiki" alijisemea kijana yule mara baada ya kugundua wakati huo bastola yake hakua ametembea nayo na kukumbuka vizuri kua aliiacha tu nyumbani,hivyo sasa hakua na ujanja mbele ya mtu yule moja kwa moja tu alijua alikua ni jambazi.

Basi baada ya kusimamisha gari lile haraka mdada yule alilisogelea gari na kuingia upande wa nyuma wa gari na kuamuru sasa safari ianze huku mda huo kwa nyuma mdada yule aliwaona baadhi ya wale wanajeshi wakiwa ndio wanafika mahala pale huku wakionekana kuchanganyikiwa juu ya uelekeo alioelekea binti huyo.

"Nafikiri kama hajateka gari hapa njiani basi atakua amekimbukia msituni na kutuchezea akili" aliongea mwanajeshi mmoja huku akiwapa ishara wanajeshi wenzake kurudi tu walikotoka kwa ajili ya kupanga mikakati yao ya kijeshi ya kumsaka mdada huyo.

"Ongeza speed tunaelekea duka la dawa sasa hivi" ilikua sauti ya huyo mdada akimuelekezea dereva yule.

"Hapo mbele kuna kituo cha mafuta kama kilometa 50 hivi pia duka la dawa linapatikana hapo" alijibu vile dereva yule huku mda mwingi akiutumia kumwangalia mdada huyo kupitia kioo cha gari lake.

Mdada huyo hakujibu chochote zaidi alishikilia tu vizuri bastola yake kama sehemu ya ulinzi kwake juu ya yule dereva ili asije kumwingiza maboya na kumkamatisha kirahisi

"Mkuu hatujampata naona tunahitaji mikakati pamoja na backup kubwa kumnasa" ilisikika sauti ya mwanajeshi mmoja akimuelekezea Steven ambae alikua nje ya jeep moja la kijeshi.

"Sawa yule mwanamke hawezi kutusumbua sana pandeni twende maana picha zake tunazo tutampata tu" steven alijibu vile na kuwafanya wenzie wapande huku safari ikianza kuelekea kambini.

Ndani ya mwendo wa dakika 5 gari lile aina ya toyota fortune nyeupe lilisimama katika sheli moja ya mafuta na kutulia.

"Sasa utaenda kunichukulia dawa za kupunguza maumivu pamoja na mikasi miwili midogo ya kushonea kidonda bila kusahau spirit bandeji na pamba pakti moja, lakini duka la dawa naliona lina vioo usijaribu kukaa pembeni ya vioo ila kaa kwenye kioo ili kusudi niweze kukuona na sitanii kwenye hili" aliongea vile binti huyo kwa sauti ya amri na kumfanya dereva kuitikia kwa kichwa kua alikua kaelewa.
"Haya shuka taratibu" aliongea mdada yule huku nae akishuka huku bastola ikiwa mbele ya dereva yule.

"Wale nao wanamichezo gani tena" ilisikika sauti ya askari mmoja akimuelekezea mwenzake ambao hawa walikua ndani ya gari lao pale njiani wakipita kwa mwendo wa kawaida.

"Mbona kama huyo mdada aliesimma nyuma kuna kitu kama amekishikilia hivi" askari mwenzie nae aliongea huku akisimamisha gari lile na kubaki wakiwatizama yule mdada pamoja na dereva.

"Em ngoja niwasogelee" aliongea askari aliekua siti ya abiria huku akifungua mlango ule na kushuka chini taratibu.

"Em simama kwanza usitembee" aliongea mdada yule hasa baada ya kuona katika kioo cha nje ya gari lile, askari mmoja akiwafuata pale walipo kuwepo.

Je itakuaje askari yule akiwakuta wawili hao hasa mdada ambae licha ya kua bado hatujamjua jina lake ila ni mdada ambae mkononi mwake ameshikilia bastola.

Je atasalimika kweli mbele ya askari huyo ambae anawasogelea walipo ama atapambana.

Basi usikose sehemu ijayo nayo itakua sehemu ya tatu
Cha msingi ewe msomaji fanya tu kulike share na comment yako juu ya kipande hiki cha pili ili tuweze kujua kama tuko pamoja
Kumbuka huu ni mwanzo mwanzo wa sinema letu mambo ni 🔥 🔥 🔥 huko mbele
 
Ahsante best wingi wa koment zenu ndio ujio wa episode zijazo nafurahi kusikia hivyo
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…