Story yako nimeipenda, nimeisoma kwa mfululizo, umeileta vizuri, sio kama wale analeta leo kipande halafu anasema subirini baada ya siku tatuNawatakia maandili mema ya Mwaka Mpya 2018
Tafadhali Mkuu hii adithi niyakweli?je kama ni yakwwli nawew ndo muhusika?kama ndio pls tuambie baada ya zena kuchukuliwa wewe maisha yako yaliendaje?je ulimuoa salama mke wako yule au ilikuwaje!!!yani tunataka sasa utuelezee ilikuaje baada ya zena kuchukuliwa maana dah inaskitishaa af siaminigi mim kuwa haya mamb yapo so pls Mkuu tupee mwendelezoo wakoSEHEMU YA 69
ILIPOISHIA
Baada ya siku ile nilikaa kama wiki moja hivi nikiwatemebelea ndugu na jamaa niliopotezana nao. Siku hiyo nikiwa nyumbani kwangu saa sita usiku nikasikia mlango wa mbele unabishwa. Nikaenda kuufungua. Kwa mshituko mkubwa nilimuona Zainush binti Jabalkeys mbele ya mlango.
“Hujambo Amour” akanisalimia kwa bashasha.
Nikajikuta nikimjibu.
“Sijambo. Karibu ndani”
Zainusha akaingia ndani na kukaa sebuleni.
“Wazee wangu waliniudhi sana. Wananifanya kama mimi mtoto mdogo wakati mimi ni mtu mzima na nina maamuzi yangu”
Wakati Zainusha akainieleza hivyo ghafla wakatokea wale majini wawili walioambiwa wakimuona Zainusha ananifuata wamkate kichwa au wamkamate na kumpeleka kwa sultani wao.
Nilipowaona majini hao nikajiambia Zainusha sasa amekwisha.
Majini hao walipotaka kumvamia Zena wakiwa na majambia yao mikononi Zainusha alikurupuka akaruka upande mwingine wa sebule na kuwauliza majini hao kwa ukali.
“Mna nini nyinyi wapumbavu! Mnataka nini kwangu?”
SASA ENDELEA
“Unatuita sisi wapumbavu! Ngoja tutakuonyesha!” Mmoja wa majini hao alimwambia Zainush kwa hasira kabla ya kuliinua jambia lake.
“Tumeambiwa tukupeleke mzima au tukukate kishwa lakini sasa tutakupeleka ukiwa vipande vipande” jinni huyo aliendea kumuambia huku akimsogelea Zainush ili amkatekate.
Zainusha alipiga ukulele mkali akarudi hatua moja nyuma kabla ya kuuvuta unywele wake mmoja kutoka kichwani mwake kisha akaupulizia.
Baada ya kuupulizia unywele huo uligeuka jambia lililokuwa likimeremeta.
Akawambia majini hao kwa sauti ya kishujaa.
“Sasa njooni nyinyi niwararuerarue kama paka aliyeshambuliwa na mbwa!”
Majini hao kwanza walisita kisha ghafla walimfuata Zainush kwa pamoja wakiwa wamepunga majambia yao kwa unyenyekevu wa hali ya juu kama mtu alipigwa na baridi ya Lushoto kule Mkoani Tanga.
Zainusha aliruka upande mwingine huku akitamba na jambia lake. Alilichezesha mikononi kwa haraka haraka kabla ya kulikinga jambia la jinni mmojawapo aliyekuwa amemshushia dharuba.
Baada ya kulikinga jambia hilo Zainusha aliruka tena akamsukumia dharuba jinni huyo ambayo aliikwepa. Kwa muda wa dakika kumi Zainusha aliwakabili majini hao kama mwanaume!
Hawakuweza kumpiga hata dharuba moja japokuwa walikuwa wawili. Zainush alikuwa amefundishwa kupigana na alikuwa shujaa wa kike aliyeweza kupigana na wanaume.
Katika kulikinga jambia la jinni mmoja wapo lililoelekea kichwani mwake ndipo jambia la Zainush lilipokatika vipande viwili. Zainusha alikimbilia upande niliokuwa nimesimama nikiwa nimegwaya. Akaja nyuma yangu na kunishika shati.
“Amour wainue majini hao wataniua!” Zainusha aliniammbia kwa sauti ya huruma.
Kwa kweli nilimuhurumia lakini sikuwa na namna yoyote ya kumsaidia.
Majini hao wakamfuata Zainusha mgongoni kwangu.
“Msimuue! Msimuue!” nikawambia.
Zainusha alijaribu kuwakwepa lakini majini hao walimdaka.
Zainusha alikuwa akipiga kelele na mimi nilikuwa nikipiga kelele kuwambia majini hao wamuachie lakini hakuna aliyenisikia.
Walimbeba Zainush wakatoweka naye pale sebuleni. Sikuwaona tena.
Bila shaka walimpeleka kwa yule sulatani wao aliyewaagiza wamkamate na sijui alifanywa nini kwani tangu siku Zainush sikumuona tena.
Sikujua kama Zainush alifungwa au aliuawa. Lakini nilimkumbuka sana. Hivi sasa nimekuwa tajiri mkubwa na chanzo cha utajiri huo ni yeye.
Kuna wakati huwa najimabia nilifanya kosa kwenda kumshitaki kwa sulatani wao, bora ningemuacha tu kwa sababu nilishamzoea.
Nitakusimulia kisa kingine nitakapopata nafasi ili ujue maisha yangu yalikuwaje baada ya hapo na pia ujue kama Zainusha aliibuka tena au la.
MWISHO.
Mkuu nikweli unachosema lakin bado mim najiuliza je hi story niyakweli?kama niyakweli basi amuru atkuwa mpmbaf mana kasaidiwa sana na dem alimpnda lakin mwsho wa sik kamsaliti kwa baba ake zena hatimaye imeishiaa kwa majonz sanaStori ni mzuri sana ila huyu Amour sijamuelewa kabisa,mfano alishafunga ndoa na Shamsa ambae ni Zena na walishaishi pamoja na ukiachilia mbali amemuokoa mara nyingi sana ,sasa kama yy Binaadam ameshindwa kulitambua hilo!pia huyo tayari ni mkewe pamoja na kujigeuza kuwa Shamsa,ss kwa nini ameenda kumsaliti mbele ya wazazi wake! Mijitu mingine buana sijui ikoje
Mkuu nadhan amuru atamuoa salma cjui yule mke wake maana hakumpa talaka¡!!ila tunatka kujua maisha ya amuru baada ya zena kuchukuliwa nawale majin wenzakee!!je alirud tena au vip ?kama alirud vip walioana na amuru?kama hapana ilikuuwaje sasa maisha ya amuru??japo imeishia kwa huruma mana nmemwonea huruma sana zenaStory nzuri muda wote nimeshikilia simu tangu saa tisa uuwi. Sasa amour aliishia kumuoa nani baada ya Zena kuchukuliwa.
Story hii inaendana na jini uliyezaa nae au ?![]()
SEHEMU YA 1
Sitausahau mwaka elfu moja mia tisa na sabini na nane. Nina sababu tatu za kutousahau mwaka huo. Sababu ya kwanza ni kuwa kulitokea vita vya Kagera. Majeshi ya Iddi Amin aliyekuwa Rais wa Uganda yalivamia nchi yetu na kusababisha maafa makubwa.
Kaka yangu wa kwanza alikuwa ni miongoni mwa askari waliokuwa mstari wa mbele waliokwenda kuikomboa nchi yetu na aliuawa katika vita hivyo.
Sababu ya pili ya kutousahau mwaka huo ni kuwa ndio mwaka nilioanza kufanya kazi. Niliajiriwa na kampuni ya STC iliyokuwa na maduka ya ushirika nchi nzima. Na mwaka huo pia ndio nilitimiza umri wa miaka ishirini.
Lakini sababu ya tatu na iliyokuwa kubwa zaidi ya kutousahau mwaka huo ni kuwa nilikutana na tukio ambalo lilibadili maisha yangu.
Je lilikuwa tukio gani?
SASA ENDELEA
Ilikuwa februari 18 mwaka 1978. Nilikuwa mmoja wa wafanyakazi wa STC tuliokopeshwa pilipiki. Furaha yangu ikanituma kwenda kuangalia sinema. Wakati huo hakukuwa na video wala televisheni. Kulikuwa na majumba ya sinema. Kwa pale Tanga nilikokuwa naishi kulikuwa na majumba matatu ya sinema.
Kulikuwa na Majestic Sinema, Novelty Sinema na Regal Sinema. Majestic Sinema ndiyo iliyokuwa kubwa na maarufu zaidi na ilikuwa katikati ya jiji.
Mimi nilikuwa mpenzi sana wa filamu za kihindi. Filamu za kihindi zilikuwa zikioneshwa siku ya jumapili tu, yaani mara moja kwa wiki na zinakuwa zinajaza watu kuanzia wahindi wenyewe hadi waswahili.
Tikiti huanza kukatwa tangu asubuhi. Ukienda jioni hupati kitu. Nakumbuka filamu iliyokuwa inaoneshwa siku hiyo iliitwa Dost, ilikuwa filamu ambayo nilishapata sifa zake, hivyo kutokana na furaha ya kupata pikipiki nikaona niende nikaione.
Pikipiki tulikabidhiwa siku ya jumamosi, siku ya jumapili ndio niliamua kwenda kuitazama filamu hiyo ya Dost.
Nilikwenda na pikipiki yangu hadi Majestic Cinema. Nikaiegesha katika eneo la kuegesha na kwenda kupanga foleni. Nilikuta foleni ndefu ya watu waliokuwa wanakata tikiti.
Nilifika hapo saa nne asubuhi. Mpaka nafika kwenye kidirisha cha kukata tikiti ilikuwa saa tano kasorobo. Mbele yangu kulikuwa na watu watatu. Wakimalizika wao kukata tikiti ndio inafika zamu yangu. Akaja msichana mmoja ambaye alikuwa amevaa baibui na hijabu akaniomba nimkatie tikiti.
Ilikuwa ni kawaida mtu kukufata ukiwa kwenye foleni na kukuomba umkatie tikiti. Hivyo sikushngaa msichana huyo ambaye sikumfahamu aliponiomba nimkatie tikiti.
Alikuwa anataka kunipa pesa nikakataa kuchukua pesa yake.
“Nitakukatia kwa pesa yangu kisha utanipa” nikamwambia.
“Asante kaka yangu”
Alikuwa na sauti nzuri ya kusisimua.
Wakati amebaki mtu mmoja mbele yangu, kundi la vijana wakihuni likavamia pale kwenye kidirisha na kuharibu foleni, ikawa vurugu. Mmoja wa vijana hao alinibana na kunikatia vifungo vya shati langu. Nikajaribu kutumia nguvu mpaka nikafanikiwa kukifikia kidirisha, nikakata tikiti mbili za usiku.
Nikazitia mfukoni tikiti hizo kisha nikaanza kumtafuta yule kijana aliyeniumiza. Nikamuona akiuza tikiti yake kwa bei ya juu kwa mhindi mmoja. Nikamkwida ukosi na kumtikisa.
“Wewe mshenzi umenifanya nini pale?” nikamuuliza.
“Hebu niache fala wewe…” akaniambia huku akiukutua mkono wangu.
Nikamtandika ngumi moja tu iliyomtupa chini. Damu ikawa inamtoka mdomoni.
Yule msichana aliyeniomba nimkatie tikiti akanifuata haraka.
“Usipigane” akaniambia huku akinishika bega.
“Angalia jinsi alivyokata vifungo vyangu”
Nikamuonesha yule msichana papi za shati langu ambalo lilichomoka vifungo vitatu.
“Basi muache”
Yule kijana alinyanyuka na kukimbia.
Nilitoa zile tikiti mbili, nikampa tikiti moja yule msichana.
“Asante kaka yangu, ngoja nikupe pesa zako” akaniambia.
Nikaona nimuachie tu.
“Basi usinipe pesa, nimekukatia kwa pesa zangu”
“Kwnini unakataa pesa?” akaniuliza.
“Nimekukatia mimi kama zawadi yako”
“Asante kaka yangu”
“Haya, kwaheri” nikamuaga.
“Basi tutaonana jioni” akakiambia kichogo changu. Nilikuwa nimeelekea kwenye mlango nikitoka.
Nikiwa nje ya jumba hilo nilichukua pikipiki yangu nikaondoka kurudi nyumbani.
Nilikuwa ninaishi eneo la Mabawa kwenye nyumba ya kupanga. Nyumba yenyewe ilikuwa na sehmu mbili. Sehemu moja nilipangisha mimi na sehemu nyingine alipangisha kujana mmoja wa kichaga aliyekuwa akifanya biashara ya duka la nguo barabara ya kumi na tatu.
Nilipofika nyumbani niliingiza ndani pikipiki yangu nikakaa sebuleni kwangu na kutafakari.
Nilikuwa sijaoa, sikuwa na mke wala mtoto. Ndiyo nilikuwa naanza maisha. Wakati huo mzazi wangu aliyebaki alikuwa mmoja, ni mama yangu. Baba yangu alikuwa ameshafariki dunia miaka miwili iliyopita.
Mama yangu alikuwa akiishi barabara ya tisa kwenye nyumba yetu tuliyozaliwa. Kaka yangu wa pili alikuwa akiishi eneo la Chuda na kaka yangu mwingine aliyefuata alikuwa akiishi eneo la Kwaminchi.
Usiku ulipowadia nilitoa pikipiki yangu nikaenda kwenye mkahawa mmoja kula chakula kisha nikaongoza njia kuelekea Majestic.
Nilifika Majestic saa mbili na nusu. Sinema ilikuwa inaanza saa tatu hadi saa sita usiku. Baada ya kuegesha pikipiki yangu niliingia kwenye ukumbi huo nikatafuta siti yenye namba yangu nikakaa. Mpaka imebaki dakika moja kuanza trela, siti ya upande wangu wa kulia ilikuwa tupu. Nilishuku ilikuwa siti ya yule msichana niliyemkatia tikiti kwani siti hizo zilikuwa zikifuatana na namba zilizomo kwenye tikiti.
Ghafla taa zikazimwa na trela ikaanza. Hapo ndipo nilipomuona msichana akiingia na kuja kukaa kwenye kile kiti kilichokuwa kitupu. Alikuwa ni yule msichana niliyemkatia tikiti. Sikujua alijuaje kuwa kiti chake kilikuwa pale. Nikawaza kwamba pengine aliwahi kuingia mapema akakiona kiti chake kisha akatoka.
“Tumekutana tena” akaniambia huku akitabasamu.
“Nilikuwa najiuliza huyu msichana yuko wapi”
“Nilichelewa kidogo, unajua ninaishi mbali”
Sikumuuliza anaishi wapi, akili yangu ilikuwa kwenye ile trela iliyokuwa ikioneshwa.
Sote tukawa kimya. Tuliangalia trela hadi ikaisha. Msichana alitoka, mimi sikutoka. Baada ya muda kidogo alirudi akaketi kwenye kiti chake. Mkononi alikuwa ameshika chupa mbili za soda na pakiti mbili za karanga.
“Chukua soda” akaniambia huku akinipa ile chupa moja.
Nikaipokea.
“Chukua na karanga”
Akanipa na pakiti moja ya karanga.
“Asante’
Hapo hapo taa zikazimwa na filamu ya Dosti ikaanza. Ile filamu ilikuwa ikizungumzia marafiki wawili, mmoja kipofu na mwingine mlemavu wa miguu. Ilikuwa filamu nzuri na ya kusikitisha sana. Ilikuwa na nyimbo nne. Nyimbo tatu ziliimbwa na muimbaji maarufu wa India Mohamed Rafiy ambaye kwa sasa ni marehemu na moja iliimbwa na Usha Mangesh ambaye ni dada wa Lata Mangesh.
Sinema ilipomalizika tuliinuka kwenye viti na kutoka. Kwa vile kulikuwa na watu wengi, nilipotoka sikumuona tena yule msichana, nikaenda kuchukua pikipiki yangu nikaiwasha na kuondoka.
Kutoka Majestic Cinema nilishika barabara ya Eckenford hadi bustani ya Uhuru ambapo nilikata kushoto na kushika barabara ya Pangani. Wakati nalivuka eneo la Tangamano niliona mtu akinipungia mkono mbele yangu. Alikuwa mwanamke na nilihisi likuwa anataka kuniomba lifti.
Kusema kweli muda ule wa usiku nilikuwa sipakii mtu nisiyemfahamu hata kama ni mwanamke. Kwa hiyo nilitaka kumpita lakini pikipiki ikazimika moto ghalfa. Mwanamke huyo akaona nilisimama kwa ajili yake, akanifuata.
Alipofika karibu yangu nikaona alikuwa ni yule msichana niliyekuwa naye sinema. Nikajiuliza alifikaje pale wakati nilimuacha kule Majestic?
MAMBO YAMEANZA. JE NINI KITATOKEA? USIKOSE KUENDELEA NA MKASA HUU WA KUSISIMUA MWANZO HADI MWISHO.
Mkuu naikumbuka hiyo sinema ilikuwa inaitwa Dostana.![]()

Hiyo no hadithi tu sidhani kama no ya kweli nilishaisoma kwenye gazeti LA sani mwaka 2006 yeye kaifupisha tu wala hajamalizia hadithi yote, kwa faida ya wengi ni kwamba baada ya zena/zainush kukamatwa Na wale majini alipelekwa kwa sultani Na alihukumiwa kifungo cha milele ndani ya chupa kisha ikatoswa baharini, Amour hakuoa mke tena wala kurudiana Na salma bado ila alijilaumu kwa kumkosa msichana aliuyemtajirisha kwa vile alikuwa jini, alipata utajiri mwingi akajenga hotel kubwa sana akaamua kuiita zainush hotel ili kumuenzi zena. Baada ya miaka kadhaa kuppita mvuvi mmoja akiwa anavua samaki katika pwani ya mji WA tanga alivua kitu kama chupa au mkebe ambao aliupeleka nyumbani kwake, hiyo chupa ndio zena aliwekwa Na sultan kama adhabu ya kifungo bila kijua kilichopo ndani binti WA yule mvuvi akafungua ile chupa Na zena akaganikiwa kutoka akiwa mzima akamshukuru yule binti kisha akamuahidi kumlipa fadhila. Baada ya hapo break ya kwanza akaenda kwa mpenzi wake armour akamkuta yuko vizuri tajiri Na hajaoa bado .Kwa upande WA amour alimpokea zena kwa Furaha sana baada ya zena kumsimulia mkasa uliompata. Pia alishangaa sana ile hotel aliyoijenga armour Na kuipa jina lake. Mapenzi yakawa motomoto zena hakurudi kwao hadi aliletewa habari za msiba WA yule sultani aliyempa adhabu. Baadae zena alimwambia armour wazae mtoto lakini isingewzekana kuzaaa Na zena kwa sababu alizozitoa yeye zena mwenyewe Ila akamwambia amour atamtafutia mke mwenza yeye mwenyewe ambaye ni binadam mwenzake. Ndipo alipomchukua yule msichana aliyemfungulia ndani ya chupa akalipia mahari kisha amour akamuoa kama mke mdogo. Ni hayo tu kwa ufupiTafadhali Mkuu hii adithi niyakweli?je kama ni yakwwli nawew ndo muhusika?kama ndio pls tuambie baada ya zena kuchukuliwa wewe maisha yako yaliendaje?je ulimuoa salama mke wako yule au ilikuwaje!!!yani tunataka sasa utuelezee ilikuaje baada ya zena kuchukuliwa maana dah inaskitishaa af siaminigi mim kuwa haya mamb yapo so pls Mkuu tupee mwendelezoo wako
Asante Mkuu sasa ndonimeamini kuw hizi ni fiction tu hakuna maisha ya rahisi kiasi hicho dunia hiiHiyo no hadithi tu sidhani kama no ya kweli nilishaisoma kwenye gazeti LA sani mwaka 2006 yeye kaifupisha tu wala hajamalizia hadithi yote, kwa faida ya wengi ni kwamba baada ya zena/zainush kukamatwa Na wale majini alipelekwa kwa sultani Na alihukumiwa kifungo cha milele ndani ya chupa kisha ikatoswa baharini, Amour hakuoa mke tena wala kurudiana Na salma bado ila alijilaumu kwa kumkosa msichana aliuyemtajirisha kwa vile alikuwa jini, alipata utajiri mwingi akajenga hotel kubwa sana akaamua kuiita zainush hotel ili kumuenzi zena. Baada ya miaka kadhaa kuppita mvuvi mmoja akiwa anavua samaki katika pwani ya mji WA tanga alivua kitu kama chupa au mkebe ambao aliupeleka nyumbani kwake, hiyo chupa ndio zena aliwekwa Na sultan kama adhabu ya kifungo bila kijua kilichopo ndani binti WA yule mvuvi akafungua ile chupa Na zena akaganikiwa kutoka akiwa mzima akamshukuru yule binti kisha akamuahidi kumlipa fadhila. Baada ya hapo break ya kwanza akaenda kwa mpenzi wake armour akamkuta yuko vizuri tajiri Na hajaoa bado .Kwa upande WA amour alimpokea zena kwa Furaha sana baada ya zena kumsimulia mkasa uliompata. Pia alishangaa sana ile hotel aliyoijenga armour Na kuipa jina lake. Mapenzi yakawa motomoto zena hakurudi kwao hadi aliletewa habari za msiba WA yule sultani aliyempa adhabu. Baadae zena alimwambia armour wazae mtoto lakini isingewzekana kuzaaa Na zena kwa sababu alizozitoa yeye zena mwenyewe Ila akamwambia amour atamtafutia mke mwenza yeye mwenyewe ambaye ni binadam mwenzake. Ndipo alipomchukua yule msichana aliyemfungulia ndani ya chupa akalipia mahari kisha amour akamuoa kama mke mdogo. Ni hayo tu kwa ufupi