FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 2,229
- 4,345
THE JOURNALIST (TONE LA DAMU)
AMANI KILONZO!!!!!...
Ni jina ambalo lilikuwa alama ya ushindi, lilikuwa ni jina maarufu ambalo kila mwandishi wa habari pamoja na waandishi wote walikuwa wakilichukulia kama jina la mfano.
Jina maarufu kutoka kwa mwanaume aliyetokea kwenye maisha ya kimasikini haswa, familia ambayo haikuwa na uhakika hata wa kula mlo mmoja tu ndiye ambaye alikuwa shujaa wa habari Tanzania. AMAN KILONZO alizaliwa yeye na dada yake tu EPIPHANIA KILONZO.
Mwanaume huyu alikuwa mwandishi wa habari za kiuchunguzi, mzalendo na mtu aliye lipenda mno taifa lake hivyo hakuwa tayari kuvumilia ushenzi na ukatili wa mamlaka jambo ambalo lilipelekea yeye kuripoti na kudai alikuwa na ushahidi wa mauaji ya watu ishirini na sita ambayo yalifanyika ndani ya hifadhi ya taifa ya Mikumi, Morogoro.
Hiyo ilikuwa safari nzuri ya kufa kwake kwa sababu nyuma ya hayo, kulikuwa na Siri nzito ambazo hakupaswa kuwa nazo ila kwa bahati mbaya alizipata. Alishuhudia mdogo wake akiwa mfu, mwanamke asiye na nguo hata moja kwenye mwili wake baada ya kubakwa. Kama kaka aliapa kuwashughulikia wale wote ambao walihusika na ushenzi huo ila kwa bahati mbaya hata yeye baada ya hapo hakuwahi kuonekana tena mpaka ulipo okotwa mwili wake.
Kupotea kwake kulianzisha safari nyingine ya mwandishi WILLIARD NZITU ambaye aliandika kitabu kiitwacho TONE LA DAMU, kitabu hicho baada ya kutoka tu kilipigwa marufuku na serikali na wale wote ambao walikinunua waliuawa lakini kuna mtu mmoja alifanikiwa kubaki na nakala moja akaificha vizuri kwa siri.
Sababu za kufungiwa kitabu hicho ni Williard kuandika siri za mambo ambayo yalifanya role model wake AMAN KILONZO kuweza kuuliwa hivyo hata yeye hakuwa Salama kwa watu hao. Uhatari ambao aliutengeneza ulikuwa mbaya kwake, jina lake lilikuwa zaidi ya kirusi hivyo hata yeye alitakiwa kupotezwa.
Baada ya waandishi hao wawili nguli kupotea, ilipita miaka mitano ndipo akaibuka mwandishi mwingine, bwana huyu alitafutwa na watu wasio julikana ambao walimpatia siri nzito ambazo zingemfanya kuingia kwenye maisha ya hatari tofauti na yale aliyokuwa anayaishi mwanzo. RASHID MAZINDE ndilo lilikuwa jina lake, alikuwa mwanaume mmoja mstaarabu sana, mtu wa MUNGU sana ambaye aliishi akiitegemea Kalamu yake hivyo hakuwa na makuu na mtu.
Lakini habari mbaya ni kwamba bwana huyo alidaiwa kuwa na kurasa ambazo zilitisha kwenye maisha yake. Kurasa za maisha yake ya nyuma alikuwa amezizika na hakuna binadamu ambaye alikuwa hai alikuwa anazijua kwa imani yake yeye. Rashid Mazinde alidaiwa kuhusika kwenye mauaji ya watu zaidi ya mia-tano wakiwemo matajiri wakubwa duniani mia-moja lakini hakuna mtu alikuwa anazijua kurasa hizo.
Sasa hao ambao walimtafuta walizijulia wapi? Hizo siri kwanini walimpa yeye na walitaka azifanyie nini? Zilihusiana vipi na mwandishi wa habari za kiuchunguzi AMAN KILONZO?
Huyu ndiye binadamu ambaye anaenda kutulia muda wetu kuweza kuzigusa hizi kurasa tujue kuna nini ndani yake....
Simulizi hii inaitwa THE JOURNALIST (TONE LA DAMU)....karibu tuone namna hilo Tone La Damu linavyo husiana na huyo mwandishi.
Simulizi hii ina mengi ya kukufunza kwenye maisha unayo ishi hususani kwenye mazingira ya kisiasa hivyo ISOME kwa utulivu uielewe...
Usiishie tu kufurahia mapigano, storyline kali Wala dialogue kali sana bali elewa na content yake utaenjoy zaidi.
NB
Hii ni simulizi ya kubuni tu na kufikirika, haihusiani na mtu yeyote, mamlaka yoyote Wala taasisi yoyote hivyo ISITAFSIRIWE TOFAUTI.
Majina ya mahali na watu yamewekwa ili kutia uhalisia kwa wasomaji wake.
Unaweza kunicheki WhatsApp kwa namba +255621567672
Au kwa email thomasibabuya@gmail.com
Langu jina FEBIANI BABUYA
Wasalaam.