Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Ndugu zake wamesimulia tabia yake na kilichotokea siku ya tukio.
Mazishi yake yanasubiri kuwasili kwa wazazi wake, ndugu na jamaa kutoka mkoani Geita. Marehemu ameacha watoto watano, wa kike wawili na wa kiume watatu, ambao alizaa kabla ya kutengana na mume wake.
Mwajiri wa dada huyo, Anna Kasanda, akizungumza jana na Nipashe nyumbani kwake, Ukonga Mombasa kwa Fundi, jijini Dar es Salaam ambako msiba huo uko, alisema asubuhi baada ya kuamka, Mabuga alikuwa anafanya kazi zake na siku ya tukio aliomba amtumie fedha mama yake mzazi aliyeko Geita.
"Nilipotoka nilimtumia pesa mama yake, ambaye ni shangazi yangu, sababu tuna undugu, nilituma majira ya saa 2:30 asubuhi, na nikatoa taarifa nimeshatuma," alisema Kasanda.
“Hakuwahi kubadilika wala hakuwa na ugomvi. Alikuwa mwenye furaha kila siku, nimeshangaa tukio hili. Huwa namtania dada hapa mbona hujafanya hili, sielewi," alisema Kasanda.
Shangazi asimulia
Akisimulia tukio hilo, Mary Kasanda alisema hafahamu hadi sasa sababu ya kifo cha ndugu yake huyo.
"Yeye ni mtoto wa kwanza kwa mama yake. Tuna undugu na mama yake marehemu, ni dada yangu tena baada ya kutumwa pesa kwa mama yake akasema zitasaidia kununua nguo za mwanawe (wa marehemu)," alisema Mary.
"Nilipoondoka nilimuaga nikaenda kuchukua mtoto. Niliporudi niliita Tina, Tina… tena kwa sauti ya ukali nikajua anafanya makusudi maana tulikuwa tunataniana. Lakini hakuitika baadaye nikasikia sauti ya kukoroma, nikasema ngoja nizungukue nyuma," alisema.
“Nikachungulia dirishani nikaona damu, kuangalia pembeni nikaona mwili na kisu pembeni mguuni, akiwa amelalia kifudifudi, nikapiga kelele majirani wakaja kwa muda mfupi," alisema Mary.
Baada ya tukio
Mary anasema alitumia simu ya marehemu kupiga ili kutoa taarifa, ambayo aliiacha mezani kabla ya kwenda kumchukua mtoto, kwa kuwa simu yake ilikuwa imezima.
Alisema walipoomba msaada wa gari na kumpakia, walianza kwenda kituo cha polisi Ukonga Mazizini kutoa taarifa na kisha hospitali ya Amana ambako walisema kwa kesi kama hizo wampeleke (marehemu) Muhimbili.
"Kabla sijaenda kumchukua mtoto, nikatoka kwanza kwenda dukani nikarudi na soda moja, akanilaumu kwa nini nimerudi na soda moja. Baada ya muda nikaitwa na jirani yangu dirishani, nikatoka huku nikiwa nimeacha soda nusu, niliporudi ndani sikuikuta, akawa ameinywa yote... akasema bora ulivyoondoka maana ulininyima soda, nimeinywa," alisema Mary.