FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 2,229
- 4,345
Kwenye huu ulimwengu wa mabavu kuna mambo mengi yanatokea kiasi kwamba wanadamu tunakimbilia kulaumu bila kujua sababu ya mambo hayo kutokea.
Kwenye IDAIWE MAITI YANGU uliisoma historia na chimbuko la binadamu hatari sana GAVIN LUCA. Bwana huyu historia yake ilianzia huko Tanga ambapo kuna kijana mmoja alishindwa kumuoa mwanamke ambaye alimpenda sana kwa sababu hakuwa na Mali, alikuwa maskini wa kutupwa.
Hilo lilimfanya kufanya maamuzi magumu ya kulikimbilia jiji la Dar es salaam kutafuta maisha. Baada ya kufika huko mambo hayakuwa vile alitarajia ikamlazimu kujiunga na magenge ya uuzaji wa dawa za kulevya.
Kijana huyo akaja kusumbua sana mpaka akafanikiwa kumuua kiongozi wa watu hao kutoka Mexico ambapo akaja kuwa ndiye kiongozi wa mitaa ya PEENUGA STREETS na mwisho wa siku akaja kujenga mji wake wa LUCAS VILLA baada ya kuwa na ukwasi wa kutosha.
Bwana huyo baadae alikuja kumuoa kwa Siri mtoto wa waziri mkuu wa Tanzania na ndipo historia ya GAVIN LUCA ikazaliwa baada ya watu hao wawili kupata watoto mapacha. Bwana huyu alitupatia mambo ya kutisha mno ambapo alikuwa analipa maisha ambayo aliyaishi baba yake tangu siku atoke Tanga kwenda Dar es salaam.
Mambo yalionekana kuisha na GAVIN LUCA akaja kupotea ikidaiwa kwamba amekufa na hapo ndipo tukaipata sehemu ya pili ya IDAIWE MAITI YANGU ambayo inaitwa THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA-LIONELA yaani SAFARI YA GAVIN LUCA. Humu tulimsoma kwa undani LIONELA, mtoto wa damu na wa pekee wa GAVIN LUCA ambaye alianza kutafutwa na watu ambao walikuwa masalia na makosa ya baba yake kuwaacha hai.
LIONELA alipambana na watu hao baada ya kuwa mkatili kupita kiwango cha mwanadamu wa kawaida naye akaamini kwamba alimaliza kazi na ndipo akaamua kuolewa kabisa kwa ajili ya kwenda kuishi maisha ya kawaida na ya amani lakini haikuwa hivyo.
NANI ALIKWAMBIA MWANADAMU WA HIVYO ANAWEZA KUPUMZIKA KIRAHISI? Mwisho wa andiko hilo ilionekana harufu ya usaliti kutoka kwa mwanaume ambaye alimpenda sana kwa maisha yake yote na akampa maisha.
Sasa kulikuwa na sababu zipi za bwana JABARI kufanya hayo mambo? Alikuwa ni nani haswa mpaka amsaliti mwanamke na familia ambayo ilimpa maisha baada ya kukataliwa na kila mtu? JABARI alikuwa na historia ndefu ya maisha yake na aliapa kwamba ni lazima aiteketeze familia hiyo kwa gharama yoyote ambayo ingekuja mbele yake bila kujali kwamba yeye na mwanamke huyo walikuwa na mtoto tayari naye akiwa kama baba wa familia.
Sasa kwenda kuyajua maisha ya JABARI ndipo tunatakiwa kulisoma andiko hili tuweze kuelewa kulikuwa na nini hasa? Walimkosea wapi kwenye maisha ya nyuma! Yeye alikuwa ni nani na kwanini alikuwa anayafanya hayo? .....
LIONELA na familia yake watapona kutafunwa na mtu ambaye ndiye mume wa bosi mwenyewe na anaaminika kuliko watu wengi ndani ya familia? OTHMAN CHUNGA atahusika vipi kuisaidia familia na mtoto ambaye aliachiwa na bosi wake GAVIN LUCA amchunge kwa gharama ya maisha yake?
Ili kupata majibu yote haya ndiyo sababu ya msingi ambayo imenifanyia leo nikuletee andiko hili ambalo ni season 3 na sehemu ya mwisho kabisa ya collection hii...
Simulizi inaitwa THE DARKNESS OF AN ANGEL - SIKU ZA MWISHO waweza kuita GIZA LA MALAIKA.
Waite marafiki, ndugu na wasomaji wote ili tuweze kujua ni MALAIKA yupi huyo ambaye anatuletea hilo Giza?
Nyuma ya kalamu nipo mtaalamu mwenyewe FEBIANI BABUYA ✍️
NIPE MUDA WAKO........ DIVE IN 👇