Simulizi: Sihusiki

Karibuni...

CC Litro Daudi Mchambuzi The Hurricane Jael brucella moneytalk saneneto Affet dluv FabreG ndulle Morgan Freeman unprejudiced Mshana Jr Heri Zabron Hamis kisukari totopack lanyese maubusu Minja Ngalason positive is normal Mine eyes popie Mr no bioto yona raphael Bigjahman nyakisese Tanayzer Shupavu Ngoheranga kilambon renason ADK Makandila9090 General Galadudu Said Cosmetics SnowBall binti mapozi kingkimwe BILLIONAIRE 2025 Badar_01 kanonb bweke undeceivable Marcie KigaKoyo Justine_Dannie sir ide Verifier dokta lu langoni makedonia Kudo Queen M jonoma Sangomwile Lovekid The Planner Mbobo Jenseny Shunie Rosicky Drizzle nabali Secret genius mkulima2 mkulungwa02 Breki ya Kenge EnnoMX Galbi Siratheboy irumba1 mjingamimi TAUNO KIDUDU orturoo Mavindozii Sky Eclat Vangigula seeker of knowledge PapaaSide bardizbah Nascent richard Mzimu wa Kolelo boscop kawoli song 16 Mjep asan njau Silencer Kimatu hambiliki mwanangu Sigara Kali The Wolf Melvine Royal Son Edward A chapa chichiboy1 Scofied EINSTEIN112 Oyaaa majomba mwera hao Katavi Semere92 tokenring ilu Wand Mtoto halali na hela dan oseko Jovet Panel Matumbwela saadatmontana Forgotten MAWAZO UJENZI Masking Agent Madame S Stephen Chelu bouy saleh Rukube Covid nineteen marybaby Mama mimi Mlume ndagu kinjeboy Lubebenamawe FabreG Zion jrGong Marley pirate Careem ndulle FabreG Tajiri mpole BETONY manumbu1 dluv saneneto aramika kiletza Shupavu nsharighe Kambaku Iammoshyn song 16 Affet unprejudiced Agent007 enjai ya kyasha Edward A chapa dendaboy Req pwiro aggyd brucella Lengutee nyakisese mtume wawatu mr chopa The Hurricane Puppy Restless mpwisa kikoozi Mirlz B Matthew ASA 1 ndulle Tanayzer sawima manji h kawoli
 
Shukran mkuu.
 
uwiiiii ya lini hii asante mkuu vitu ni vyenyewe sana hivi
 
SIHUSIKI - 19



ILIPOISHIA...

"Simu kutoka kwa Kamanda wa Polisi Tanga? Kuhusu nini shemeji?"

"Ni masuala yetu tu haya ya unyanyasaji wa kijinsia. Kuna kesi fulani nimeanza kuifuatilia... Huyo baba Hellen yuko karibu hapo?" Kabla ya kujibu Andrew alijiuliza maswali kadhaa bila majibu na kusababisha Salome amuulize kulikoni amebaki kimya.

"Shemeji kuna mtu ananisemesha hapa na mimi nikawa namsemesha kwa ishara... Kuhusu baba Hellen kapata matatizo kidogo ndio maana nimekupigia."

"Matatizo? Kuna nini shemeji, mbona umenishitua hadi nasikia moyo ukinienda mbio."

"Usiwe na wasiwasi shemeji. Ni matatizo ya kawaida tu."

"Enhe, ni yapi shemeji."

"Aah ni kwamba, Malima amekamatwa na polisi."

"Amekamatwa na polisi? Kivipi?"


SASA ENDELEA...

"Sababu za kukamatwa kwake bado sijazifahamu kwa kweli. Hivi ninajiandaa kwenda polisi kumwona."

“Shemeji una hakika Baba Hallen amekamatwa?” Aliuliza tena.

“Ndiyo shemeji.”

"Yuko kituo gani?" Aliuliza baada ya kukaa kimya kwa muda.

"Central."

"Basi nikitoka hapa nitapitia huko kituoni. Asante kwa taarifa."

* * *

Andrew alitafuta eneo la kuegesha gari lake dogo baada ya kuwasili katika kituo kikuu cha polisi. Tangu ametoka ofisini njiani alikuwa anajiuliza maswali mengi kuhusu namna polisi walivyoweza kumfahamu Jackson na kumkamata. Sasa alihisi kwamba huenda katika hoteli aliyofikia Jackson kulikuwa na kamera za ulinzi (CCTV) zilizotumika na kuwawezesha kumkamata.

Alikumbuka jinsi Jackson alivyojitoa yeye na mkewe katika kuokoa ndoa yake baada ya mkewe kuanza kudai talaka kwa sababu ambazo hata hazikuwa na kichwa wala miguu. Aliona pia atumie muda huo kujadiliana na Jackson namna nzuri ya kukabiliana na mkewe ambaye aliahidi kuja kumtembelea polisi baada ya kuwasiliana na ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga kama alivyoahidi.

Baada ya kuacha gari mahala salama na kuingia katika jengo la polisi, aliomba kuonana na Jackson. Polisi wakamkubalia. Jackson alipojulishwa kwamba kuna mgeni anayeitwa Andrew Mambo alitaka kuonana naye, alimjibu askari kwamba hakuwa tayari kuonana naye. Wakati yule askari anageuka kuondoka, Jackson akamwita tena kwani aliona hakukuwa na sababu ya kutokutana naye na pengine huo ulikuwa wakati mwafaka wa kumweleza anavyomtuhumu kwa kumsaliti.

“Samahani ndugu kwa usumbufu. Mwambie tu aje kuniona,” alisema kwa upole.

"Karibu Mambo. Nini kimeendelea ofisini kwa sababu nimesikia bodi imemteua Mapunda."

"Nilitegemea niwe wa kwanza kukufikishia hizi habari ambazo zimewaudhi wafanyakazi wengi. Yaani kuna ambao morali ya kazi imewaisha hadi wakaamua kuondoka kazini kwa hasira."

"Lakini bila shaka kuna waliofurahia pia, hasa kukamatwa kwangu."

"Uvumi ulianza kuzagaa kwamba umekamatwa lakini nimejitahidi kuuzima.”

“Nashukuru kwa hilo lakini Mr Mambo, unadhani polisi wamekuja kunikamata hivi hivi tu? Labda kama walipiga ramli kwa mganga wa kienyeji! Huoni kama kuna mtu anayenisaliti na ambaye anaijua vyema hii issue?”

“Hata mimi njia nzima wakati ninakuja hapa nilikuwa ninajiuliza kuhusu hilo.”

“Lakini wanaojua suala hili ni mimi na wewe. Lazima mmoja wetu ndiye atakuwa kawaita polisi. Nasema uongo?”

"Haiwezekani iwe mimi au wewe. Nimepata hisia kwamba huenda katika nyumba hiyo ya wageni uliofikia kuna kamera za ulinzi, CCTV. Hukuona kitu kama hicho?"

"Andrew unaleta hadithi gani? Yaani kile kijigesti kiwe na kamera za aina hiyo? Anyway, kwa kujibu swali lako hakuna kitu kama hicho."

"Unajibu kwa hisia tu au kweli ulichunguza ukaona hakuna kamera hizo?"

"Sikujisumbua hata kuchunguza na ninaamini kwa asilimia mia moja kwamba hakuna kitu kama hicho. Labda tujaalie kwamba zilikuwepo, unadhani kama ndivyo ingekuwa haraka hivyo kunikamata. Yaani tukio linatokea Ijumaa halafu leo Jumanne nakamatwa. Huoni ni muda mfupi mno kwa polisi wetu kuweza kuchakata picha za kamera, kutafuta mtuhumiwa hadi kumkamata? Na kumbuka Jumamosi na Jumapili hazikuwa siku za kazi na kwa hiyo kama ni kazi wamefanya jana."

"Umejibu vyema kwamba hukuchunguza lakini kwa tukio kama lile polisi wanaweza kufanya kazi usiku na mchana hadi kumnasa wanayemtafuta. Tuseme wewe unatuhumu kwamba mimi ninaweza kuwa ndiye nimewajuza polisi kuhusu wewe?"

"Nisiwe mnafiki, kwa kweli ndivyo ninavyohisi kwa sababu kila nikiwaza na kuwazua sipati picha. Ni kweli polisi wangeweza kunikamata siku moja lakini si kwa haraka kiasi hicho. Katika nchi hii hatujafikia hapo."

"Mr Malima kweli umefikia hapo? Mimi? Unaweza kweli kunituhumu kukusaliti?"

"Katika mazingira kama haya unadhani ninaweza kumtuhumu nani? Yaani ninajuta hata kukushirikisha. Sijui umefanya hivi ili kunikomoa, kupata maslahi yoyote au kuna mtu unamtumikia. Isije ikawa umenunuliwa na Mapunda?"

"Baba Mchungaji, naomba uwe na hofu ya Mungu. Ninajua mtu ukikumbwa na janga kama hili unaweza kufikia hatua ya kutuhumu ovyoovyo. Ni sawa na mgonjwa anapougua kwa muda mrefu hufikia kuamini kila dawa anayoambiwa. Lakini ninaapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba sijafanya hivyo na wala sitafanya. Nitaanzia wapi?"

"Andrew, naomba uniache niendelee na matatizo yangu kwa sababu ninaweza kusema jambo baya linaloweza kukuudhi zaidi."

"Lakini nilitaka pia kujua mipango yako ya kushughulikia hii kesi, na..."

"Nimesema ondoka tafadhali. Kama kuna anayekutuma kamwambie mwisho wangu umegota. Mmeshanifikisha hapa niache nipambane. Kama nitafungwa kwa kosa si langu ndio majaaliwa aliyoniandikia Mwenyezi Mungu lakini atanilipa siku ya kiama. Haya maisha ya duniani ni ya muda mfupi na yana ukomo. "

Andrew, akiwa amegubikwa na mshangao alibaki mdomo wazi.

* * *



Simu ya mezani kwake iliita Salome alipoipokea. Karani wa mapokezi alimjulisha kwamba ni simu kutoka Tanga aliyokuwa akiisubiri.

"Hapa ni ofisini kwa Mkuu wa Polisi Tanga. Nazungumza na Salome Bakunda wa mtandao wa kijinsia wa Mwanamke Lulu?" Sauti ya upande wa pili wa simu iliuliza.

"Yes, ndio mimi."

"Afande amerejea ofisini punde. Basi nakuunganisha naye ili akupe majibu ya maswali yako."

"Nitashukuru sana dada," alijibu Salome.

Baada ya sekunde chache alisikia sauti nzito ya Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Tanga ikiita: "Hallow.

"Naye akajibu: "Hallow."

"Wewe ndiye ulitaka kujua zaidi kuhusu mkasa wa baamedi wa Tanga Raha Club?"

"Ndio."

"Mtuhumiwa, kama tulivyowaahidi wananchi tumeshamkamata tayari na bado anahojiwa. Tumemkamata leo jijini Dar es Salaam na hatua za awali zikikamilika ataletwa hapa Tanga."

"Kama nilivyowaambia awali taasisi yetu imedhamiria kutoa msaada wa kisheria kwa nyinyi polisi na mawakili wa Serikali na pia kusaidia kila hatua zikiwemo za upelelezi ili kuhakikisha haki inatendeka. Kwa hiyo nitakusumbua mara kwa mara kuhusu maendeleo ya shauri hili hadi hapo tutakapoona mahala tunakoweza kuingia ili kutoa mchango wetu. Na kwa vile umenithibitishia hilo kesho tutaandaa mkutano na waandishi wa habari. Tunataka umma wa Watanzania wajue kwamba sasa taasisi yetu haina utani na masuala ya unyanyasaji wa kijinsia, mauaji ya vikongwe, ubakaji, ukeketaji na mengine kama hayo."

"Tunawashukuru sana kwa hilo na sisi tuko tayari kutoa ushirikiano kadiri itakavyowezekana. Nitakukabidhi kwa mtu rasmi atakayekuwa anashughulikia hili. Wasiliana nami kesho jioni."

"Nashukuru sana. Huyu mtuhumiwa ni nani na sasa yuko kituo gani hapa Dar es Salaam. Bila shaka atakuwa boyfriend wa zamani wa huyu binti."

"Sijui kama ni boyfriend wake wa zamani au mpya. Huyu bwana tumeambiwa na msiri wetu kwamba ni Mwanasheria wa Tume ya Teknolojia na Mawasiliano aliyekuwa semina hapa Tanga, anaitwa eh eh Jackson Jorwa Malima ni..."

"Umesema nani?"

"Anaitwa Jackson Jorwa Malima."Salome alishikwa na bumbuwazi na hajui namna simu ilivyomdondoka kutoka mkononi baada ya mapigo ya moyo kubadilika ghafla.

Kwa vile alikuwa ameanza kusumbuliwa na shinikizo la damu, aliambiwa na daktari akisikia hali kama hiyo atafune tembe za aspirin haraka.

Kwa vile alikuwa anatembea nazo, alizitoa kwenye pochi akazimung'unya kisha akajiegemeza kwenye meza.

Wakati akipambana na hali hiyo alisikia tena simu ya mezani ikiita lakini hakuwa na uwezo wa kuipokea. Alibaki amejiegemeza kwenye meza kwa muda wa dakika kumi hivi na taratibu akaanza kusikia mapigo ya moyo yanarejea katika hali yake ya kawaida.

Baada ya kutulia, alianza kujiuliza kama alichosikia kutoka kwa KPM wa Tanga ni sahihi kwa masikio yake au hakusikia vizuri.

Lakini akakumbuka kwamba Andrew alimpa taarifa za mumewe kukamatwa. Kutokana na Andrew kutomwambia sababu za kukamatwa kwake, wakati ule alihisi kwamba huenda alikamatwa kwa masuala ya kazi. Alihisi huenda kulitokea purukushani baina yake au wafuasi wa Bruno na wa kwake katika suala zima la nani akaimu ukurugenzi wa Tume na ndipo akakamatwa kwa sababu mumewe alikuwa amemdokeza kwamba suala hilo lingeweza kuleta kishindo TTM.

"Kumbe ni mume wangu ndiye mhusika mkuu? Yaani ndiye kamuua binti wa watu hivi hivi," alijiuliza mwanamke huyo huku machozi yakimbubujika kama maji bila kupata jibu. Alijiuliza kama mumewe na binti huyo walikuwa wakifahamiana kabla au la.

"Au ndiye baba wa mtoto wake... Na kwa nini akamuua?" Aliendelea kujiuliza. Alikumbuka usiku ule wa Jumamosi aliposikia habari hiyo ya mauaji ya msichana wa baa walipokuwa sebuleni na mumewe, kisha mumewe akabadilika ghafla hadi akalazimika kwenda kulala.

"Kumbe ndiyo maana akawa vile... Nitafanyaje sasa?" Alijiuliza na kujijibu kwamba angeendelea na harakati zake kwa sababu mumewe kama kweli ndiye mtuhumiwa, ni mhalifu kama wahalifu wengine na kwa mtazamo wake yeye alikuwa mhalifu mbaya zaidi wa kunyanyasa wanawake kutokana tu na jinsia zao.

"Nilimpenda sana mume wangu na nilitegemea kitutenganishe kifo kumbe Mungu amepanga vinginevyo. Siwezi kuendelea kuishi na mwanamume wa aina hii. Nitaishije na mwanamume malaya na muuaji? Hii maana yake ni kwamba hata mimi anaweza kuniua muda wowote akitaka. Itabidi sasa nichukulie kana kwamba nimefiwa na mume. Nijipange mimi na wanangu," alijisemea.

Kitu kilichomwongezea hasira ni kwamba kumbe mumewe alikuwa anamsaliti kwa kutembea na wanawake hadi mabaamedi. Alijihisi uzito kwenda tena kwa mumewe lakini akaona ni vyema aende akamsikilize na kumpasha kwamba katika suala hilo hatoangalia kama alikuwa mumewe bali kuhakikisha analipia makosa yake.

Kwa jinsi alivyokuwa amechanganyikiwa aliondoka bila kumuaga yeyote wala kufunga ofisi yake kwenda kituo kikuu cha polisi. Baada ya kutoka nje alitafuta usafiri wa magari ya kukodi ya Uber na baada ya muda wa dakika tatu hivi, gari dogo liliwasili, akapanda na kumwambia dereva ampeleke kituo kikuu cha polisi.

Wakati gari lile linazidi kusogea kwenye kituo kikuu cha polisi ndivyo hasira zilivyozidi kumsonga kooni. Aliporuhusiwa kuonana na mumewe kwa sekunde kadhaa walibaki wakiangaliana bila yeyote kusema chochote.

"Yaani nakuangalia hata sikumalizi. Hivi aibu hii nitaiweka wapi, yaani mtu mzima na akili zako, mtu na familia yako unakwenda kutembea na changudoa. Kama vile haitoshi unaamua… Unamnywesha sumu na kumuua?" Alianza kusema Salome huku machozi yakianza kumbubujika.

"Mke wangu mpenzi sihusiki na hili abadani..."

"Kwanza koma kabisa kuniita mkeo. Nani mkeo hapa…" Alimkata kauli. Akaendelea "Kama unajua una mke unakwendaje kutembea na msichana wa baa? Hivi ulimuua kwa nini? Wewe ndiye ulizaa naye mwanawe wa kwanza au ulisikia kakuambukiza Ukimwi ukaamua kumuua?" Aliendelea kulalamika huku akiendelea kufuta machozi.

Jackson alijilaumu tena kwa kumpa Andrew kazi ya kumjulisha mkewe kuhusu kukamatwa kwake. Ilionekana mkewe alikuwa na taarifa zote kuhusu kilichotokea. Alizidi kumlaani Andrew na kumchukia.

"Naomba unisikilize mke wangu nikueleze hatua kwa hatua kilichotokea..."

"Kwanza nimekwambia ukome kuniita mkeo. Mimi sina mume mshenzi kama wewe. Mimi ninaweza kuwa na mume malaya na muuaji. Haiwezekani. Kimsingi huna cha kuniambia kwa sababu habari zako nimeambiwa na chanzo ambacho hakina mashaka... Kwanza napoteza muda wangu kuongea na jitu katili, jitu malaya, jitu shenzi kama wewe."

Mwanamke huyo akihisi mapigo ya moyo yanataka kubadilika alisonya na kugeuka kuondoka.

"Mama Hellen mbona unanihukumu bila kunipa nafasi? Nisikilize."Alikiambia kisogo chake.

________________________________

Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu ninalazimika kuikatisha hadithi hii, kwani kitabu tayari kipo mtaani. Unaweza kujipatia nakala yako kwa Sh 12,000, kinapatikana kwa wauzaji mbalimbali au unaweza kuwasiliana moja kwa moja na mtunzi wa hadithi hii kwa simu namba 0758 143457.



CC Litro Daudi Mchambuzi The Hurricane Jael brucella moneytalk saneneto Affet dluv FabreG ndulle Morgan Freeman unprejudiced Mshana Jr Heri Zabron Hamis kisukari totopack lanyese maubusu Minja Ngalason positive is normal Mine eyes popie Mr no bioto yona raphael Bigjahman nyakisese Tanayzer Shupavu Ngoheranga kilambon renason ADK Makandila9090 General Galadudu Said Cosmetics SnowBall binti mapozi kingkimwe BILLIONAIRE 2025 Badar_01 kanonb bweke undeceivable Marcie KigaKoyo Justine_Dannie sir ide Verifier dokta lu langoni makedonia Kudo Queen M jonoma Sangomwile Lovekid The Planner Mbobo Jenseny Shunie Rosicky Drizzle nabali Secret genius mkulima2 mkulungwa02 Breki ya Kenge EnnoMX Galbi Siratheboy irumba1 mjingamimi TAUNO KIDUDU orturoo Mavindozii Sky Eclat Vangigula seeker of knowledge PapaaSide bardizbah Nascent richard Mzimu wa Kolelo boscop kawoli song 16 Mjep asan njau Silencer Kimatu hambiliki mwanangu Sigara Kali The Wolf Melvine Royal Son Edward A chapa chichiboy1 Scofied EINSTEIN112 Oyaaa majomba mwera hao Katavi Semere92 tokenring ilu Wand Mtoto halali na hela dan oseko Jovet Panel Matumbwela saadatmontana Forgotten MAWAZO UJENZI Masking Agent Madame S Stephen Chelu bouy saleh Rukube Covid nineteen marybaby Mama mimi Mlume ndagu kinjeboy Lubebenamawe FabreG Zion jrGong Marley pirate Careem ndulle FabreG Tajiri mpole BETONY manumbu1 dluv saneneto aramika kiletza Shupavu nsharighe Kambaku Iammoshyn song 16 Affet unprejudiced Agent007 enjai ya kyasha Edward A chapa dendaboy Req pwiro aggyd brucella Lengutee nyakisese mtume wawatu mr chopa The Hurricane Puppy Restless mpwisa kikoozi Mirlz B Matthew ASA 1 ndulle Tanayzer sawima manji h kawoli
 
Pamoja sana mkuu tuko pamoja sana unapatikana wapi? na endapo mtu yupo mbali nawe anakipataje hicho kitabu?
 
bahati mbaya sana kwangu sitapata kuimaliza sababu niko nje ya tz
 
dah.........................................................................................................................
 
Pamoja sana mkuu tuko pamoja sana unapatikana wapi? na endapo mtu yupo mbali nawe anakipataje hicho kitabu?
Piga simu au wasiliana kwa WhatsApp: 0758 143457, unaweza hata kuletewa mahali ulipo...
 
bahati mbaya sana kwangu sitapata kuimaliza sababu niko nje ya tz
Usijali, jaribu kuwasiliana na mtunzi (Hamisi KIbari) kwa simu/WhatsApp: 0758 143457, nadhani anaweza kukutumia softcopy...
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…