ChikoTz
Member
- Feb 26, 2019
- 37
- 33
Simulizi: SALHAT
Sehemu: 01
Mtunzi: Salma Ramadhani
Ulikuwa usiku wa manane ulioambatana na radi za kutosha huku mvua nyingi na Kubwa ikiendelea kunyesha katika maeneo ya Arusha mtaana wa Moshono karibu kabisa na uelekeo wa chekereni alionekana msichana mmoja akiwa na Mtoto mdogo mbele ya kifua chake huku akikimbia kwa hofu Kubwa sana na kutizama nyuma ambako ndiko kulikomfanya hofu yake itande zaidi.
Alijikwaa na kusimama tena kisha akambeba Mtoto yule na kuendelea kukimbia naye alikimbia naye hadi mahali alipohisi sasa ni salama kama atajificha hapo. Alijibanza katika kibanda kimoja na kuhisi kuwa hapo anaweza akawa salama wakati huo wote Mtoto yule mwenye miezi kama Minne alianza kulia na hivyo mama yule alichukua jukumu la kumnyamazisha kwa kumnyonyesha Mtoto yule ambaye alilipokea ziwa lake na kuanza kulinyonya akiwa hapo hapo liliingia kundi la watu wanne huku wakiwa wamevalia mavazi meusi na kushikilia bastola mikononi mwao huku wakiendelea kumtafuta hapo hapo liliingia gari jeuc na mlango ulifunguliwa na mmoja kati ya watu wale wanne waliowahi kutangulia. Vilishuka viatu vya kike vyenye rangi ya kijani na suruali nyeuc iliyoweza kumbana barabarah huku ikipokelewa na kibody cheupe kilicho chomekezwa ndani ya suruali ile na kikoti cha jeans cha kitop kilichoweza kuishia kwenye kifua chake.
Alitoa miwani yake na kivua kofia iliyokuwa imefunika uso wake alikuwa ni binti ambaye makamo yake hayakuweza kupishana na mama yule mwenye mtoto........Jina lake aliitwa Badra.
"Mmeshampata huyo Malaya???!! Aliuliza. "Hapana bossi bado hatujampata ila nahisi hawezi kukimbia umbali mrefu Kwani tayari tulishamjeruhi kwa risasi katika mbavu zake changa. Alijibu msichana mmoja ambaye aliongozana naye huyu waliimwita Mainda.
"Sawa nazihitaji mahiti zao hapa ziletwe sasa hivi hasa hasa huyo Mtoto" alizungumza Badra ambaye hakuonekana kuwa na hata roho ya huruma kwa Mtoto yule ambaye hata kujitambua bado.
Watu wale wanne walianza kumtafuta mama yule mwenye Mtoto wakiongozwa na Mainda.
Badra akiwa pale alifanikiwa kuyaona matone ya damu yakiwa yanaelekea katika njia ambayo ndimo alikojificha mama yule.
Alitabasamu na kucheka kinafki kisha akaanza kuzifuata alama zile za damu huku akiita.
"Samia!!! Samia!!!! Samia!!!!! Njoo rafiki yangu kipenzi kwanini unanipa wakati mgumu mimi wa kukutafuta wewe jaman ilihali unajua mimi sina shida sana na wewe zaidi ya huyo Mtoto wa Naseeb. Kwani huyo Mtoto anakipi kikubwa mpaka mnamficha hivyo jaman , Naseeb kafa leo kwaajili yake eti utaamini hilo. Samia!! Nilee tu huyo Mtoto hapa. Aliendelea kuongea huku akisogea karibu zaidi, wakati huo Samia alikuwa akitetemeka na asijue kipi cha kufanya ghafla mwanaye alianza kulia na kuwashtua hata wale waliokuwa hawajui ni upi upande alioko alimziba mwanaye mdomo na ghafla nayeye alizibwa mdomo na Mtu aliyetokea nyuma yake alijitahidi kumng.ata lakini Mtu yule alimgeuza na kumpa ishara ya kuwa anataka kumsaidia aliwasha simu yake iliyokuwa na mwanga hafifu kisha akaiplay sauti ya Mtoto iliyokuwa ikilia ndani ya simu na kumpa ishara ya Samia aondoke eneo lile pindi watu wale watakapoanza kumfuata yeye. Kijana yule alianza kupiga hatua na kuelekea chini kabisa ambako kulikuwa na kama bonde dogo tu lililobinuka kwa chini kidogo. Watu wale walianza kumfuata wakiamini ya kuwa ni Samia akiwa na mwanaye.
Wote walianza kumfuata na kumuachia nafasi Samia ambaye aliinuka eneo lile na kuanza kutembea taratibu huku akihisi maumivu makali sana upande wa kushoto katika mbavu zake na hii ni kutokana na risasi aliyokwisha tayri kupigwa na Badra.
Badra alipofika mbele kidogo baada ya kumfukuza Samia na kutokomea kusiko julikana alianza kuchezwa na machale na kuhisi tu huko siko baada ya kuanza kuisikia tena sauti ile ya Mtoto iliyokuwa ikilia kwa style ile ile tena kwa kujirudia wakati huo zilibaki mingurumo kadhaaa iliyokuwa ikisikika juu ya mbingu na radi chache zilizoweza kufanya waweze kuona hata kama siyo kwa mbali sana.
Badra alishtukia mchezo ule na kugeuka nyuma ambako alifanikiwa kumuona Samia akianza kutokomea maeneo yenye vibanda.
Samia alijitahidi kutembea lakini alishindwa kutokana na kidonda alichonacho wakati anaendelea kujisogeza zaidi aliviona viatu vya kike vikianza kumsogolea.
"Tafadhali Badra, Tafadhali usiniulie mwanangu!!! Alizungumza Samia akijitahidi kumtizama ni nani aliyekuwa akisimama mbele yake alipofika usoni hakuweza kumtambua vzuri na Kwani tayari alishaanza kuona kizungu zungu hakuchukua muda mrefu alipokonywa na Mtoto na hapo hapo alidondoka chini na kuzimia.
***** ****** ******
Ilikuwa acubuh yapata saa mbili kamili alionekana Badra akiwa amevalia gauni la kulalia na kutoka chumba kimoja ndani ya jumba Kubwa la kifahari alilokuwa akiishi tajiri mmoja aliyeweza kufahamika kutokana ma wingi wa Mali anazomiliki Jina lake walimwita Mr Matata huyo alikuwa tajiri aliyebahatika kuwa na Mtoto mmoja tu wa kiume ambaye alimpenda sana baada ya mkewe kufariki lakini mambo yalibadilika baada tu alipomuowa Badra Kwani hakumpenda tena mwanaye na mwisho wa siku kutokana na visa vya Badra baba huyo alimfukuza mwanaye ndani ya nyumba yake na kuishi na Badra.
Badra alijinyoosha na kuelekea moja kwa moja kwa friji ambapo aliiifunua na kuanza kukagua kipi cha kutumia kwa asubuhi yake hiyo. Aliichukua juice mango na kuelekea kwenye glass kisha akaimimina na kuanza kuitumia taratibu kabisa huku akitizama TV.
"Unaelekea wapi??! Aliuliza Badra baada ya kumuoma Mr Matata amevaa asubuhi asubuhi.
"Nataka kwenda kumchukua mjukuu wangu sitaki akae na baba mpuuzi na mama kama yule Kwani mazingira wanayoishi hayatamfaa yeye" aliongea Mr matata na kuondoka zake.
Badra alishikwa na hasira na kuitupa glass anayoitumia ukutani.
"Mpumbavu wewe Salhat...... Unawezaje kuwa kikwazo kwangu ukiwa na miezi michache tu!! Aliongea kwa hasira na kuuma meno yake kisha kuyatoa macho yake yaliyokuwa makubwa naya mviringo.
******* *******
Samia kutokana na jua alilokuwa akipigwa nao usoni na mawimbi ya habari kuwa makali kwa siku hiyo hakuweza kulala kwa muda mrefu. Alishtuka na kuita
"Salhat"!!! Pembeni yake alimuona mwanamke mmoja aliyekuwa amembeba Salhat na kumpatia uji.
Alimchukua mwanaye Salhat na kumuuliza.
"Wewe ni nani???!! Na hapa ni wapi??! Tafadhali okoa maisha ya mwanangu yeye ni mdogo sana hajui wala hatambui chochote Tafadhali!! Aliongea Samia akihisi ya kuwa Mtu yule ni mbaya wake, hapo hapo aliingia kijana aliyeweza kumsaidia Jana ucku ili asikamatwe.
"Huyu ni mke wangu anaitwa Lidia, mimi na yeye Jana tulisaidiana kwa pamoja kwaajili ya kuokoa maisha ya mwanao, na sasa usijali Kwani haupo tena Arusha alizungumza na kufungua upande aliotokea huku akimfanya Samia kuona bahari njee.
"Huku wapi??!!! Aliuliza kwa mshangao.
"Dar es salaam ila usijali pia kwasabab kesho kutwa tutaenda mwanza na huko itakuwa vigumu kwa Mtu yule kukufuatilia tena....... Lakini Dada!!!
Aliongea na kunyamaza huku akihisi azungumze au.
"Endelea" kauli ya ruksa ilitolewa na Samia.
"Kwanini wnamuandama Mtoto mdogo namna hiyo??!!
Samia alitizama chini na kumtizama mwanaye mdogo Salhat. Kisha akawaambia.
"Kweli kwenye maisha kuna kupanda na kushuka, na siku zote unaambiwa fadhila mfadhili mbuzi binadamu anamauzi, na nimeamini mbuzi akikuuzi utamnywa mchzi ila mkataapo pema pabaya panamuita" alizungumza maneno hayo ya mafumbo na kuwa kama ameendelea kuwachanganya zaidi Joseph na mkewe Lidia ambao wlitizamana tu na kurudisha macho kwa Samia aliyekuwa akiendelea kulia tu baada ya kuyazungumz maneno Yale Kwani aliyaelewa mwenyewe.
Kip kitafuata katika sehemu ya pili ya cmuliz hii ya Salhat ikiw huu ndyo mwanzo tu wa simuliz hii usikose kuifuatilia
CHANZO
bongosimulizi.com