Simulizi: Maiti inayotembea

Simulizi: Maiti inayotembea

Roisa group

New Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
4
Reaction score
4
RIWAYA: MAITI INAYOTEMBEA.
MTUNZI: RONALD
NAMBA YA SIMU: 0694840213.

SEHEMU YA 1.
Jina langu ni Masanja mabula, jina nililopewa na wazazi wangu wangu bwana na bibi mabula kwa kiligha jina langu lina maana ya " Akili zimo", huenda wazazi wangu walikuwa na nia njema ya kuniita hilo jina maana wakati mwingine majina husadifu maisha ya mtu.

Kabila langu kama msukuma kuwa mtoto wa kwanza wa kiume ni fahari kubwa sana kwa familia pia jamii kwa ujumula. Hali yetu nyumbani haikuwa nzuri sana kiuchumi tulitegemea kilimo na mifugo ili wazazi wangu wakidhi haja yangu na wadogo zangu sita, hasa katika upande wa chakula na nguo zetu za shule.

Maisha yetu yalikuwa vizuri sana maana baba kwa kipindi hicho alikuwa mkurugenzi katika shirika la utangazaji TBC, lakini kila kitu kilibadirika baada ya baba kupata ajali mbaya iliyosababisha kupoteza maisha yake papo hapo.

Fedha zote za pensheni na miradi aliyoacha baba ndugu zake walikwapua hivo tukaanza kama mwanzo, nikiwa katika umri wa miaka 8 tayari niliingia katika majukumu mazito ya kuanza kulea wadogo zangu pendo, Imani na Ester.

Mama alijitahidi kwa uwezo wake kupitia uuzaji wa samaki wabichi aliokuwa akichuuza ziwa Victoria, kipato chake kilikidhi mahitaji madogo Sana. Lakini nae alikuwa akisumbuliwa na mguu kidonda kilikuwa katika mguu wake wakati wa baridi kilikuwa kinampa shida sana.

Kutembea peku na kuamkia kula kipolo cha ugali ili tupate nguvu za kwenda shule ilikuwa jadi yetu hali hiyo tuliizoea kabisa. Mkombozi pekee aliyekuwa amebaki ili tuepukane na wimbi hili la umaskini ilikuwa elimu pekee,
Elimu ulikuwa mwanga pekee niliotegemea maana wahenga husema" Elimu ni ufunguo wa maisha" basi na mimi nilikamata hiyo elimu vizuri nikitegemea kuwa itakuwa ufunguo wangu kweli.

Mungu aliniwekea neema yake nilihitimu kidato cha sita, shule ya wanaume Bwiru Boys mwanza nikimaliza pia kama mwanafunzi bora kwa mwaka huo na hata matokeo yalipotoka Division 1 point 3 ilisoma katika matokeo yangu ya NECTA.
Nilimshukuru Mungu sana, kwa hicho nikamueleza mama juu ya njozi zangu za kuwa mhandisi mkubwa wa barabara (Civil engineer) ndoto zangu ilikuwa pia kuwa na kampuni kubwa ya ujenzi wa barabara.

Mama alibariki kila kitu na kunitakia neema kubwa sana, na pia nilimshirikisha mpenzi wangu ambae nilijuana nae kitambo Zaituni akaweka mkono wake.

Zaituni alikuwa amehitimu kidato cha sita na alitegemea pia kwenda chuo lakini mambo hayakumuendea vizuri sana akabaki nyumbani.

Alikuwa msichana aliyejitoa kwangu, ndoto yetu ilikuwa nikimaliza nimuoe awe mke wangu kulipa fadhira za uvumilivu wake kwangu na anavojitoa katika familia yangu.

Selection za vyuo vikuu zilitoka, chuo cha ndoto yangu University of Daresalaam (UDSM) ndo nilichaguliwa faculty of Civil engineering.

Nashukuru pia mkopo nilipata kwa asilimia mia toka HESLB, moyo wangu ulijawa na amani sana na hata kabla sijaondoka nilimuahidi mama kuishi katika misingi ya imani na boom litakapokuwa likitoka angalau kiasi niwe nawezesha familia.

Moja ya jambo ambalo leo linanifanya kuandika mkasa nikiona dunia imenielemea,.wazazi wangu walionipa tumaini na wadogo zangu waliokuwa wanapiga magoti kila jumapili katika madhabahu ya " Mt. Augustino, jimbo kuu la mwanza" nimewatupa mkono.
Nakuandikia wewe nikikuonya " usiposimulia nitasimulia mimi" Mola wangu hii barua ifike dunia nzima kwa jina yule mwenye ndoto kubwa basi aziishi ndoto zake.
Ajue katika dunia hii muda wa kutengenezea maisha ni ujana, baada ya hapo ni majuto mjukuu.

Sijilaumu mimi ila nalaumu kitu kile kilichofichwa na mimi sikufahamu mapema ikasababisha majeraha yangu ya moyo na familia yangu, mimi nimekuwa kama mpumbavu.

asubuhi katika nyumba yetu ndogo ya udongo Kisesa, mwanza . Mama alikuwa amesimama mlangoni, mikono yake imeshikilia begi langu la zamani la shule begi ambalo lilikuwa limechoka na safari nyingi za shule ya sekondari. Ndani yake kulikuwa na nguo chache tu na picha moja ya familia yetu yote na baba (Mungu ailaze mahali pema), mama, na wadogo wangu watatu.

"Masanja, usisahau kuomba kila siku," aliniambia huku macho yake yakijaa maji. "Na usikose masomo hata siku moja. Hii ni fursa ambayo itakutoa sehemu moja kwenda nyingine"
Nilikubali kwa kichwa tu, kwa sababu koo langu lilikuwa limejaa.
Sikutaka aone machozi yangu yanadondoka.
Zaituni na yeye alinifata na kunikumbatia, japo niliona aibu kidogo mbele ya mama yangu lakini sikuwa na namna, alinambia maneno machache lakini yaliyonigusa
" Masanja, najua unaenda dunia njingine tofauti na huko. Kuwa makini sana mama yako, na wadogo zako wanakusubiri wakiamini wewe ndio masiha wa familia yao hivo jifunge nila.
Na pia mimi nitazidi kukuombea usije badirishwa na jiji hilo ukanisahau" Aliongea akiwa amenikumbatia, kisha alitoa noti za elfu kumi nilipohesabu ilikuwa laki moja na nusu.
" chukua hicho kiasi kidogo kitakuwezesha mpenzi"
" asante sana mpenzi sitokuangusha".

Nilipanda bus la Dar luxury la kunipeleka Daresalaam chuo ambacho ni ndoto ya kila mmoja, kuchukua shahada yangu ya kwanza ya Civil engineering, bus likiwa limejaa watu na mizigo. Barabara ilikuwa ya lami safi hivo kunifanya nifurahie safari. Chuo kikuuu cha dares salaam wengine hukiita UDSM.

Mahali ambapo watoto wa wakulima kama mimi wanaweza kuwa mhimili mkubwa katika familia na kuwarudishia watoto wengine ndoto zao.

Nilifika dares salaam usiku saa sita, sikuwa na pa kwenda wala kulala maana bajeti ya pesa yangu ilibaki ya kupanga pango na chakula hvo ikanibidi nilale stendi kubwa ya mabasi Magufuli Bus Stand, nililala mpaka jua la adhuhuri.
Jua lilikuwa limeanza kupanda juu, na hewa ilikuwa safi, yenye harufu ya magari mengi na watu ambao usiku au mchana walionekana kuwa katika pirika za hapa na pale.

Moyo wangu ulikuwa ukidunda kwa kasi ya injini ya basi nilipokuwa nateremka kituo cha MAGUFULI BUS STAND. Dar es Salaam ilinipokea kwa fujo; kelele za wapigadebe, joto lililokifanya shati langu la "tetroni" linate mwilini, na harufu ya moshi wa magari iliyokuwa tofauti kabisa na hewa safi ya kijijini.

Nilikuwa nimebeba sanduku langu la mabati, lilelile ambalo mama aliliuza mbuzi wake wa mwisho ili nilinunue. Ndani yake kulikuwa na ndoto za ukoo mzima.
@itaendelea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom