JASMINE
MTUNZI BEBAS CUTELY .
SEHEMU YA 31
BOOKING 0756748557.
Jasmine alianza kuogopa kuona aibu . Watu wote" Jasmine kubari ,kubari ,kubari "wasichana wezake . Jasmine alibidi akúbari na kumpa mkono Hans kwenda kwenda adi kwenye red kapeti na kuanza kupiga picha .
Walipiga picha kibao kumshinda bibiarusi mwenyewe . Zuri mpana huyo alianza kuwatafutia wezake mapozi ya wanamitindo . " Jasmine mkumbatie Hans kwa nyuma lile ponzi la Rihanna na mchumba ake ". Jasmine alikuwa akiona aibu sasa . Watu wote Jasmine " unatualibia furaha yetu Jamani ".
Jasmine alibidi aende kumkumbatia Hans iliasijulikane vibaya , Zuri alipiga picha . Walipiga picha mapozi mengi Hans kambeba Jasmine , nyingine wanahangalia , nyingine Hans kamkumbatia Jasmine , nyingine Hans kamkiss Jasmine kwenye shavu.
Najma aliona donge na kuamua kuondoka zake chumbani akiwa analia . Watu wote walibakia kumuangali Najma na Hans alibidi afate Najma chumbani kwake..
"Wewe vipi unaniletea habari za kishamba kishamba hivi " Hans alionge akiwa yupo serious . " Hans ni mwanamke gani anaweza kukubari kupiga na mwanamke mwingine ingawa yeye yupo ".
Hans alicheka sana " imekuuma eeeh " aliongea . " Wewe umeshaambiwa picha za best friend unataka tukae maponzi ya baba mkwe , yale ndo maponzi ya rafiki " aliongea akiwa yupo serious. " Kama imekuuma endelea kumia vizuri ” alifungua mlango na kutoka zake akiwa anafonya .
" Huyu mwanamke mpumbavu kunicheat kaanza mwenyewe wivu anaona mwenyewe akwende zake" aliongea na kuingia chumbani akiwa anaimba.
" Aise Jasmine mzuri sana na wamemechi na Hans kwenye picha" aliongea Nasra . Rahma" eeeh mashallah ndo maana brother saa 6 karudi nyumbani sasa hivi sio mzigo uo nyuma ". Jasmine " ebu mnipishe mimi huko punguzeni majungu yenu " aliongea akiwa yupo busy anamenya ndizi .
Walipika vizuri na kula na kila mtu akienda na kazi nyingine. Najma alikaa akiwa na mawazo sana " siwezi kukubari Jasmine habakie hapa kama leo kapiga picha na Hans kunizidi mimi kesho anaweza kupendwa na Hans pia ".
*****************
Najma alichukua simu nakupiga kwa yule mwanaume aliyomtafutia Jasmine . " Hello Abdull" .
Abdull alipokea " hello Najma" . Najma" vipi lile zoezi limeishia wapi ? aliuliza. Abdul "mimi nimeshindwa kumuoa huyo binti maana sina uwezo wa milióni mia mimi Najma". Najma " jamani naomba please unisaidie mimi "..
" Najma sina uwezo wa kutoa milióni 50 mimi jamani " aliongea Abdul . Najma alishangaa! " milióni 50 ? aliuliza. Abduli " ndio Najma ndo mahari nilioandikiwa ". Najma" ok poa " alikataa simu na kukaa kitandani .
" Kwanini Hans anakataza Jasmine asiolewe kuna siri gani ? alíjiuliza na kuamua kulala akiwa ana ata amani. Asubuhi ndo waliamka ndo maandalizi ya uchumba wa Najma na Hans yamepanda moto.
Hans akiwa ampendi kabisa Najma kazama kwa Jasmine tena . Kamati ya uchumba wake ilikaa jumapili ndo sherehe lasmi za uchumba . Wageni kutoka sehemu mbalimbali walianza kufika na kupokelewa.
Najma alivyokuwa na roho mbaya kwa Jasmine shida ake atoke pale nyumbani alimpigia simu bwana ake Hamza. Hamza alijibu'' njoo nyumbani tupange sawa" . Najma alikubari " juma pili ataenda kwasababu anaenda saloni ndio sherehe .
Kesho yake ijumaa baba Hans alirudi kwake kutoka bungeni akiwa na furaha sana . " Maandalizi teali maana bunge zima wanakuja kusherehe ya kijana wangu ". Hans alikuwa ayupo katoka sehemu moja kukaa .
Zuri alienda nakumkuta brother wake amevimba sura. " Vipi brother mbona hivi ? aliuliza . Hans alijibu'' mimi siwezi kumuoa Najma tena kwa vitu alivyonifanyia mimi ".
Alichuku simu na kumuonyesha mdogo wake sms za Najma mbaya zaidi adi ananiibia mimi kweli.
Zuri " mmmmh pole sana brother sasa itakuwaje na baba kashandaa uchumba na kawalika Watu kibao" . Hans alíjikuta akimuangalia mdogo wake nakumwambia" kumchumbia sio tatizo lakini asahau kuja kumuoa" .
Hans alipanda kwenye gari lake adi nyumbani kwao alifika nakulala. Jumamosi asubuhi shamla shamla zilipanda moto huku Hans akiwa ana muwaza Jasmine wake jinsi alivyokutana nae adi kupendana nae.
Hans alitoka na kuingia ndani mlango alimuona Jasmine akifuta futa vumbi mwenyewe . Hans alibaki kumuangali tu , Najma alitoka palepale na kumkumbatia Hans. " Kesho nitakufanyia surprise " alisema Najma .
Hans alikuwa na mawazo na kuingia chumbani kwake kulala akuwa na furaha na uchumba wenyewe.
Itaendelea