MTUNZI: XAVERY E. LUOGA
RIWAYA: "MACHOZI YA DAMU"
SEHEMU YA 01.
WhatsApp NO. 0672493994.
#SimuliziHuruMediaProduction
×--------------SHUMP---------------×
DAR ES SALAAM:
"Kwa Majina naitwa EPIPHANIA WILNERY MKOMBO Au Mama Bright Kama ilivyozoeleka hapo mwanzo" Sauti ya Kigugumizi iliyoanza na utambulisho wa majina ilianza kusikika karibia kila kona ya ukumbi.
Kila mmoja sasa alikua tayari kusikiliza mkasa wa Kweli wa bidada huyu aliyejitambulisha kwa jina EPIFANIA, kulingana na mengi aliyopitia, Eppie aliamua kuweka wazi sasa mambo yaliyomsibu hadi kufikia hapo. Aliitwa katika mkutano mkubwa wa waandishi wa habari na mkutano huo kupewa jina la MACHOZI YA DAMU.
Waandishi walitamani haswa kujua ni kipi haswa kimsibu mwandada Eppie hadi kutumbukizwa gerezani kwa kosa la Mauaji?. Mkasa wake ukasimuliwa kama ifuatavyo;
“Mimi ni mwanamke nisiyezidi hata miaka thelathini na nne, Mzawa wa Wilaya ya Madaba iliyopo mpakani mwa Mkoa wa Ruvuma na Njombe. Kiasili mimi ni Mbena kabisa niliyechanganyika na Ungoni na Matengo kwa mbali, kilichonileta hapa ni kuhusu huu ushuhuda wa Machozi ya Damu ambao umepitia katika maisha yangu. MACHOZI YA DAMU!, MACHOZI YA DAMU!, MACHOZI YA DAMU! "
Alirudia Mara kadhaa maneno hayo kwa kutuweka sawa na vifaa vyetu ili tupate mkasa kamili, jambo lililoendelea kutia hamasa zaidi ya watu kusikiliza makini ni machozi ambayo yalikuwa yanamtiririka mwanadada huyu, kila mmoja akijiuliza kuna kipi kilichomsibu hadi kuporomosha machozi mzito mithili ya damu? na kwanini Mkasa wake aliupachika jina la MACHOZI YA DAMU???. Tukabaki vinywa wazi kusubiri majibu.
“NDUGU Waandishi, Ndugu Wasikilizaji, Ndugu Wanaume na Ndugu Wanawake wenzangu, najua Tanzania nzima sasa imetega sikio na jicho lake kusikia na kuona kile ambacho natamani kusimulia. Sidhani kama nitafanikiwa kuyatoa maneno yote ya moyo wangu kutokana na machungu yaliyonishika. Moyo wangu unauma sana na kujihisi nina hatia, labda ni kwa sababu ya maamuzi ambayo niliyachukua baada ya kuteseka kwa muda mrefu, Nimesababisha kifo mimi ndugu Waandishi ah, oh, Ohah ha ha ha ha mimi Eppie... Eh Mungu Jitahidi kunisamehe kosa hili japokuwa wanasema halina msamaha!" Eppie aliendelea kuongeza kilio kidogokidogo na kuacha hudhuni itawale chumba kizima. Kabla hajaanza kusimulia vizuri tayari kila mmoja mule ndani alianza kuonesha kumhurumia. Aliendelea.
“Nilizaliwa Tar 25/10/1998 hadi leo hii 2030 nipo mahali hapa nimeshatimiza miaka 32.
Nilizaliwa wakati wa wazazi wangu wote wawili wakiwa wanapatana, wote wakiwa wazima hadi leo hii ninapoongea nanyi. Nilimaliza Elimu yangu ya Msingi na Sekondari hukohuko Wilayani Madaba na Shule ya Upili nilimaliza pale shule ya sekondari ya Wasichana wilayani Masasi mkoa wa Korosho-Mtwara. Kwasababu za kufanya vizuri katika masomo yangu, Mungu akaniadhibu sasa kwa kinipeleka kusomea Kozi ya Ualimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, lakini katika tawi la Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) kwa miaka mitatu ya shahada ya kwanza.
Kipindi chote hicho tayari nilishaanza kujiweka wazi kuwa nitasimamia msimamo wangu wa kuishi maisha yangu, na sitakuja kulia kisa Mapenzi. Na leo nasimama mbele yenu na chozi la damu likitiririka kama mvua. Ah, jamani!, jamani! Jamani!, Omba tu uendelee kusimuliwa. Maisha ya mapenzi yanalaana. Yana laana ndugu zangu...." Eppie aliendelea kuongea akisogeza kitambaa chake chepesi na kuyafuta machozi yake yaliendelea kutiririka. Akaweka sawa kora yake sare ya magereza na kuendelea.
"Hapohapo chuo nilikutana na kila aina ya wanaume, warefu, wafupi, wembamba, weupe, maji kunde, chotara, wenye pesa na wasio na pesa lakini moyo wangu uliendelea kutulizwa kuwa hakuna mwanaume hapo ambaye anaweza kukidhi haja ya moyo wangu. Wote nilihisi ni wababishaji tu. Wakaka wa chuo? Ah, hapana kwa kweli. Labda kwasababu ya mazingira niliyotoka nikawa nawachukilia wanaume kawaida tu. Na pia labda kwa sababu pengine labda sikupata yule nyonga mkalia ini ambaye amethubutu kuucha’chafya moyo wangu na kujikuta nauhifadhi kwake!. Nikaendelea kutunza usichana wangu. Niliiutunza, kumtunzia mwanaume ambaye hakuwa na shida na moyo wa mtu. Mwanaume ambaye alibadili Eppie mimi kutoka utulivu na hofu ya Mungu hadi kuwa mhusika wa kifo chake. Nikaitwa Muuaji. Eppie mimi ni muuaji jamani haaaah!"
HADI hapo Eppie aliweka kwanza nukta na kuendelea kushusha machozi. Moyo ulinisuta sana kutaka kujua nini ambacho kipo ndani ya mkasa wa Eppie, Kwanini ajutie vile maisha yake kiasi cha kumkosoa hadi Mungu? Kwanini awe muhusika wa mauaji? Kamuua nani?, na kwanini???
Indelea...
Karibu Simulizi Huru Media Production. Sapoti kazi zetu katika mitandao yote ya kijamii. @SIMULIZI_HURU_MEDIA_PRODUCTON
MTUNZI: XAVERY E. LUOGA
RIWAYA: "MACHOZI YA DAMU"
SEHEMU YA 02.
WhatsApp NO. 0672493994.
#SimuliziHuruMediaProduction
×--------------SHUMP---------------×
HADI hapo Eppie aliweka kwanza nukta na kuendelea kushusha machozi. Moyo ulinisuta sana kutaka kujua nini ambacho kipo ndani ya mkasa wa Eppie, Kwanini ajutie vile maisha yake kiasi cha kumkosoa hadi Mungu? Kwanini awe muhusika wa mauaji? Kamuua nani?, na kwanini???
CHOZI LA PILI...
"Ndugu Waandishi, Mwishoni kabisa mwa mwaka wa tatu, alikuja mtu maarufu sana chuoni kwetu, alikuja kutupa baadhi ya mambo ambayo yanaendelea mtaani hasa katika shida ya upungufu wa ajira.
Mtaalamu yule aliichambua vizuri sana Tanzania, alikuja na ushaidi wake wa data na takwimu nyingine mbalimbali. Akafanikiwa kuniteka pia katika suala lake la mahusiano, kauli yake bado haijatoka katika kumbukumbu zangu, nakumbuka! Nakumbuka alisema kuwa eti “Tafadhali huu ndio muda mzuri wa kupanga maisha yako.. Mwanamke! tafuta mwanaume wa maisha yako. Mtaani mambo sio poa. Jaribu sasa kumuweka mwanaume mmoja ambaye hisia zako zimekuweka huko. Mpende, mjari, mheshimu, kwa maana usipokuwa na msimamo sasa na kujiandaa katika maisha ya familia, utajikuta unapoteza muda mwingi sana kujifunza vitu vipya na vigumu ukiwa ndani ya ndoa. Nawashauri kwa kuweka hazina!. Jifunze kuchagua na kupenda. Jifunze kuwa na msimamo”: kauli hii aliitoa yule mtaalamu wa saikolojia katika mkutano mkubwa wa wanawake. Nikaichukua kama ilivyo, sijui niielewa vibaya au la lakini niliitendea kazi.
Tokea siku hiyo nikafungua kufuri la moyo wangu kwa kuanza kutafuta mwanaume ambaye atakuwa ndoto za maisha yangu. Nikaacha kufikilia mambo mengine na sasa kujikita zaidi katika masuala ya kuchunguza wanaume na sifa zao, yote hiyo ni kujua nani nitampa sehemu zangu za siri na akazitunza!, hatimaye nikaangukia katika mtego wa nguruwe. Mtego ambao hadi kufikia hapa sijajua ni nani aliutega? Na alikuwa anakusudio gani?. Kama kuniua basi amefanikiwa... Eppie mimi leo sina ndoto wala malengo tena. Miaka Thelathini na mbili tu nimeshazikwa tayari... Jamani mapenzi.."
Eppie aliendelea kutoa mkasa wake huku machozi yakiwa kama kinywaji. Kila neno aliloongea alionesha kuwa na uchungu mno. Bila shaka alikuwa anajuta, anajuta na atajuta sana. Sasa kwanini awe muuaji? Bado ukumbi ulikua kimya kumsikiliza.
"Kabla ya kufanya mtihani wangu wa mwisho wa kuhitimu elimu ya chuo kikuu shahada ya kwanza, nikakutana na mwanaume wa maisha yangu. Mwanaume ambaye ameacha kovu kwangu, ‘labda mtu alikua sahihi ila muda ndio haukuwa sahihi…’
Ah, Ilikuwa ni katika Uzinduzi wa Kampuni ya SIMULIZI HURU MEDIA PRODUCTION pale UBUNGO PLAZA. kwa kweli nilikua mpenzi sana wa simulizi za kusisimua. Simulzi zilinijenga sana. Nilijutia maisha wapitayo wahusika katika simulizi ila sikuamini kwamba kweli wandishi wanaandika mambo yanayotokea katika jamii.. Nilihisi ni visa tu vya kubuni na wameandika ili kujipatia kipato.
Kwa kuwa nilikua mpenzi wa Simulizi na mdau mkubwa wa Simulizi nilikuwepo siku ya uzinduzi ili nikutane na waandishi wangu watano muhimu ambao kazi zao nilikua nikizipenda kila kuchwao... Naomba niwataje tu hata kwa majina kwani nao yaweza kuwa ni wahusika wakuu wa mkasa huu... Aaaaah jamani.. Jamani... Jamani.. Mapenzi!.
Ah, naomba nimtaje Ibrahim Hussein katika nafasi ya kwanza.. Huyu alinikosha na mkasa wake wa Talaka kwa Mke Mwema. Twende kwa Talhat Moudy nae alinisukumia katika mkasa wa mwanamke mwenzangu ambaye Alishindwa kumsahau Mtunza moyo wake. Sam Darfur kama Mwenyekiti wa Simulizi Huru Media Production alinigusa kwa mikasa kadha wa kadha naomba nitaje tu huu wa Nani Kaniambukiza nikajifunza namna bora ya kutunza siri zangu usije yakanikuta yale mambo ya UKIMWI na nikashindwa kutambua nani ameniambukiza!. Marcus Cona pia alinikosha kwa visa vyake vya hapa na pale, kaka mcheshi sana huyu nilianza kumpenda toka ya kwanza anapandisha simulizi yake ya THIS IS DAR ES SALAAM huko YouTube katika Channel yao hiyo hiyo ya Simulizi Huru Media Production.
Naomba nimalize na huyu mwandishi. Beloved One, My Heart Beat, My Heart Master, Kipenzi Cha Wapenzi.. Aliniandikia PENDO HURU na simulizi ya MKUKI WA MAPENZI na kunichoma kabisaa!! Aliutumia huo mkuki kunichoma kabisa, kwa kweli alinipata, na huyu ndio sababu ya yote haya hadi leo hii nipo hapa kutoa ushuhuda huu, nikampa hadi uhusika katika moyo wangu nikiamini kuwa anaweza kuunda kama aundavyo vyema hadithi zake. Lakini....!! Da!. Da! Daa!
Inaendelea
Karibuni Wakubwa