bioto
JF-Expert Member
- Oct 1, 2017
- 1,261
- 2,099
SIMULIZI: EQUATORIAL FOREST (msitu wa
Equatorial)
MTUNZI: AISHA KHAN
SEHEMU YA 01
UTANGULIZI: kwa Jina naitwa Najma Abdallah, Nina
umri wa miaka 22 na soma university mwaka wa
pili sasa, wazazi wangu wote wapo hai ila baba
yangu mzazi alifungwa jela sasa ni mwaka mmoja
kwa kesi ya uchochezi wa wana nchi ili waweze
kuleta mgomo selekalini kuwa mshahara waliopewa
ulikuwa mdogo.
Nakumbuka siku hio baba na wafanyakazi wenzie
(walikuwa ni wajenzi) hivo walipata tenda kutoka
kwa mkuu wa mkoa ili waweze kujenga shule za
wanafunzi wa primary, baba na wenzie tenda hio
waliichukuwa kwa mikono miwili Baada ya
kukubaliana kipato kizuri, walipomaliza mkuu wa
mkoa na ma supervisor waliokuwa wakiwasimamia
takribani wa nne waliwapa pesa ndogo sana kama
asilimia arobaini kwa ile waliokuwa wamekubaliana
hali ya kuwa selekali ilitoa pesa ya kutosha, kitendo
cha kupewa pesa ndogo kiliwafanya wachukie na
kudai pesa yao, siku moja baba na wenzie ishirini
Walikubaliana waende kwa viongozi wa Juu
wakaombe msaada ikiwezekana wawawekee hata
asilimia kumi Juu zingine wakaushie ila kila
waliekuwa wakimlilia aliwapotezea kama vile
wanamsumbua, waliamua wachukuwe uamzi wa
kwenda kituoni kulipotia swala lile ajabu mkuu wa
mkoa aliwazunguka wote wakawekwa Chini ya ulinzi
kwa kesi ya kuleta vurugu nchini, hivo Walikaa siku
nne sero.
Siku hio ya nne supervisor mmoja aliwafuata sero
akawaambia wapotezee ile kesi Ila baba akazidi
kuwapa moyo wenzie waendelee kutetea haki yao
Ipo siku mheshimiwa Raisi litamfikia Jambo hilo na
atawachukulia hatua, mwishowe baba alichezewa
mchezo wenzie wakamzunguka Baada ya kupewa
pesa ndogo wakampachika kesi kuwa Yeye ndie
alikuwa anawachochea waje kuleta vurugu selekalini
ili kuwachafulia Jina hali ya kuwa pesa walipewa
zakutosha hivo kesi Ilikuwa kubwa tena kubwa Mara
dufu, kila Tukienda Mimi na mama yangu kuuliza
tulikuwa tukiambiwa kesi imeshikiliwa mahakamani.
*******************************************
Mama yangu Umu-kulsum toka baba aingie jela
alipatwa na ugonjwa wa presha kutokana kutulea
Mimi na mdogo wangu Latina ilikuwa kazi kubwa
kwake ukija kuangalia sote tulikuwa Wa kubwa na
tulikuwa sote tunasoma university Mimi mwaka wa
pili mdogo wangu Latina mwaka wa kwanza na
pesa yote ya Ada ya chuo ulikuwa ni mkopo baba
aliouchukuwa selekalini akiamini angelipa taratibu
taratibu ila majanga ndo hayo mwaka sasa yupo
jela, hilo ndilo lilizidi kumchanganya mama licha
kila siku tulikuwa tukimpa moyo asijali tupo kwa
ajili yake tukimaliza chuo tukapata kazi nzuri
tutamsaidia baba na tutalipa madeni yote
tunayodaiwa.
SONGA NAYO!
Asubuhi mapema ya tarehe 2 may mwaka 2019
Mimi Latina Pamoja na mama yetu tulijiandaa
tukaelekea mahakamani iliopo dar es salam Maana
Sisi makazi yetu yalikuwa dar es salam maeneo ya
kijitonyama, tulipofika mahakamani kesi za watu
wengine zilisomewa mwishowe baba akaletwa
kizimbani ili kusomewa hukumu yake, aisee
nilipomuona baba yangu anahofu nyingi na sio
Kawaida yake machozi yaliyatawala macho yangu
Nikajilazimisha kumpa moyo huku nikitabasamu,
baba alipoiona familia yake imekuja kumpa moyo
alifurahi moyoni huku akiendelea kututazama, kesi
yake haikuwa na wakili hivo alikatiwa kifungo cha
miaka mi tano au faini ya milioni tano, mama
aliposkia hivo nguvu zilimuishia akalegea huku
akipumua vibaya, Tulianza kumpepea huku tukilia
Pamoja na wasamalia wema waliokuwa hapo,
kitendo kile kilimfanya baba aanze kumuita mama
kwa uchungu: Umu Umu Umu mke wangu !!!
Mapolisi walimchukuwa baba na kumrudisha jela,
Baada ya lisaa limoja kupita tulikuwa tupo njiani
tunarudi nyumbani huku mama akionekana vizuri
tofauti na Muda uliopita.
Tulipofika nyumbani Nilimpa moyo mama asiwaze
Sana milioni tano sio pesa nyingi atatoka jela muda
sio mrefu.
Siku hio ilipita kila mtu Hana raha, siku moja
Baadae niliporudi nyumbani Baada ya kutoka shule
Latina kwa presha aliniambia: mama hali yake sio
nzuri.
Nikashangaa na kumuuliza: Kulikoni?
Latina: ndio toka asubuhi anaongea maneno ya
ajabu ajabu hata simwelewi.
Nikamuuliza: anaongeaje?
Latina: Njoo umuone mwenyewe.
Tuliingia ndani nikamkuta mama akiwa amekaa
sebuleni huku akivuta vuta uzi taratibu uliopo
kwenye nguo aliokuwa amevaa, nilikaa pembeni
yake na kumuuliza: mama nini shida?
Mama hata hakuniangalia aliendelea kufanya
alichokuwa Anafanya ndipo Nikamuuliza tena:
unafanya nini mama???
Mama alikurupuka na kunisukuma kisha akasema
kwa sauti ya Juu: Mume wangu yupo wapi???
Mimi na Latina Tulimshangaa ndipo mama akatoka
nje anakimbia huku akipiga kelele, Tulitoka hapo
tukamfuata haraka ila kwa mbio alizokuwa nazo
Alituacha mbali, siku nzima iliisha tukiwa
tunamtafuta ila hatukuweza kumuona.
Majira ya jioni tukiwa tupo njiani Mimi na Latina
mwenye umri wa miaka 20 njia nzima tulikuwa
tunalia bila kujuwa wapi tutamuona mama, tukiwa
tunazidi kulanda Landa mtaani mdada jilani yetu
alitusimamisha na kusema: mnisubiri Kidogo.
Tulisimama ndipo akatufikia na kusema: mama
yenu nimemuona kule Chini ya barabara kuelekea
Ilala.
Tuliposkia hivo tulimuomba atusaidie atupeleke
huko nae hakuwa mgumu kwetu alitupeleka huku
tukikimbia Sana, tulipofika maeneo aliotuambia
alisema: ndo Yuleeee..
Tulimuona mama kwa mbali alikuwa ametugeuzia
mgongo huku akiwa amekaa Chini kama vile kuna
kitu anachambua, muonekano wa mama ulinifanya
niangue kilio kikali ndipo mdada Yule akanipa moyo
nisijali Allah yupo Pamoja na Sisi, mdada Yule
Alituacha hapo akaenda nyumbani maana muda
ulikuwa umeenda, tulimaliza kama dakika kumi
tukiwa tunamtazama kwa mbali ndipo Latina
akaniambia: tukimfuata akatuona wallah
hatutampata tena Sasa sijui tunafanya nini.
Nikamjibu: Kikubwa tunamuona, Ngoja mi niende
kumuona Yule Doctor Rafiki yake baba nikamuambia
ikiwezekana aje kutusaidia.
Tulikubaliana hivo Mimi nikaenda kumtafuta mzee
huyo, Baada ya muda tulikuja nae akiwa
ameongozana na Manesi wengine wanaohusika
kuwalinda Wagonjwa wa hakili, tulipofika
walimsogelea taratibu ile kuwaona tu alishtuka Ila
walikuwa tayari wamemchoma sindano ya
kumpunguza nguvu mwilini.
Tukiwa tupo hospital doctor aliniambia: mama yako
amepata mshtuko mkubwa Ila hili ni tatizo dogo
mambo yatakuwa vizuri.
Siku hio ilipita mama alihifadhiwa hospitalini nasi
tukarudi nyumbani.
Baada ya siku nne kupita bila kwenda chuo
kutokana na Matatizo ya familia, siku hio tulikuwa
tumekaa sebuleni Mimi na mdogo wangu ndipo
Latina akaniambia: dada pesa ni ndefu Sana sasa
Kama sindano moja ni Elfu stini hio gharama
tutaiweza kweli?
Nikamjibu: kesho twende chuo mambo mengine
tutayajuwa Baadae.
Latina: tunaendaje chuo na Hali ya familia Ipo hivi?
Nikamjibu: shule tuliifanya mkombozi Wa familia
yetu Acha tusome baba Ndo anavyotaka
ikiwezekana nikahitimu mambo yote yatakuwa sawa
Najuwa baba nikimtoa jela Halafu mama akamuona
basi atapona na familia yetu itarudi kwenye furaha
kama mwanzo.
Latina: sawa.
Siku iliofuata tulielekea chuo, kizuri sote tulikuwa
tunasomea science hivo chuo kilikuwa kimoja
tulipofika tulishangaa kukuta maandalizi sio ya
Kawaida mpaka tukashindwa kuelewa ndipo mdada
Rafiki yangu Jina lake Joyce alikuja tulipokuwa
tumesimama na kusema: come on Najma mbona
hivo?
Nilitabasamu na kumjibu: Kwani nipoje?
Joyce: Jana nakupigia haupokei simu why?
Nikamjibu: mama yangu amechanganyikiwa Baada
ya hukumu ya baba Ndo maana siku hizi sifiki chuo.
Joyce: Oohh my God pole Sana my dear.
Nikamuuliza: kuna nini mbona Mishe Mishe Sana?
Joyce: my dear hapa tuna ugeni mkubwa Si
unamjuwa Yule specialist mkubwa hapa Tanzania
kwa maswala ya upasuwaji wa moyo! atakuja
kutembelea chuo chetu Leo na atatoa somo kwa
masaa ma wili Baada ya hapo anaenda England
aisee Najma yaani sio Mimi ntaona Nimeiona sura
yake naskia watu wanamsifia ni kijana mdogo
mdogo tena handsome.
Nikamjibu: tatizo you talk to much.
Joyce alicheka kisha akaondoka zake kwa maringo,
Latina aligeuka kuniuliza: mbona hukutaka
kumsikiliza?
Nikamjibu: Nina raha gani?
Latina: Ila huyo specialist wa masuala ya upasuwaji
wa moyo unamjuwa? maana nahisi atakuwa peke
yake hapa Tanzania nzima kama atakuwa mbongo.
Nikamjibu: Anaitwa Derick ni mwana science
mkubwa alisomea wingereza anauwezo mkubwa
Sana na nitegemezi nchi nyingi za Africa mpaka ma
ulaya.
Latina alishtuka na kuniuliza: ulijuwaje?
Nilimpita huku nikimjibu: niliambiwa na teacher.
Latina alitabasamu kisha akanifuata kwa nyuma.
Baada ya muda tulijipanga freshi baadhi ya
wanafunzi walisimama mkono wa kushoto Wengine
mkono wa kulia katikati kuelekea ofisini kwa
mwalimu mkuu walitandika red-carpet Chini ili ugeni
Huo mkubwa tuuoneshe kuwa tunaujali sana, nikiwa
nimesimama mawazo yalienda mbali
nikamkumbuka mama hali alionayo nikajikuta
nakosa furaha kwa dakika mbili, Latina akiwa
amesimama upande wa pili aliponiona Nimeingia
kwenye emotion mbaya alinipa moyo kwa
kunionesha dole gumba ndipo nikatabasamu na
kumrudishia dole gumba, muda Huo kwa mbali
tuliona gari za kifahari kama tatu, watu macho
yaliwatoka wakitamani kujuwa Nani anaekuja Ila
Mimi sikuwa na habari nao.
Gari Zile zilipakiwa sehemu maalumu kisha
wakatoka vijana wawili na Wazee wa nne, walipofika
pale red-carpet inapoanzia walitabasamu kwa furaha
kisha wakaanza kupiga hatua huku wakisalimia
mwanafunzi kwa mwingine kupitia mikono,
wanafunzi walipomuona Derick walitamani Sana
kumuuliza maswali mengi kuhusu science ila muda
ulikuwa bado, mdogo wangu Latina alipomuona
Derick alijawa na tabasamu isio ya Kawaida ila
Mimi hata kupoteza muda eti nipo nawatazama
wala.
Derick kila mwanamke Aliekuwa akimpa mkono
alionekana kushoboka Haina mfano, Derick alipofika
mbele yangu na kuiona sura yangu alishtuka Ila
Mimi nilijifanya kumpotezea ndipo akanipa mkono,
Nilimpa bila kujali ndipo akaushika mkono wangu
kwa dakika mbili huku akinitazama usoni Mpaka
kila mtu hapo akashangaa kwa kile kinachoendelea,
aibu ilinitawala nikaamua kujikohowesha ili aniachie,
ndipo akaniachia na kuendelea bila hata
kuwasalimia wanafunzi waliokuwa wamebaki maana
alionekana kuchanganyikiwa baada ya kuniona,
Baada ya muda Wageni wakiwa wapo ofisini kwa
mwalimu mkuu Latina alinifuata na kuniuliza: hivi ni
wewe Wa Muda ule?
Muda Huo alifika Joyce na kuniuliza: Najma it's
you?
Niliwapotezea nikaamua kuondoka zangu.
Baada ya muda somo ilianza na Aliekuwa
akiendesha somo alikuwa ni Derick, wana science
wote kuanzia mwaka wa kwanza kuendelea tulikuwa
kwenye class moja, nikiwa nimekaa na mdogo
wangu Latina nilimuambia kwa sauti ya Chini:
tukitoka hapa twende magereza kumuona baba ili
tumpe taarifa kuhusu mama.
Latina: Nikweli ila hujaniambia Derick Muda ule
alikuwa anakuambia nini?
Nikamjibu: Potezea.
Latina: Mbona sasa anabaki anakutazama Muda
wote?
Nikamjibu: kama huwezi kusoma toka nje.
Latina: sawa basi yaishe.
Derick alianza kuzunguka darasa taratibu, alipofika
nilipo alisimama kama vile kuna jambo anataka
kuniambia, muda Huo watu wote waligeuka
kumuangalia Derick huku kila mtu akijiuliza maswali
bila kupata majibu, Na mimi Muda Huo nilijikausha
kama vile simuoni, Derick uzalendo ulimshinda
akasogea kwenye dawati yangu akaweka mikono
huku akinitazama usoni, Latina alishtuka mpaka
akabaki anashangaa ninavyompotezea, wanafunzi
hawakuamini haswaa Mabinti wenzangu, Derick
alishusha pumzi kwa kasi kama mtu mwenye hasira
vile, Na mimi wala sikumpa muda macho yangu
pembeni tu, ndipo Derick akaniuliza huku akiwa
yupo serious: Kwa nini unanifanyia hivi?
Latina uzalendo ulimshinda Akajishika kwenye
mdomo ishara ya mshangao, bila wasi wasi wala
kuteteleka nikamjibu: Kwani wewe Nani?
Wanafunzi waliokuwa nyuma yetu hawakuamini,
Latina alishindwa aseme nini akajibu pahali yangu:
muelewe ana matatizo Muda huu.
Latina alinigeukia na kuniambia huku akiwa
amebananisha meno: Ndio nini sasa mtu mkubwa
Kama Huyu kumjibu utakavyo?
Sikumjibu Niliendelea kufanya inshu zangu ndipo
Derick akasema: unanipa wakati mgumu Sana, kila
siku nafikiria Upo wapi Kumbe upo hapa hapa
Tanzania why hukunitafuta?
Nikamjibu: Kwani Mimi nakuhusu tena?
Derick: somo ikiisha usiende bila kuonana na Mimi
please!
Derick Alichukuwa kauntbook yangu ajabu akaandika
namba, alipomaliza Akaniambia: this's my fone
namba please ni call kabla ya kwenda nyumbani.
Derick aliondoka wala hakutoa somo tena alitoka
moja kwa moja nje ndipo akaingia mzee waliekuja
nae ili kuendeleza somo, wanafunzi walitamani Sana
kuniuliza maswali kadhaa Ila kwa kuwa soma
nyingine ilianza waliamua wakaushie, muda wote
Latina macho kwangu Mpaka akashindwa aniweke
kwenye Aina gani ya binadamu.
Simo ilipoisha tu! wanafunzi waliniwahi kama wote
maswali yalianza kutoka kila kona * Najma
ulimjuwaje Derick *
*Najma ulikuwa unajuwana nae kabla na Derick *
*Najma mbona kakushobokea sana Kulikoni? *
Nilinyanyuka na kusema kwa sauti ya Juu: Simjui,
hanijui mniacheeee.
Niliwapita nikatoka zangu nje huku Joyce na Latina
wakiwa wananikimbilia, waliponifikia Joyce alisema:
Shostiii Mbona upo hivo?
Nikamjibu: nipoje?
Joyce: why hili swala unalikwepa sana Huyu mtu
mnajuwana Eee???
Latina akadakia: dada sema ukweli bwana Mbona
kama vile anakujuwa sana na wewe unamjuwa Sana
Ila ukaamua kumpotezea na Kwa nini Sisi watu
wako wa karibu hutaki kutwambia?
Joyce: wallah atuweke wazi Nipo nakuambia Derick
mpaka walimu wametamani namba zake
hawakuzipata ila wewe kirahisi rahisi hata
Haujamuomba amekuandikia unajuwa hata Watoto
wa maraisi wanatamani Sana kufanyiwa
alivyokufanyia, wallah siwezi kukuelewa.
Nilipaza sauti kwa hasira huku nikiwajibu:
niacheniiii! Eti Watoto waraisi wanaitamani nafasi
ile, hivi wewe unawajuwa Watoto waraisi vizuri?
sasa kwa taarifa yenu naondoka na sitampigia
kwanza na namba nachana.
Nilichana ile karatasi iliokuwa imeandikiwa namba
ya Derick kisha nikarudia nikachana Chana vipande
vidogo vidogo kwa hasira na kutupa Chini, Latina na
Joyce walibaki wameachama kwa mshangao ndipo
nikawapita na kuondoka zangu.
Nikiwa nipo njiani naelekea magereza machozi
yalianza kunitiririka nikasema:........!!!!!
Unahisi nini kitatokea!
Usikose mkasa huu!
Ukiihitaji yote kwa haraka unanunua kwa Elfu 2
namba 0l+255757449871.
TANGAZO!
Simulizi hii itakuwa inarushwa Mara mbili tu kwa
wiki ijumaa nne na ijumaa.