Simuelewi wifi yangu

MamaBeata

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2013
Posts
325
Reaction score
112
Wifi yangu amekuja juzi. Ni dada wa mume wangu. Alipofika sikuwepo nilikua kazini. Nilipofika toka kazini nikamkuta amelala. Nikamsubiri alipoamka akaja tukatambulishana tukaendelea na maongezi.

Jana siku ya pili kaamka kaoga kawasha tv, akitoka anaenda kulala. Anaamka anakula anarudi kulala. Leo siku ya tatu ameamka mapema tu ameoga karudi tena kulala. Mwenzenu Simuelewi huyu mwanamke mwenzangu hata mlango wa jikoni haujui. Nimekua kama nina waume wawili. Kuolewa kuna shida wenzangu.
 
Huyo ni mtu mstaarabu sana sababu hapo ni kwako sasa akikurupuka mpaka jikoni wakati hajakaribishwa ungesema anakuingilia!!!!!!!
Either ways wewe siku ya tatu tu ushaanza mpaka ku post huku, je angekuja mgonjwa kukaa hapo mwezi mzima!!!????
Kwanza wewe mtu wa kazini so hushindi hapo kazi anafanya dada labda sasa wewe nini taabu yako!!!!???
Leo wkend kesho sikukuu muamshe mwambie mwende sokoni mkanunue vya kununua na mkija fikia naye jikoni mpe nyanya muombe akusaidie wakati wewe unafanya mengine then anzisha story kuwa uko happy kwa ujio wake sababu sikukuu mtapika vyakula mbalimbali kwa kushirikiana, mtamaliza mapema na ku enjoy.................


Sikuhukumu ila ni kama hupendi ndugu wa mume au una ghubu flani kama sio mvivu..........ungekuwa mke wangu ningekuchana live!!!!!
 
Kuwa mpole na mvumilivu,inawezekana anakujaribu kuona kiwango cha uvumilivu wako.Usimpe sababu.Vumilia
 

Umekaa ukaongea nae chochote?kwa mazingira yapi
 
Wee usitafute ugomvi nae mwache tu akae, mwisho atajistukia mwenyewe ataondoke ama ataanza kufanya kazi!
 
Nadhani atakua na miaka 20 na kitu hivi. Ni mwalimu wa shule ya msingi hajaolewa bado
 
Brother shikamoo!!

Asomaye na Afahamu.
 
huyu mwanamke inaonyesha hapendi upande wa mume,maana sioni kama kuna baya hapo alilofanya huyo wifi yake,afu pia nina wasiwasi na utimamu wa akili ya huyu mtoa mada kama anajua majukumu yake(kama mke)...inabidi akafundwe upya huyu...
 
Mi kwa kweli jikoni kwangu ndiko ufalme Wang ulipo.naamini hivyo hats nikienda kwa mtu.
Unless uniambie njoo tupike.
Kila nyumba na kila mwanamke ana namna yake ya upishi.
Sitegemei mdada analilia mtu kuingia jikoni kwake.
 
Nadhani atakua na miaka 20 na kitu hivi. Ni mwalimu wa shule ya msingi hajaolewa bado

hyo sio busara hayo mambo madogo sana umemkaribisha jikon kakataa?! Sk nyingne hayo ndiyo wanaita majungu.. Usirudie kueleza kwa watu tabia za ndg mapema hvyo. Kaa naye mpe mpango kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…