Simuelewi my X anataka nini!!!!!

Kaka jaribu kuwa na subira njia ya mwongo huwa ni fupi. Wewe waache waendelee kuchat jifanye kama there is nothing happened , Ila kuwa mwangalifu usidisclose mambo yako na mipango yako kwa mdogo wako maana inaonekana huyo dada anamtumia mdogo wako kukufuatilia. Wapotezee!
 
Huwa wanasema watu wakiachana ushemeji haufi lakini bado dogo anatakiwa atumie busara kwamba yule alikuwa awe shemejie lakini kakake ameshaachana nae so nionavo mimi dogo anatakiwa kupunguza mawasiliano na huyo dada, wanaweza kuendelea kuwasiliana lakini si kihiiiivyo. Lakini upande wa pili naona huyo dada anazidisha mawasiliano na dogo ili tu akurushe roho hana lolote.

Sasa wewe unatakiwa umrushe roho kwelikweli kwa kufanya kweli (kumuoa huyo dada ambaye umeshampata)
 
Usifanye makosa ya kumrudisha mdogo wako Bongo...Ni aje wewe? :rant:
 
Unajua kuna jambo moja amblo ulikosea toka mwanzo,wewe ndiye ulimuintroduce huyo mwanamke kwa mdogo wako,wakawa wanawasiliana,tayari waliishajenga "Bond" ambyo wewe kuivunja ni ngumu, vilevile ujue wao hawajagombana ,ila wewe ndio umegombana na yule.sasa unapokua unampiga bit dogo unamuonea.Wanawake huwa ndipo wanapotuweza ukiisha mtambulisha kwa ndugu zako huwa wana wawin kwanza ndugu.Siku wewe utakapokuja na mawazo tofauti hautaeleweka.Ulikosea kumtambulisha kwa mdogo wako wakati hukuwa na uhakika wa kuendelea nae.Na hiyo ni kwa wengine wajifunze kuwa unapofikia hatua ya kumtambulishamme/mke kwa ndugu zako lazima uwe na uhakika uhusiano wenu umefika mbali.Sio mtu umelala nae siku moja mbili,tayari ushamtambulisha ,kesho unatambulisha mwingine ,hata ndugu zako watakuona unamatatizo.
Kwa ushauri wangu kama uliamua kumsaidia mdogo wako ,endelea kumsaidia lakini sio kwa sababu anachat na x wako ndio umrudishe home.Maisha ya mapeni huwa hayana formuala,pengine ndio Mungu alipanga wakutane kupitia wewe.wakipendana hiyo haikuhusu,kumbuka dogo anafeelings tofauti na wewe hata kama mmetoka tumbo moja.unaweza ukawa unafanya hivyo kumsaidia lakini kumbuka mwisho wa siku mko tofauti.
Imetokea mara nyingi,mtu anaenda kuoa familia fulani,akashindwana na dada mtu akaoa mdogo mtu na maisha yakaendelea.
Usije ukajaribu kumrudisha mdogo wako sababu tu ya huyo demu,nakuhakikishia huyo dogo hiyo kitu haitamtoka maishani mwake,kwani tayari ameishakua na matarajio fulani ya kimaisha, utakapoikatisha ndoto yake maishani na wewe siku mambo yakikuendea kombo utakuja juta.
 
Ahsanteni sana member wenzangu kuna vitu nimejifunza hapa nashkuru woote kwa jumla'
 


Yericko nimekupata mkuu'wala usijali maisha yanasonga'lakini ipo siku naamini kama tutakuwa hai nitaleta uzi wa huyo bint na dogo watapofikia,kwa sbb mm naamini anataka kumtumia dogo kwa faida yake,ambacho hata mimi nimeshampa warning dogo'
 
pole sana ndugu yangu jaribu kuongea na x wako vizuri ili umwambie aachane na mdogo wako afanye maisha yake hy sio tabia nzuri anayofanya huyo mdada hata kidogo
 
nakubaliana na wewe. kama kweli hawa wawili wamependana basi wasingepoteza muda wa kumponda huyu bwana mkubwa ktk mazungumzo yao. wote huwa tunabadilisha mahusiano , lakini ktk mauhsuiano mapya tunapeana upendo kwa kuwaponda waliopita? wanaomwita huyu mkubwa mbinafsi wamwite , ni maoni yao. ila mimi ninamkosoa tu kwa kusema amtudishe dogo, kumrudisha si sawa, bali ampe muda dogo atafute makazi yake. lakini hili la huyu mwanamke anania mbaya na hawa ndugu ninaweza kulikubali kwa kiasi fulani.
 
NGOSWE Penzi "Kitovu Cha Uzembe" aftrol tupo kwenye mwezi mtukufu...tupa kule tafta mwingine
 
kaka presha ya nini. just sit back and watch the show between those two......kaa kimya, usimrudishe hom mdogo wako, muache tu aendelee na huyo dada, yakimshinda si utajua tu?ukimrudisha hom kisa huyo dada utaonesha udhaifu wako sasa! kama ulimwaga totally, kauka kimya acha dogo ajiachie, ila kama ni partially, kazi unayo mkuu!
Paka hiyo sio bahati'kwa sisi wafrica huo si utamaduni wetu kuchukua mwanamke m1 family nzima,na faham kuwa huyu alikuwa ni mchumba wangu'
Na huyu ni mdogo wangu,
 



Ama kweli WAHENGA WALISEMA: Mwalimu wa wanawake ni Kipofu......ndo haya sasa unayoyaongea yamethibitisha: Naomba unijibu swalihili Kaunga Please:- " INA MAANA KUWA WEWE MUME WAKO AKIKUPIGA CHINI/ AU BOYFRIEND WAKO AKIKUMWAGA .....MAZIMA.....UPO TAYARI.....KUMDOWNLODIA HIYO PANTS/kufuli shemeji yako wakiume na ale mzigo kama kawa kisa eti wewe umeachwa na bro wake??? Tell us ili tujue jinsi wanawake mlivyochanganyikiwa na mapenzi ili wote tuone mpo sawa tu!
 
Huna hoja iliyokomaa ya kumrudisha dogo hme zaid jipange
 


Ni kweli binadamu tunatofautina tabia,utashi,na hata haiba,ila kwenye wengi hakiharibiki kitu,nashkuru kwa ushauri wa wana jamvi'
 
Kitendo anachofanya huyo mwanamke ni ishara tosha kuwa ulifanya uamuzi sahihi wa kumwacha. Inaonekana hana maadili mema na hata kama huyo dogo atamchukua ataishia kupata shida tu kwani mila na desturi za kiafrika haziruhusu.
 
Dogo hana adabu hata kidogo yaani anataka X wako awe shemeji kweli kizazi hiki kimelaaniwa
 
ningukuwa wewe ningemuambia dogo ukweli kwamba akiendelea kuwasiliana na huyo x nitamrudisha bongo ili waendelee naye,then kama ataendelea kuwasiliana naye atajua kifuatacho ni kurudishwa bongo
 
We si ushafanya yako,km vipi mwache dogo nae afanye yake ila usijekubali huyo mwanamke awakosanishe nyie ndugu
 
Kwa mtazamo wangu huyo mwanamke anamtumia Mdogo wako ili awe karibu na wewe(kwa mfano taarifa kuhusu maendeleo yako Huko uliko)
Kama Dogo ataamua kuwa Nae kimapenz basi ni dhahir Hana adabu kabisa,ushauri wangu mueleweshe Mdogo wako unavyojisikia vibaya kwa Kitendo cha yeye kuwa na mawasiliano ya karibu na x wako..asipokusikia muache atajifunza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…