Simuelewi mtu huyu

Waswahili tunasema; "Pema ni pema usipopema, ukipema si pema tena"
 
Nimeamini kweli wanaume ni wabinafsi,pamoja na yote hayo bado anakuomba msamaha? angekuwa ni yeye wala asingekupokea na hata ushauri asingesikiliza,ila wewe ndio mwenye maamuzi
 
kama kuna uwezakana wa kumrudishia mahar na posa yake mrudishieni ili asikusumbue kabxa,,
but kama unahtaji kurudia tena makosa,rudiana nae.
ila kama aliweza kukfukuza mwanzo hato shindw kukfukuza tena,,kaa ukiljua hilo.

ushaur wang kwako kiki14 we songa mbele na maisha yako and never look back.
 
Wanaume wa hivyo wengi huwa hawabadilika tena kadri unavyomsamehe na kurudi kwake ndo anakuwa worse zaidi, kwa mtazamo wangu kwa vile umeshaweza ku move on ni bora kutorudi nyuma, ila wewe ndo unaeielewa situation zaidi kwahiyo fanya vile moyo wako unavyoona, lakini am sure ukirudi kwake mwaka hautaisha utarudi hapa tena kutafuta ushauri mwingine
 
Kuna mambo mengine huwa siwezi kabisa kushauri, hususani kisa kama hiki alichokileta bi mkubwa huyu....
 

Tunaishi mara moja dia baada ya kifo hatujui kama kuna maisha mengine na kama kufa uje kufa kwa ahadi ya mungu sio kwa pressure za kusababishiwa na mtu,fanya maisha yako lea wanao ye abaki kama mzazi mwenzio bt kama roho bado inapenda rudi shosti,Ni ushauri tu jamani ifike mahali ujue unasimamia wapi
 

pole sana,binafsi wakati mwingine huwa nashindwa kutoa ushauri kwani sijasikiliza stori za upande wa pili.anaweza akaja na yeye na stori tofauti kabisa tukashindwa kujua nani mkweli.anyway,mnaweza mkaishi pamoja na kulea wanenu
 

Kaa mbali nae hakufai utapoteza muda wako na utaishi kwa stress, If someone can't treat you right, if someone can't love you back let it go
 
Mkuu kiki 14

Wewe ndio mwenye maamuzi, hapa hakuna anayejua mazuri na mabaya ya huyo mwenzi wako. siri umeibeba wewe, mpaka uliacha kazi sababu yake, ukazaa nae, ukaishi nae nje ya ndoa kama mke na mume.....hii ni ishara tosha kwamba umeridhika nae. Chukua hatua na chukua maamuzi sahihi na tahadhari kuu.

Au, kama mlitaka kufunga ndoa, hakikisha mnakamilisha hilo halafu ndio unaenda kama mke sio kubebana tena. Mpe hayo mashart ya kuona kwanza ili familia ziwaelewe.
 
Last edited by a moderator:
Dada wanakupotosha tu humu utaachana vipi na mtu uliyezaa naye watoto wawili.......

Mimi nakushauri mambo mawili tu.
Mosi kwa kuleta hili hapa inaonesha bado unamuhitaji na wewe ,hakikisha hamrudiani Bali kwa ndoa halali ya kidini aukiserikali
Bila Ndoa usirudi.

Pili kazi usiache kamwe ,baada ya ndoa mmoja wenu atafute uhamisho au kutafuta kazi mpya......ila usiache kazi kabla hujapata kazi ,asikufanye mtumwa wa mahusiano.
 
inaonyesha huna maamuzi dhidi yake asee
na inavyoonyesha una nia ya kurudi kwake tena which means utaacha kazi kwa mara ya pili

hakika hatobadilika
na utajutia kuacha kazi tena
 
Habarini kwanza, naombeni ushauri kwa hili.
Niliacha kazi kwaajili yake maana tulikuwa tukaa mikoa tofauti ila sasa hivi nimerudi tena kazini ila yeye mpaka sasa hajui kama ninafanya kazi nimfanyaje mtu huyu.

Kwanza msamehe bure...Kisha mwambie akuhakikishie amebadilika. Na angalia mwenendo wake katika malezi ya watoto ili ujue anajitambua kama baba ama bado ni boyfriend.

Pili tell him to man up. Achukue majukumu yake kama mwanaume akupose officially, mbariki ndoa muwe na vyeti. Na atume Workable Proposal ya maisha yenu ya ndoa alivyojipanga na iwe na viambatanisho stahiki. Akupe heshima yako kama mke.

Ni hayo tu mwaya!
 
ulikosea sana kuacha kazi kwa sababu isiyo ya msingi
 
usirudi dada angu, ataenda kukuchinja.
 
mpaka umekuja huku,,,, una lako jambo.....mwambie aache kazi akufuate..hahahahahaaaaa,,,,,tumia akili zako, changanya na busara za watoto wenu jumlisha na hekima za wazazi.....songa mbele...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…