Simuelewi huyu shemeji mwenzenu

four eyes

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
904
1,399
Nimeoa na nampenda mke wangu sana tu, pale kwao kwa baba na mama kuna wapangaji wao kadhaa wa vyumba vya uwani.

Mmoja kati ya wapangaji hao ni rafiki wa mke wangu na kila tukienda hapo kusalimia wakwe huwa namkuta nae akiwa anaendelea na shughuli zake binafsi zaidi ya salam mimi sinaga story nae.

Siku za hivi karibuni amezua katabia ka kunisifia sana kwa mke wangu akidai umbo kangu la mazoezi linamchanganya sana(nina kawaida ya kupenda mazoezi hasa push ups za kila siku)

Mwanzo alipomwambia huku namsikia nikiwa nje ya nyumba wao wakiwa sebuleni nilidhani masihara yao tu ya kawaida lakini juzi nilienda kwa wakwe kufata vitu flani akaniona, cha ajabu akamtumia SMS mke wangu kwamba kaniona na anadata kweli na umbo langu.

Nashindwa kumuelewa kwanini anamueleza mke wangu hivi vitu na kwa nia gani, na kweli akiniona kuna jicho flani ananikazia, nachoshindwa kuelewa ni je kama kweli ananitamani kwanini amwambie mke wangu? Na kama ni utani kwanini auendeleze na kwanini kweli akiniona ananiangalia sana?

Huwa najaribu kumjibu mke wangu kuwa huo ni utani tu hamaanishi kitu lakini yeye huwa ananiambia anamfahamu vizuri tabia zake na kwamba yuko serious hapo.

Huyo dada ni mke wa mtu pia, je nimbutue au nipotezee? Kimuonekana mashallah ana guu la bia na tako la kutosha tena lainii japi sura sio kivile, nikimtathmini kimuonekano anafaa sana tu kwa matumizi.

Ushauri wadau please huyu ana nia gani? Na kwanini anamwambia mke wangu? Je nibutue japo Mara moja halafu basi au nikaushe?
 
Eti anamwambia mkeo Wanawake unatujua wachana na Hiyo habari kabisa sijui kufaa kwa matumizi
 
Empty set ww..wanawake wanaongea unaenda kula chabo kusikiliza

mkeo anakudharau anakuona kikatuni cha Kipanya

We endelea kupiga push up tu na kulala kwa wakwe zako
 
Hata wewe Heleweki pia.
Kwasababu unasema ni yeye ndiye humuelewi lakini umeshamthaminisha eti anafaa kwa mlo...

Kwani hujui kama Mume wa mtu unapaswa kuyashinda majaribu?

Mke wa mtu ni sumu, chalii yangu.
 
acha mawazo ya um.@l@ya chief....
ss kila mwanamke akikusifia na kukuangalia kwa hilo jicho utalala na wangapi.!!? jifanye mjinga tu.
 
Ukishatibua alafu ukimchunia atamwambia tena wife wako,
Kuwa mtu mwenyewe mbeba vyuma bure kume hana marinda na kibamia juu, nayo atakuwa anamtania tu!
 
Yani umekosea tu kutunga hapo uliposema anamwambia mkeo badilisha weka neno lingine
 
Wanaume walio wengi ndio zenu hizo yaani hamjuagi kumwambia mtu wazi hasa akishakuwa mwanamke hivyo hata sishangai.

Piga moyo konde mwambie uwazi kwamba mkeo hapendi hizo sifa anazokupa.
 
Back
Top Bottom