Mkuu Edison, pole na yaliyokukuta! Kwanza rejea kwenye ukweli kwamba mwanaume ndiye kichwa cha familia katika mji wowote, yeye ndiye mwenye majukumu yooooote ya kifamilia, hili ni compulsory na wala halina option! Utamaduni uliojengeka hasa katika jamii zetu hizi za kiafrika ni kwamba, mama halazimiki kuwa bread winner of the family, hasa kama baba yupo, tena akiwa mzima mweye afya! Hivyo,mwanamke yeye ana opton katika kuitunza familia as they consider it not being their mandatory task, regardless uchumi wa mke ni mkubwa kiasi gani ukilinganishwa na wa mumewe! Imezoeleka hivyo, na ndivyo wafanyavyo wanawake walio wengi Afrika, na hata karibuni dunia nzima! Imeandikwa katika vitabu vya dini, "Enyi wanaume, ishini na wake zenu kwa akili". Mkuu stuka usingizini!-
MY TAKE!
-Mkuu kama ulioa mtumishi kwa maana ya kuwa upate unafuu wa maisha, hilo liondoe kwani linategemea saana mtizamo wa mkeo, inawezekana yeye anawathamini na kuwajali zaidi ndugu zake kuliko wewe! Ieleweke kuwa, wapo wanawake waandaao future zao somewhere else kusikojulikana na waume zao! Hii ni hatari zaidi kwani kufanya hivyo logically kunamaanisha hana mpango wa kuendelea na wewe hapo baadae, na nina hisi mkeo hili ndo alifanyalo so longer hauelewi transaction za pesa zake zinaelekea zaidi kwa dada yake bila wewe kujua nini sababu ya yeye kufanya hivyo!
Pili, jitahidi saaaaana uishi -na mkeo pahala pamoja! Hii mambo ya eti uko Dar, yeye yuko Musoma ni uongo! People do change bhanaa... sie binadamu tunashawishika! Inawezekana tayari mapedesheee wameshamvuruga akili ndo maana anakujibu hovyo! Angelikuwa nyumbani uko naye kila leo, ingelikuwa ni rahisi kuitambua na kuidhibiti mapema mienendo yake usiyoridhishwa nayo!