mtoto mpole
JF-Expert Member
- Mar 22, 2010
- 678
- 148
Simu ya mkononi ni kama roho ya pili ya mtu ukitaka kumjua vizuri mtu chunguza sana simu yake ya mkononi....
sasa naomba kujua kwanini wanandoa wengi hawapendi mume/mke ashike simu yake kuna nini zaidi kwenye hizo simu?
simu za mkononi imekua janga la kitaifa hasa hizi smart phone utakuta mume yupo busy na simu hata muda wa kulala alafu bila aibu utakuta anajiongelesha kwa mkewe yaan dah me addicted na twitter siku hizi hivi ni kweli haki hii jamani......nini kifanyike kukomesha hii hali yaan mimi nakasirikaga sana na haya masimu...
hoyeeePole sana inabidi uende na kazi ya technology smartphone hoyee
simu ya mkononi si majanga majanga ni mwenye simusimu za mkononi kweli ni majanga maana kuna watu tayari ndoa zimevunjika, wengine wameshapata ugonjwa wa moyo n.k ila nakupa pole sana kwa kukosa raha kisa simu ya mwenzio..!
simu si tatizo.....
simu ya mkononi si majanga majanga ni mwenye simu
Mkuu hizi tabu zinatokea kwenye ndoa ambazo hazina uaminifu,either kati wanandoa anacheat au wote wanacheat.Ndoa ambazo hazina migogoro na kuna uaminifu swala la kushika simu ya mwenza ni kawaida sana.Thanks
Tatizo si wakati wote kuna ukosefu uaminifu katika ndoa ila kutumia muda mwingi kuchat na simu wakati mwingine kunapunguza mawasiliano katika ndoa.Unakuta mume karudi toka kazini badala ya kukaa na mkewe waongee wapeane habari za matukio ya siku hiyo na pia kuzungumza na watoto, badala yake mtu yuko busy na simu.