Simu vs haki ya usiri kwa wanandoa


...mkuu Bujibuji nimerudi,nilikuwa mbali sana. kwanza si kweli kwamba haki ni kitu mtu anachozaliwa nacho,pili si kweli kwamba kila mtu anahaki ya kutunza siri zake hata ikiwa za namna gani. kwa mtazamo wangu mimi siri za mtu zinatofautiana kulingana na uhusiano wa watu husika. mfano kwa suala la simu, isipokuwa pale tu endapo simu itakuwa na mambo ya siri ya kikazi ambayo mweni wako hatakiwi kuyajua(hapo tu ndo simu itakuwa siri) lakini kwa namna yeyote mke anakila haki ya kuaccess simu yaako na hii ndiyo maana ya mwili mmoja, kwani kuna lipi la kuficha kwenye simu...?je ni jambo gani la ndugu zako unalolifanya ambalo mkeo/mumeo akijua inakuwa hatari kwako..?

kuna siri gani kubwa zaidi ya mke/mume kuvua nguo mbele ya mwenzi wako na akawa kama alivyozaliwa...?, lakini hili tunalifanya bila kuhoji tukijinanga ni halali yangu si mke/mume wangu...!! na kwanini simu iwe tatizo...?

mkuu bujibuji kwa heshima na taadhima nipe mfano wa jambo moja tuuuu, ambalo mke wako hapaswi kulijua kwenye simu yako nami nitakupa sababu kuwa si usiri bali kuna kitu zaidi ya "siri"....
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…