ccr airtel
Member
- Mar 27, 2011
- 96
- 14
unaweza ukawafikiria vibaya watu wa hivyo ila hiyo inatokana na namna anavyohudumiwa.unaweza kukuta mteja mwingine kazi yake kupiga tu namba 100 na akipokea mwanaume anakata (shida yake ni wadada tu)...
AHSANTENI SANA WADAU KWA KUCHAGUA AIRTEL KUMBUKENI WEEKEND OFFER SALIO KUANZIA 1000 UKIONGEZA UNAPATA 10 MINUTES FREE,100 SMS NA KIFURUSHI CHA 200MB KUANZIA SAA NNE USIKU HADI KUMI NA MBILI HASUBUHI
kumbe hii kitu imehamia na kuwa ni kwa w/ends.....sasa mbona hamtujulishi wateja kuwa mambo yamebadilika......halafu hizi offer za 200mb zinawekwa usiku namna hiyo kwa nini isiwe kuanzia hata saa 2 usiku? kwa muda wa maongezi kidogo sawa......ni maoni yangu tuu lakini
wateja raha ilipokua saa sita walisema kwann isiwe japo saa nne saiv wanataka saa mbili...ila ni maoni na lazimayaheshimiwe...kumbuka kama utaweka vocha iwe ni ya 1000 sio mia tano 2 na kuweza kutumia ofa yako salio liwe zaidi ya sh 4
Ndugu wadau tatizo ni kwamba kupiga simu huduma kwa wateja ni bure so kuna wateja wengi wanapiga simu hasa wa maeneo ya kishapu,katesh,babati,shinyanga,mtwara (haswa masasi),rorya,tandahimba...Hawa wananchi anaweza akapiga simu (ofcoz anapokelewa kama mteja mwingine yeyote anavyopiga coz huwezi jua shida ya mtu au kujua huyu mtu atauliza nini hadi atakapotamka tatizo lake),kisha anakwambia nilikua nataka kukusalimia tu,au naomba nitumie japo 200 ndugu yangu sina kitu kabisa (hapo ana salio la 500),au akakwambia nilitaka tu kujua saa ngapi, au mwingine anasema,au tatizo jingine kubwa tunalokabiliana nalo kwa sasa ni wateja kuuliza maana ya 200MB (kifurushi cha intanet cha ofa baada ya kuongeza salio),kuna mteja mimi binafsi aliwahi kunipigia simu anataka tuombe coz huko alipo kuna tatizo lamtandao...na hii yote ni kwa sababu huduma ni ya bure with no limitation,au unaweza kukuta mteja mwingine haweki salio kazi yake kupiga tu namba 100 na akipokea mwanaume anakata (shida yake ni wadada tu)...ila ukweli ni kwamba kwa siku wafanyakazi wanaokua online kuhudumia wateja ni zaidi ya 350 na bado wanaongezwa na kila mmoja anapokea wastani wa simu 165 wastani wa dk 2.5 kwa simu...AHSANTENI SANA WADAU KWA KUCHAGUA AIRTEL KUMBUKENI WEEKEND OFFER SALIO KUANZIA 1000 UKIONGEZA UNAPATA 10 MINUTES FREE,100 SMS NA KIFURUSHI CHA 200MB KUANZIA SAA NNE USIKU HADI KUMI NA MBILI HASUBUHI
kiukwel airtel mmeanza kuwa wababaishaji kama hawa ndugu zetu wa kigali kidogo.zamani ilikuwa ukipiga simu airtel unapokelewa haraka sana.mimi nilishapiga simu siku mbili mfululizo bila kupokelewa na mtu yeyote yule.tatizo kubwa nilikuwa sipati comfirmation sms ya bundle ya mb 400.siku ya tatu akapokea sharo baro akasema hajui jinsi ya kunisaidia.nilikaa nikaja kupata msaada kwenye ofisi ya huduma kwa wateja baada ya miez miwili tangu tatizo litokee.jirekebisheni.na wala usinibishie nasema ukwel mtupu!
Hamna kitu hapo, yaani watu wa marketing hapo ndio mnaona mmetoa offer, mtu aanze kutumia kuanzia saa nne usiku? nadhani offer hiyo mngewapa wanafunzi/wanavyuo kwani wao mida hiyo wanakuwa wako macho, lakini mtu kama mimi huduma hiyo hainifai..
mkuu juzi niliweka vocha za elfu elfu 3, sikuona message yoyote ya kuniambia kuwa nimepewa offer, au ndio imehamia hiyo weekend