Simu Feki: Kosa la nani, Serikali, Muuzaji, au Mteja?

a4apple

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
927
1,131
Ni dhahiri kuwa serikali kupitia TCRA imedhamiria kuzima simu feki ifikapo June 16, 2016. Lakini suala hili lina utata wa kisheria ya nani ashtakiwe na nani awajibike.

Serikali ndiyo yenye dhamana ya kudhibiti ubora wa bidhaa zote zinazoingizwa nchini. Hivyo kama kuna Simu feki nchini basi zimeruhusiwa na serikali ziingie. Kwa upande mwingine ni kosa kumtapeli mtu kwa kumuuzia bidhaa bandia. Hivyo muuzaji wa simu hawezi kukwepa hii lawama kwa kuwauzia wateja simu feki huku muuzaji akijua kuwa anauza bidhaa feki. Kwa upande mwingine: sioni kosa la Mteja.

Huyu mteja anatafuta kununua simu kutoka katika maduka yaliyosajiliwa na serikali na yanalipa kodi. Yeye si mtaalamu wa simu , hivyo hawezi kutambua simu feki na original. Kosa lake nini. Sasa serikali imeamua kumuadhibu mteja badala ya kumuadhibu aliyeagiza bidhaa feki na yule aliyeruhusu bidhaa feki iingie katika maduka ya Simu. Huu ni uonevu.

Serikali ilipasa kuja na mkakati kabambe wa kuwashtaki wafanya biashara walioagiza simu feki. Pia ilitakiwa kuwawajibisha mamlaka za serikali ambazo ziliruhusu Simu feki ziingie nchini. Pia serikali ilitakiwa itoe hatma kwa wateja waliouziwa simu feki ili pesa zao ambazo nyingine zimelipia kodi zisipotee bali serikali au wafanyabiashara wa simu yawabadilishie simu na kuwapa Simu original, mwisho serikali iseme simu feki zimeingiza kodi kiasi gani, na nini hatma ya kodi hiyo.

Kwa hiyo, mteja hana kosa. Kosa ni la mamlaka za serikali na wafanyabiashara wa simu. Wateja wapewe haki zao
 
Kwa uzoefu akili za kibongo zimekaa ktk kutoa sababu zaidi badala ya kutenda/kuchukua maamuzi.Acha simu feki zizimwe tena zoezi hili lisiishie kwenye simu tu
 
Kama serikali imeshindwa/ilishindwa kukulinda haina maana na wewe ushindwe kujilinda. Serikali ni wewe, madhara ya simu feki yanakulenga mtumiaji moja kwa moja
 
Kosa la Mwananchi
We uanunuaje simu fek,wakati ukiishika tu unaijua,cha kushagaza eti wa Mjini hasa DAR ndio wanaongoza kwa kupigwa sim fake.
Hii ni sawa na kusema kwamba Watoto wa mitaani kosa la nani?utasema la serikali?
Au watoto wa nje ya ndoa kosa la nani,utasema la serikali?
Tutakutana kesho kujuliana hali baada ya maumivu
 
Jamani, vitu vingine tusiseme serikali, serikali,
Wewe hapo humuoni mfanyabiashara, huoni mnunuzi kweli?
ok, serikali ni taasisi kubwa sema labda mamlaka/ ofisi moja wapo inayohusiana na mambo hayo ya simu.

Mmmmh, ila TANZANIA TUNAHITAJI CHAMA BINAFSI CHA KUWATETEA WALAJI/WANUNUZI WA BIDHAA, MAANA WANUNUZI WA SIMU WALIAMBIWA HII NI ORIJINO KAMA ORIJINO ZE COMEDY.KUWASAIDIA KUDAI FEDHA ZAO WALIZOUZIWA SIMU FEKI NA WAFANYABIASHARA.

Ni maoni tu jamani.

Haa haaaa jamani, mi simo!!
 
Back
Top Bottom