singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
SERIKALI imesema haitarudi nyuma katika jitihada za kushughulikia migogoro baina ya wakulima na wafugaji kwa lengo la kuimaliza kabisa na kuonya kuwa wote watakaobainika kwa namna moja ama nyingine, wamekuwa ni visababishi vya migogoro hiyo watashughulikiwa ipasavyo ikiwamo kuwavua nyadhifa zao kwa mujibu wa sheria.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene alisema hayo juzi wakati akizungumza na watendaji wa serikali za vijiji, kata na wadau wengine wakiwemo wakulima na wafugaji kutoka vijiji vitano vinavyopakana na Bonde la Mgongola lililopo wilayani Mvomero.
Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero na kuhudhuriwa na watendaji wa vijiji na kata za Hembeti, Sugaji, Mkindo, Dihombo na Kambala vilivyopo katika Tarafa ya Mvomero.
Simbachawene alisema wilaya za Mvomero na Kilosa zimekuwa na migogoro ya muda mrefu inayohusisha wakulima na wafugaji, ambayo kwa nyakati tofauti imesuluhishwa na viongozi mbalimbali wa wilaya, wakuu wa mikoa na mawaziri wa wizara mbalimbali, lakini bado migogoro hiyo imekuwa ikizidi kuendelea kila kukicha.
“Leo nimekuja hapa kutoa maelekezo na msimamo wa serikali hasa kwa watendaji wa vijiji, kata, wenyeviti wa vijiji na madiwani ambao wamebainika kuwa ni chanzo za kuendelea kwa migogoro hii, nataka tuambizane ukweli na kuchukua hatua stahiki kwa wale wanaojihusisha na jambo hili,” alisema Simbachawene.
Aliwaonya watendaji wa serikali za vijiji, kata, wenyeviti na madiwani kuacha mara moja kuchochea migogoro hiyo baada ya kubainika kuwa ni chanzo kikuu cha migogoro hiyo na kuwa kamwe haitawavumilia na wale watakaoleta ubishi, watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
“Kuanzia sasa watendaji wa vijiji na kata watakaobainika kuwa chanzo kikuu cha migogoro inayotokea tunawashughulikia kwa mujibu wa sheria na kuwatimua kazini...,” alisema Simbachawene.
Mbali na kundi la watendaji wa serikali, alisema kwa viongozi wa kuchaguliwa watakaobainika wanatumika kuchochea migogoro hiyo, Serikali utaratibu uliotumika kuwaingiza madarakani na ndiyo utakaotumika kuwaondoa kwenye nafasi hizo wakiwamo wenyeviti wa vijiji pamoja na madiwani.