SIMBACHAWENE: Serikali imekusanya Bilioni 19 katika mradi wa mabasi ya mwendokasi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Habari wanaJF,

Waziri George Simbachawene asema kati ya Mei hadi Disemba 2016 serikali ilifanikiwa kukusanya TZS bilioni 19 katika mabasi ya mwendokasi.

Screen-Shot-2017-01-25-at-4.46.22-PM-1.png
 
Hii ni baada ya kutoa gharama zote? Kama ndio hivyo, basi tuendeleze mradi huu na hiyo barabara ifike hadi kibamba kama Magufuli alivyosema hivi karibuni.
 
Lengo lilikuwa shilingi ngapi? Na kabla ya mwendokasi malengo yalikuwa kiasi gani na walikuwa wanakusanya kiasi gani? Na je, kufikia lini deni la World Bank litakuwa limekwisha?
 
Tusiwekeze kwenye kugawa bali kujengea wananchi uwezo wa kipato. Wakitengeneza miundo mbinu, watu watapata ajira.
Hiyo ni Vision mbayo ni lazima nchi yoyote iwe nayo lakini suala la njaa ni suala la DHARURA inatakiwa warescue hali za watu kbl ya kuanza mikakati ya kutengeneza mazingira ya ajira.
 
Hiyo ni Vision mbayo ni lazima nchi yoyote iwe nayo lakini suala la njaa ni suala la DHARURA inatakiwa warescue hali za watu kbl ya kuanza mikakati ya kutengeneza mazingira ya ajira.
Hili la njaa tunalikuza kiasi. Bei bado zipo stable. Wananchi wakijengewa uwezo watamudu maisha yao.
 
Jana walisema kuwa wanasafirisha watu 62,000 kwa siku ukipiga hesabu inaleta 40mil kwa siku hapo kabla hujatoa zile ambazo wanafunzi wanaingia nazo
 
Hayo makusanyo bila kujua matumizi yana tafsiri gani kwa Mtanzania?

Na Je, hayo ni makusanyo ya serikali au ya kampuni ya UDA ambayo jana tu ndio tumeambiwa serikali imefanikiwa kurejesha hisa zake asilimia 49 ambazo ni kama bilioni tano?

Tuambieni ukweli kuhusu sehemu ya pesa zetu kupitia mkopo wa benki ya dunia ziliongizwa kwenye ununuzi wa mabasi ya UDART, na je zimeathiri vipi share ya serikali?

Na mtuambie toka hicho kipindi cha UDA na assets zake zote kuthaminishwa kwa bilioni kumi ili iuzwe bwana Kisena amewekeza ngapi za ziada?
 
kwa mieza saba kwangu mimi sio biashara nzuri .kwa sababu mradi huu unaghara nyingi . ujenzi wa barabara zake .mabasi yenyewe na uendeshaji .ila mimi sijui kama hiyo bil 19 ni net profit au ni makusanyo ya jumla?.
 
Habari wanaJF,

Waziri George Simbachawene asema kati ya Mei hadi Disemba 2016 serikali ilifanikiwa kukusanya TZS bilioni 19 katika mabasi ya mwendokasi.

View attachment 464083
matumizi ni sh ngapi??

sisi tunataka kujua faida. nadhani hata bosi wake ndicho anachotaka, labda kama huyo bosi wake alikuwa anaongea from his own profession (chemistry) perspective!
 
Back
Top Bottom