Simbachawene juu ya gesi ndani ya Clouds fm

Simbachawene juu ya gesi ndani ya Clouds fm

mwakichi

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2011
Posts
417
Reaction score
97
Wanajamvi
Naona sarakas za gesi zimeamia Clouds fm,hapa naona Naibu wa Nishati Nhe. Simbachawene anatema povu katika mambo ambayo hayaitaji nguvu kbsa ktk kuelezea..nimemsikia akidai kujenga miundo mbinu ya umeme kutoka Mtwara mpka Dar ni gharama zaidi kuliko kuleta gesi DSM, zaid anafafanua upatikanaj wa ajira na uwezo wa gesi ktk kutumika majumban,ila waswas wangu na pale anaposema magari ambayo yanapatikana mengi DSM yatatumia gesi..huu ni uwongo,Tanzania bado sana ila hili swala la viwanda kujengwa baada ya gesi kuja pia ni siasa,kwanin viwanda visianze kujengwa kbsa ili watu wa Mtwara waweze kuelewa faida hiyo.

Serikali ya CCM ina agenda gani na gesi ya Mtwara na kwanin hao wanaochimba wasafirishe nje wakat ges ni yetu na sisi ndo waamuz,h apa anasema serikal itasave zaid ya trillion na pesa hizi kwenda ktk elim na afya,bdo serikal ya CCM inajua Watanzania ni masikin wa elimu na afya zao sasa wanataka kutumia karata ile ile miaka yote kuhadaa Watanzania.
Hili swala la Clouds kugeuka redio ya Tanzania limepitishwa na serikal gan?

Hivi kuna ugumu gani wa gesi ya Watanzania ikaanza kuwanufaisha wana mtwara kwanza ili waweze kuendelea,pale kuna bandari,ipo mpakan kbsa kuna ardhi kubwa sana..kunani na gesi ya Mtwara?

My take
CCM iangalie kwa umakin upatikanaji na ugawaj wa rasilimal ktk kuleta maendeleo tz nzima na siyo dsm pekee

Clouds fm ni sekta binafsi haina sabab ya kupiga tantalila ktk gesi otherwise na wao ni wanufaikaji
 
CCM wapeni haki yao wanaMtwara -- tangu uhuru wamekuwa waangaliaji tu wa maendeleo --- angalieni mkiwaudhi na hawa basi tena. (Mmakua, Mkakonde ikifikia hatua akikasirika aisee kazi ipo..)

Hata mimi ningekuwa mkazi na mzaliwa wa Mtwara nisingekubali - gesi muipate kwetu then processing firm's ziwe Dar why? mnakwepa gharama zipi? mlituahidi Mtwara utakuwa ukanda wa viwanda sasa anzeni na hili la gesi.

Wana-Mtwara msirudi nyuma -- uzi ule ule hakuna siasa hapa bali mdai maendeleo yenu, hii ndiyo chance yenu kunyenyua ukanda wa kusini.

Najua Gesi ikiwa processed Mtwara:
a) Mji utapanuka, viwanda vitajengwa sababu nishati ya gesi inapatikana hapo tena ya uhakika
b) Miundombinu itaboreswa -- hii ni pamoja na upanuzi wa uwanja wa ndege kwa wa kimataifa
c) Watoto wenu watapata kazi viwandani hence kukuza uchumi wa ukanda huo; na hawa hawa walioajiriwa kwenye viwanda watawasomesha wadogo zao hence kukuza kiwango cha elimu na kupunguza umaskini katika ngazi ya kaya.
d) Huduma za afya zitaboreshwa sababu mji utakuwa na wawekezaji / watalii na wafanyakazi wa viwandani kwa hiyo na nyie mtafaidikamo
e) Mtatembelewa na wageni wengi (watalii toka ughaibuni) hili litaongeza ukuaji uchumi kuanzia ngazi ya kaya na ukanda wa kusini kwa ujumla. hata sisi akina maganga ambao hatujawahi kufika ntwara basi tutakuja tu kuona production ya gasi yetu.

na mengine mengi tu - its your chance - yes never blow!!
 
Mr.Mwakichi,
Clouds fm kwa ujumla ni lazima waitetee CCM na serikali yake maana wanapewa tenda za mabilioni serikalini, mfano ni malaria no more project, studio ya Tanzania kupewa THT, na THT wanapewa tenda nyingi sana, matangazo n.k achiliambali hela wanazopewa cha juu kwa ajili ya kupaka matope CHADEMA na vyama vya upinzani kwa maslahi yao.

Mwakichi usichukulie maanani maana hawa wameweza propaganda sana sio maswala ya kitaalamu ninakama miaka mitatu sijawasikiliza hawa ila sijui leo ilikuwaje nimewasikiliza, Na huwezi amini maneno aliyosema Gerald Hando, namnukuu"kama hawataki gesi ije"yeye na Badra masoud(professional lady) watakula maharage,coka,mayai,pepsi na vinywaji vyote vyenye gesi kwa miezi sita then watatoa gesi,ni heri kuliko kulipa Bilioni 5.2 Kwa siku!

Sasa hawa ni wa kuwatilia maanani kweli au wanakoroga watu?
 
Hakuna anayekataa kwamba gas ya Mtwara ni ya watanzania wote. Kinachogomba hapa ni kwamba Wana-Mtwara lazima kwanza wafaidike na gas inayopatikana Mtwara kabla ya watanzania wengine. HOW? hii ndiyo ingekuwa challange ya serikali aidha kwa kujenga viwanda Mtwara, Kujenga viwanda vya kufua hiyo gas Mtwara, au kurudisha mrahaba wa 40% wa gas Mtwara na 60% ndiyo iingizwe kwenye fuko kuu la Taifa.

Lakini serikali kuendelea kung'ang'ania kwamba gas ya Mtwara ni watanzania wote na lazima isafirishwe kwenda DSM bila kuelezea wana Mtwara watafaidikaje na gas hiyo, mimi nafikiri Serikali is choosing a wrong side and history will judge them, The writting is already on the wall. Ni sikio la kufa .....................

Kumbuka Wana-Mtwara wanasoma na kusikia kwamba hata kabla ya gas yao hajaanza kuchimbwa tayari vigogo wa serikali ya CCM wameshaficha pesa Uswiss zitokanazo na upatikanaji wa gas hiyo.
 
Mimi nadhani watendaji wa serikali ni wagumu kujieleza nahisi most of them ni vilaza. Kwa hali ya kawaida huwezi waambia watu gesi ifike dsm ndo viwanda vijengwe. Dsm is very populated city in Tz kupunguza msongamo vyanzo mbali mbali vitoke dsm jamani tawanyeni kwa nini wasiipeleke basi hata doodma au moro?
 
Clouds fm ni redio ya wachumia tumbo na njaa kali,pia kuhusu suala hilo la gesi ni kwamba ccm ishajua wazi ya kwamba picha lishabadilika,wanatapa tapa tuh,hali ishakuwa tofauti ukanda ule
 
Hizo fedha za ujenzi wa bomba la gesi zina kazi nyingine pia. Kwa mfano uchaguzi unakuja 2015, pesa za kampeni zinatafutwa hapo, pamoja na mengine!

Sent from my GT-I9100 using Tapatalk 2
 
Wanajamvi
....nimemsikia akidai kujenga miundo mbinu ya umeme kutoka Mtwara mpka Dar ni gharama zaidi kuliko kuleta gesi DSM, ...

HIVI HUYU NAIBU WAZIRI anajua walau jiografia ya Tz? Je anajua miundombinu ya umeme iliyopo na mahali ilipo?
Aache kudamganya umma kuwa "kujenga miundo mbinu...ni gharama", kwani hajui kuwa existing National grid inaweza kutumika? Au ndio yale ya kujenga barabara ya kudumu 25yrs mwaka huu kwa gharama za walipa kodi then mwaka kesho barabara hiyohiyo inatakiwa ibadilishwe iwe ya mabasi yaendayo kwa kasi (kwa fedha nyingine tena za walipa kodi)?
 
Akina Gerald Hando na timu yake walionyesha kujipanga vyema kuita watendaji mbali mbali wa Serikali kuja kuthibitisha kuwa Jiji la DSM lina idadi kubwa ya magari, viwanda vingi n.k ili kuisaidia Serikali kutufunika blanketi. Kwanini hilo lina ubishi?

Ukweli CCM na Serikali yke kwa kutumia Clouds FM wanaouficha ni kuwa CCM na Serikali yake wananajisi raslimali za watanzania hususan Gesi Asilia kwa kuileta kwanza katika mitambo ya kuzalisha umeme wa dharurua ambayo kwa miongo miwili imekuwa ikitumika kuwakamua watanzania kupitia malipo ya "Capacity Charge" kwa zaidi ya Shilingi Milioni 152 kwa siku hata kama haizalishi na kuendeshwa kwa mafuta ya gharama kubwa sana. Ni Mtanzania gani aliridhia kuletwa kwa mitambo hii?

Kwa kuwa Prof Muhondo anadai Gesi iligundulika hapa nchini mwaka 1974, ni kwanini hadi sasa CCM na Serikali yake haijanunua mitambo yake ya kuzalisha umeme na kuifunga huko Mtwara, hata kama ni ya ghrama kubwa? Kipi kina ghrama kubwa kufunga mitambo ya kuzalisha umeme Mtwara au Kulipia mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura zaidi ya Shilingi Milioni 152 kwa siku pasipo kuzalsiha umeme kwa miaka 20?

Simbachawene anajaribu kutudanganya eti kuwa taifa linahitaji MW 900 za umeme hivyo
zinahitajika line 3 za kusafirisha umeme wa MW 400 kwa kila line ili kuleta kiasi hicho cha umeme DSM toka Mtwara na kuwa ujenzi bomba la kusafirisha gesi ni rahisi zaidi kuliko kujenga Nguzo katika line moja ya umeme kusafirisha umeme wa MW 400.

Ni kwanini hivi sasa zijengwe line zote 3 za kuleta mahitaji yote ya umeem wa taifa wa MW 900 kuja DSM kwa mara moja? Kwani taifa lilifikia mahataji hayo mara moja kisi hicho? Kwa kuwa mahataji ya taifa ni MW 900, Je haknua chanzo kingine chochote cha umeme hapa nchini ila hiyo gesi tu? Mbona kuna mitamabo ya kuzalsiha umeme imejengwa hadi Mwanza.


kwa kifupi jinamizi la uifsadi wa IPTL, RICHMOND na DOWANS linawajia kivingine?
 
Sasa hawa ni wa kuwatilia maanani kweli au wanakoroga watu?......[/QUOTE]

Huyu Badra Masoud toka ameacha uandishi wa habari pale BBC na kujiunga na Tanesco akili zake zinazidi kudumaa sijui anakorofishwa na Bwana ake jinsi anavopenda mabinti wa pembeni?:A S 11:
 
HIVI HUYU NAIBU WAZIRI anajua walau jiografia ya Tz? Je anajua miundombinu ya umeme iliyopo na mahali ilipo?
Aache kudamganya umma kuwa "kujenga miundo mbinu...ni gharama", kwani hajui kuwa existing National grid inaweza kutumika? Au ndio yale ya kujenga barabara ya kudumu 25yrs mwaka huu kwa gharama za walipa kodi then mwaka kesho barabara hiyohiyo inatakiwa ibadilishwe iwe ya mabasi yaendayo kwa kasi (kwa fedha nyingine tena za walipa kodi)?......

Huyu Simbachawene na Kapuya si ndio wamiliki wa Band ya Akudo Impact wana akili kama za Rapa wao Kanal Tope rapa ya Akudo
 
vijana ndio nguvu kazi ya taifa hili,vijana ndio wanalia shida na maisha magumu na vijana hao hao ndio wassikilizaji wakubwa wa clouds, kataeni hii redio ikose matangazo nyie munaijali yenyewe haiwajali, clouds ni msemaji wa ccm, vijana amkeni sikilizeni redio za maana.
 
ninyi watu mnaomponda huyu waziri na kushabikia bomba lisijengwe, mlikuwa wapi kabla? mbona mmesubiri hadi mkataba umeingiwa na pesa zimetolewa ndo mnapiga yowe?...akili zenu ni ndogo sana halafu ni kama wadudu wanawanyevuanyevua vile, mnawashwa? tuje tuwakuna huko....?
 
ninyi watu mnaomponda huyu waziri na kushabikia bomba lisijengwe, mlikuwa wapi kabla? mbona mmesubiri hadi mkataba umeingiwa na pesa zimetolewa ndo mnapiga yowe?...akili zenu ni ndogo sana halafu ni kama wadudu wanawanyevuanyevua vile, mnawashwa? tuje tuwakuna huko....?
hii ndiyo athari ya mikataba inayosainiwa usiku wa manane!!! kwa faida yako tu ni kwamba katika any project user envolvement katika kila phase ni muhimu kuliko huo mkataba wenyewe!! hawa wananchi kama walishirikiswa wao si majua leo waingie barabarani kupinga mradi huu; hapa kuna tatizo tayari.
 
hii ndiyo athari ya mikataba inayosainiwa usiku wa manane!!! kwa faida yako tu ni kwamba katika any project user envolvement katika kila phase ni muhimu kuliko huo mkataba wenyewe!! hawa wananchi kama walishirikiswa wao si majua leo waingie barabarani kupinga mradi huu; hapa kuna tatizo tayari.
unamaana gani kuwa wananchi washirikishwe, na ni wananchi wepi? kwani rasilimali ni za watu gani tu? unataka wapite mtaa kwa mtaa wakiwashirikisha wananchi au wawakilishi wa wanaanchi either wabunge au viongozi tuliowapa hatamu kutufanyia mambo yetu, rasilimali zile ni zetu sota tz nzima na kama kushirikishwa tungekuwa wetu.
 
"Ukiwa karibu na waridi, unastahili kunukia" Dr John Samuel Malecela a k a Cigwiyemisi(kilichoanguka mchana)
 
Ninaomba Serikali tishe huu mradi wa geri then tuwaachie wainywe hiyo gesi.Siasa kila kona mpaka vijiweni watu hata kazi hawafanyi.Wanasiasa wanawatumia vibaya wananchi.WANANCHI SIKU HIZI WAMEKUWA VIPEPERUSHI VYA WANASIASA HASA VIJANA.
 
Kama Nchemba anasema Chadema itakufa kwa kuzeeka kwa Dr. Slaa, basi CCM itakufa kwa kulazimisha gas ya Mtwara kwenda Dar. Mark my words.
 
unamaana gani kuwa wananchi washirikishwe, na ni wananchi wepi? kwani rasilimali ni za watu gani tu? unataka wapite mtaa kwa mtaa wakiwashirikisha wananchi au wawakilishi wa wanaanchi either wabunge au viongozi tuliowapa hatamu kutufanyia mambo yetu, rasilimali zile ni zetu sota tz nzima na kama kushirikishwa tungekuwa wetu.

WABUNGE WETU HAWAJASHIRIKISHWA KASORO MBUNGE (Waziri na Naibu wake)WALIO KWENYE WIZARA HUSIKA TU. NDIO MAANA MBUNGE MNYIKA ALIIDAI HIYO CONTRACT ILETWE BUNGENI.
Sasa kama bunge halijashirikishwa unatarajia nini? Wananchi watakuwa wameshirikishwa?
 
MaCCM bana badala liwe ofisini linaende redio ya uchochoroni asubh hii!! Hakuna msemaaji wa hiyo wwizara? Analipwa ka kazi gan? MaCCM mmechoka...
 
Back
Top Bottom