Simba watakosea Kumpa Timu Dewji..

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
35,044
41,854
Simba watakua wanajirudisha nyuma miaka kadhaa kama watakubali kuruhusu Mohamed Dewji Achukue contol ya timu kwa asilimia kubwa.

Simba wamekua driven na kile kinachoonekana kama success kwa Yanga ambacho binafsi naona kama vile sio success bali ni safari kuelekea kuzimu kwa timu ya Yanga.

Simba wanaona Kwa yanga kushinda Ligi kuu na kushiriki nane bora ya Champions league kama mafanikio ya kuifanya Simba kutetereka na kuuza Asili yake.

Kinachoendelea Yanga ni kama furaha ya povu ambalo litapasuka muda wowote ikitokea mmfadhili wa sasa akaudhiwa.

Imeshawai tokea mara kadhaa miaka ya nyuma kuona wafadhili wa hizi timu wakizidump na kuleta taharuki kwa timu husika.

Vile vile sio mara ya kwanza kwa Dewji kua mfadhili wa Simba, alishawanfa hivyo na akabwaga manyanga yake.

Dewji huyu huyu baada ya kuudhiwa na Simba alianzisha timu yake ya Africa Lyon ambayo , kwa sasa hali yake haifahamiki kama imekufa au bado inaendelea kushiriki ligi mbali mbali.

Mpaka sasa sijasikia convincing argument toka kwa Dewji huyu wa sasa kujitofautisha na Dewji wa Zamani ili wana Simba wampe timu.

Waungwana wanasema " eperience is the best teacher" Hivyo nawausia wana Simba wenzangu kuwa makini na maamuzi yao, maana kuna dalili za kuja jutia huko mbele.

I stand to be corrected.
 
Kuna kitu hujakielewa vizuri. Tatizo la Simba liko kwenye suala la timu iendeshweje, kampuni au hivi hivi na wanachama?
Watu wengi wanataka timu ijiendeshe kwa mfumo wa kampuni ambapo hisa zitanunuliwa na yeyote mwenye kutimiza masharti na kisha mwenye nyingi ndie atakayekuwa na sauti ya mwisho. Hapa anaweza akawa ni Dewji au mtu yeyote mwenye mpunga.

Pili umetolea mfumo wa Yanga, huko umepotea kabisa kwa sababu Yanga haina mfumo kama huu wanaotaka kuanzisha Simba. Yanga wana kiongozi mwenye fedha nyingi ambae hana hisa wala si mmiliki ila anatoa fedha yake mfukoni kusaidia mambo yaende. Ni hisani tu anafanya, akiondoka au siku akishindwa uongozi ndio itakuwa mwisho wa kula fedha zake.

Mfumo wa Simba kama watafanikiwa ndio mfumo wa kisasa na timu nyingi duniani zinautumia, na ikitokea mtu amebadili mawazo anauza hisa kwa mtu mwingine
 
Nakuunga mkono mkuu mana kuna matajiri wengine wanajiona wao ndo kila kitu na kuitelekeza timu kwao ni jambo la kawaida angekuwa anauchungu na soka la bongo angeiendeleza African lyon ingekuwa mbali au kuwa na level inayofanana na Azam kama alivyofanya mwenzie Bakhresa sio kuwafitinisha watu uonekane unakubalika
 
wakati rage akiwaita wanachama wa simba mbumbumbu wengi tuliona kawatukana ila ukweli aliwaambia ingawa hayupo.Wanachama walipaswa kuwaoji wakina Aveva kwanini wananshindwa kuipa timu mafanikio, kama tatizo ni pesa waelez vitega uchumi likiwemo jengo la msimbazi na mauzo ya jezi yanaenda wapi.Wanachama wengi wanamshabikia dewji kununua simba hisa 51% kwa bilioni 20 wakati hakuna chombo chochote kilichokaa na kuthibitisha thamani halisi ya simba ikiwa pamoja na fanbase yake.Wameshindwa kumuuliza dewji nini kilimshindwa afrika lyon mpaka akaiuza na je simba ikimshinda hatachukua maamuzi hayohayo.Dewji anatumia umbumbu wa wananchama wa simba kutekeleza malengo yake kama kweli anaipenda simba na yeye ni mwanachama mbona kikao cha jana hakuhudhuria?wanachama wameshindwa hata kuhoji taarifa ya fedha ingawa ilikuwa na mapungufu mengi kisa kudai timu auziwe dewji.wanabaki kulaumu wazee wa simba wakati hawajui wao ndio walianzisha hiyo timu na mpaka leo bado ipo.
 
wakati rage akiwaita wanachama wa simba mbumbumbu wengi tuliona kawatukana ila ukweli aliwaambia ingawa hayupo.Wanachama walipaswa kuwaoji wakina Aveva kwanini wananshindwa kuipa timu mafanikio, kama tatizo ni pesa waelez vitega uchumi likiwemo jengo la msimbazi na mauzo ya jezi yanaenda wapi.Wanachama wengi wanamshabikia dewji kununua simba hisa 51% kwa bilioni 20 wakati hakuna chombo chochote kilichokaa na kuthibitisha thamani halisi ya simba ikiwa pamoja na fanbase yake.Wameshindwa kumuuliza dewji nini kilimshindwa afrika lyon mpaka akaiuza na je simba ikimshinda hatachukua maamuzi hayohayo.Dewji anatumia umbumbu wa wananchama wa simba kutekeleza malengo yake kama ka kweli anaipenda simba na yeye ni mwanachama mbona kikao cha jana hakuhudhuria?wanachama wameshindwa hata kuhoji taarifa ya fedha ingawa ilikuwa na mapungufu mengi kisa kudai timu auziwe dewji.wanabaki kulaumu wazee wa simba wakati hawajui wao ndio walianzisha hiyo timu na mpaka leo bado ipo.
Mkuu mambo mengi uliyoyazungumza ni ya kujenga ufahamu wa walio na nafasi ya kuleta mabadiliko katika timu. Tatizo la kushabikia mambo lipo kila mahali hata katika mambo ambayo hayahitaji ushabiki. Matawi nayo yanatumika na wahusika kutimiza malengo yao.
 
Hio bil 20 hata GOODWILL ya simba pekee haitoshi, sembuse total market value ya Simba, huo ni mzaha mtupu
 
wakati rage akiwaita wanachama wa simba mbumbumbu wengi tuliona kawatukana ila ukweli aliwaambia ingawa hayupo.Wanachama walipaswa kuwaoji wakina Aveva kwanini wananshindwa kuipa timu mafanikio, kama tatizo ni pesa waelez vitega uchumi likiwemo jengo la msimbazi na mauzo ya jezi yanaenda wapi.Wanachama wengi wanamshabikia dewji kununua simba hisa 51% kwa bilioni 20 wakati hakuna chombo chochote kilichokaa na kuthibitisha thamani halisi ya simba ikiwa pamoja na fanbase yake.Wameshindwa kumuuliza dewji nini kilimshindwa afrika lyon mpaka akaiuza na je simba ikimshinda hatachukua maamuzi hayohayo.Dewji anatumia umbumbu wa wananchama wa simba kutekeleza malengo yake kama kweli anaipenda simba na yeye ni mwanachama mbona kikao cha jana hakuhudhuria?wanachama wameshindwa hata kuhoji taarifa ya fedha ingawa ilikuwa na mapungufu mengi kisa kudai timu auziwe dewji.wanabaki kulaumu wazee wa simba wakati hawajui wao ndio walianzisha hiyo timu na mpaka leo bado ipo.
Mkuu rodrick alexander, hapo kwenye red umeandika maneno ya maana sana.
Kama kumbukumbu zangu ziko sawa ni kwamba Mzee Bakhresa alikuwa shabiki mkubwa wa Simba lakini baada ya kuona usumbufu wa 'wenye timu' akaachana nayo kiukweli na hakuendelea na mchezo wa kufitinisha hawa 'mbumbumbu'. Nasikia hata wazo la kuanzisha timu hakuwa nalo bali ni wafanyakazi ndio walianzisha tu kama 'jogging club' na walivyokwenda mtaani wakashinda 'kombe la mbuzi' ndio akahamasika na kuanza kulipa hilo wazo la timu nguvu hadi hapa walipofikia. Huenda Azam ikawa na wapenzi wachache lakini wanaojitambua na ukiangalia idadi yao na muda ambao imekuwepo ni wazi miaka 80 ijayo itakuwa mbali sana.Wenye timu wanaamini timu inavyoendeshwa ni sawa na imeendeshwa hivi miaka 80, maana wao wanapata mlo wao na hakuna mchezaji anayelazimishwa kusajiliwa.
Story mingi lakini hoja yangu hapa ni kuwa Bakhresa huenda ni mpenzi wa soka wa ukweli na MO ni shabiki tu anayeangalia maslahi yake. Japo hii inaweza kuwa nafasi nzuri kwa wale wanaooamini Simba na Yanga kuwa kikwazo cha maendeleo ya mpira hapa tz kwa maana anaweza kuwasaidia 'kuiua' mojawapo.
 
Kama ataibadilisha jina basi wanachama hao watakuwa wamekosea
 
Hio bil 20 hata GOODWILL ya simba pekee haitoshi, sembuse total market value ya Simba, huo ni mzaha mtupu

Kabla ya kujua thamani halisi ya Simba, cha kwanza ni kufanya uamuzi wa timu ijiendeshe kama kampuni au kama ilivyo sasa hivi. Ikiamuliwa iwe kampuni ndio sasa valuation process ifanyike (japo nakumbuka ni kama Aveva alishawahi kusema wameteua kamati ya kufanya kazi hiyo au inayofanana na hiyo).

Baada ya hapo ndio hisa ziuzwe ambapo MO au mtu yeyote hata Aveva na wenzie wanaweza kununua hisa. Mwenye hisa nyingi ndio atakuwa mwenye sauti ya mwisho. Nadhani watu wangejikita zaidi kwenye kujadili SIMBA IENDESHWE VIPI kuliko kumjadili MO au thamani halisi ya klabu.
 
Kuna kitu hujakielewa vizuri. Tatizo la Simba liko kwenye suala la timu iendeshweje, kampuni au hivi hivi na wanachama?
Watu wengi wanataka timu ijiendeshe kwa mfumo wa kampuni ambapo hisa zitanunuliwa na yeyote mwenye kutimiza masharti na kisha mwenye nyingi ndie atakayekuwa na sauti ya mwisho. Hapa anaweza akawa ni Dewji au mtu yeyote mwenye mpunga.

Pili umetolea mfumo wa Yanga, huko umepotea kabisa kwa sababu Yanga haina mfumo kama huu wanaotaka kuanzisha Simba. Yanga wana kiongozi mwenye fedha nyingi ambae hana hisa wala si mmiliki ila anatoa fedha yake mfukoni kusaidia mambo yaende. Ni hisani tu anafanya, akiondoka au siku akishindwa uongozi ndio itakuwa mwisho wa kula fedha zake.

Mfumo wa Simba kama watafanikiwa ndio mfumo wa kisasa na timu nyingi duniani zinautumia, na ikitokea mtu amebadili mawazo anauza hisa kwa mtu mwingine

Mkuu, timu zetu hizi ambazo wanachama hulipiwa kadi karibia na uchaguzi watanunua hisa kwa hela zipi?

Rage asipuuzwe kwenye hili. Kuna njia nyingi za kumiliki Club kubwa duniani. Tujiulize Bayern Munich na Barcelona zinamilikiwa kwa njia gani. Hata huo mfumo unahitaji muda kuwaelewesha wanachama ili waweze kuchangia sio kusubiri kulipiwa kadi za uanachama.
 
Watu wanawaza kutokufanikiwa tu..hivi Simba iendelee kuwa ombaomba ndio watu wafurahi?mfumo lazima ubadilike...zama za uendeshaji timu kwa staili hii ya mchango wa 1200 kwa mwezi hakuna mpira utakaochezwa labda ndondo
 
Mbadiliko kwa utaratibu sio kwa usanii..
Sioni kama kuna shida yoyote kwani hakuna chochote anachokabidhiwa mtu bila kuwepo terms and condition za kisheria.Hivi vitu vitaenda kisheria na makubaliano ya kisheria lazima yawepo.

Hivi kwanini sisi ni waoga kwa mambo ambayo hayana msingi.

Kwa mantiki hii na kwa jambo dogo hivi hatuwezi kuendelea kwa lolote.

Kuthubutu kwetu ni kitu kisichowezekana,na tutashindwa kwa mengi kwa mtindo huu.
 
Back
Top Bottom