Simba wafanye nini kuchukua kombe ligi Kuu Tanzania bara?

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
Natumai mu wazima,
Ni muda sasa mrefu kama misimu minne ambapo timu ya Simba SC haijafanikiwa kuutia ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara mkononi japo kwa msimu huu wamefanikiwa angalau kupata kombe la Ligi.

Lakini nafikiri bado ubingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara una msisimko zaidi na kila timu inaunyapianyapia.

Jambo la kwanza kujiuliza, Simba kama club inakosea wapi? Na wajipange vipi kuchukua ubingwa huu wenye msisimko zaidi?

Mimi kwa upande wangu naanza na kuwashauri wafanye usajili wenye tija..wamtoe Mavugo pale mbele naona wanachezesha jina kwani anapoteza nafasi nyingi za wazi, kiufupi anakosa umakini.

Pili waache uswahili, walipe wachezaji kwa wakati jambo litakalowaongezea morali.

Karibuni
 
Waende fifa na hata pia CAS wakakate rufaa kama wanaamin haki yao imeminywa bongo kinyume na hivyo asahau kabisa ubingwa msimu ujao kwani azam atakuwa moto hatar pamoja na yanga
 
Uongozi uache utoto hilo la kwanza
na la pili; wamuachie kocha kwenye kuchagua wachezaji wa kusajili... (Tatizo ambalo timu zote kubwa linalo)
 
Kombe tutachukua tukitaka, mfano mdogo waweza ona ubora wetu msimu huu uliopita umekua imara kuliko 2015-2016 pia tumepata fedha nyingi kushinda hata waliobeba kombe
 
Simba imekosa ubingwa kwa sababu hawana wale wachezaji wanaoweza kujitoa kwa extra mile...yaani wale wachezaji wa kupiga Jihad

Hili ni mojawapo..Ila pia kupungua spidi ya kichuya awamu ya pili ligi kuu..kunawezakuwa pameigharimu timu
 
Tatizo sio Simba kukosa ubingwa pekee, tatizo ni kuwa na ligi ambayo bingwa ameshuka kiwango kama Yanga.
 
Kombe tutachukua tukitaka, mfano mdogo waweza ona ubora wetu msimu huu uliopita umekua imara kuliko 2015-2016 pia tumepata fedha nyingi kushinda hata waliobeba kombe
Thamani ya kubeba Ubingwa wa Ligi haufanyiwi hesabu za namna hiyo!

Kitendo cha Yanga kubeba ndoo tu kumefanya kuwe na tofauti Kwenye mikataba ya sportpesa baina ya Yanga na Simba!

Hilo gape tu linaleta tofauti zaidi ya unayoweza kuwaza.

Hapo bado ule mchongo wa CAF Kwenye ushiriki wa competitive stages kwenye CAF Champions League.
 
tapatalk_1484802133505.jpeg
 
Back
Top Bottom