SIMBA vs YANGA: Lowassa kuungana na mashabiki kuhudhuria mechi uwanja wa Taifa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kesho ataungana na mashabiki watakaohudhuria mechi ya Simba na Yanga uwanja wa taifa jijini Dar es salaam

Lowassa amesema kinachomsukuma zaidi kwenda uwanjani ni kuungana na wadau wa soka nchini na kujionea ambavyo ligi ya Tanzania inavyokuwa na msisimko kama ilivyo kwa ligi za nje

"Kesho nakwenda uwanjani, usitake kujua mimi ni mshabiki wa timu gani, subiri utaniona uwanjani", amesema Lowassa

"Nasikitika ninapoona watu tunazipenda sana timu za nje. Yale mahaba ya zamani kwa timu zetu yako wapi? michezo hususan mpira ni eneo pana la ajira kwa vijana wetu",alisema Lowassa ambaye alikuwa mchezaji wa mpira wa kikapu hapo zamani.

Chanzo: Mwananchi
 
RAIS WA MIOYO YETU tafadhar usije.maana sikiizi ni mwendo wakutaftiana kesi maana kesho yanga anakufa c chini ya 2..theni mashabiki wao watang'oa viti lawama zote utatupiwa wewe.
 
3ae78025aba02d3c3071b6e29f85b244.jpg
Itajulikana hapo kwenye mtanange karibu, usisahau kuvaa jezi ya timu
 
Back
Top Bottom