Simba Vs Ruvu Shooting: Tutegemee soka na matokeo ya aina gani?

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,701
45,034
Mabingwa wa Nchi, Simba Sports Club "Mnyama" leo atakuwa uwanja wa nyumbani wa Uhuru kujiuliza dhidi ya Ruvu Shooting wa Mlandizi, Pwani.

Mechi iliyopita mabingwa hao wa Nchi ilikung'utwa bao moja kwa nunge dhidi ya wajelajela Tanzania Prisons! Pia ni mechi ambayo Simba ama Lunyasi iliwakosa wachezaji wake muhimu kama Kagere, Mugalu, Bocco na Chama!

Je, leo Simba wakiwa uwanja wa nyumbani tutarajie kuona soka la aina gani? Na vipi kuhusu matokeo? Je wataamka kutoka kwenye kichapo cha Prisons au wataendelea kulala hasa wakati huu watani zao Yanga nyita ikiendelea kung'aa!

Tupia utabiri wako.
 
Simba hawawezi kukubali kupoteza Point nyumbani Kwa timu Kama Ruvu,hasa wakizingatia wametoka kupoteza mechi iliyopita.
Ruvu shooting wanaongozwa na Mkwasa,ambaye kivyovyote vile akipata point mbele ya Simba atakuwa na furaha mara mbili(hili halihitaji maswali mengi).lolote linaweza kutokea,ingawa natamani na leo wapigwe.
 
Hahaha sawa
 
ebu niwekee hapa nione kapangaje kikosi cha leo

Hiki hapa kikosi
Adjustments.JPG
 
Back
Top Bottom