Simba ukweli mlifungwa tu

fasiliteta

JF-Expert Member
Jul 2, 2014
2,284
3,940
Niwakumbushe tu ndugu zangu SIMBA,mlifungwa 2-1 na KAGERA huko KAITABA.Point za KAGERA ni halali na walizitolea jasho,acheni janja janja utafikiri mlishinda mkapokwa point.

Ushauri wangu,chezeni mpira mwende mbeleee, huyo manara angeongezewa miaka 2 mbele ataacha ubaguzi wake wa kipuuzi puuzi, mwaka jana mwenzake kaongea vitu vya kawaida tu,akamchongea kwa TFF hiyo hiyo,na ikawa halali ila yeye leo ndo anaona ukabila.
Mpelekeni hata QT huyo mzeee akapanguse walau hilo vumbi la ujinga
 
Simba ni wakati sasa wa kuondoa hao wapiga dili kina manara,wanawapeleka chaka sanaaaa
 
Hakuna kitu kibaya kama ushindi wa mezani ila hapa hoja iwe je sheria inasemaje mtu kuwa na card 3 na je ni kweli alikuwa na card 3? Baada ya hapa haki ichukue mkondo wake. Na kama tunadhani card 3 ni sheria mbovu basi vikao halali vifanye kazi kuzifuta ijulikane tu card sio issue.
 
kadi3 za kujitungia,ukweli simba walilambishwa shubiri tu,aliyewatonya kawaingiza choo cha kike,either hakupiga mahesabu vizur
 
Ndio maana nimesema kama card 3 sio kweli basi simba hawana haki. Mimi sijasema simba wapewe ila kama card ni kweli sheria zipo. Haya mambo ya hovyo ndio maana tunaambulia kupigwa tu 3 mara 4 yaani hovyo tu.
 
Thimba thimba thimba! Litimu linalosaka points mezani..looh aibu yenu hiyo..kufungwa mmefungwa points mtaka mpewe nyinyie loooh
 
Hakuna kitu kibaya kama ushindi wa mezani ila hapa hoja iwe je sheria inasemaje mtu kuwa na card 3 na je ni kweli alikuwa na card 3? Baada ya hapa haki ichukue mkondo wake. Na kama tunadhani card 3 ni sheria mbovu basi vikao halali vifanye kazi kuzifuta ijulikane tu card sio issue.
Kama simba angebaki na point tatau maana yake ni kwa sababu kanuni zilizngatiwa ata anavyopokonywa point tatu ni hizo hizo kanuni zinezingatiwa pia maana kama ushindi wa walopewa na kamati ya SAA 72 ni wa kikanuni na ata haki waloipata kagera ni ya kikanuni.. Sasa turudia kwenye sheria ambapo inaonekana ni yenye mapungufu hasa unapojiulza je, unapochelewa kukata rufaa na ushaid unaonesha kuna jambo limekiukwa haki yako unaipataje?
 
Tuchukulie kadi tatu anazo na kanuni zinaelekeza kuwa lazima:-

1. Uandike barua ndani ya 72hrs kwa barua rasmi ukionesha hoja zako.
2. Uambatanishe na ada ya malalamiko yako sh. 300,000/-

Swali, je walifuata kanuni hizo? Simba
 
Mimi nakubaliana na wewe ila kana kanuni ziko sasa rufaa ya nini? Kama kanuni ziko sheria ichukue nafasi yake suala la rufaa kama unapinga huyo kanuni au hukuridhika na maamuzi. Kanuni kwanza rufaa baadae
 
Kama simba angebaki na point tatau maana yake ni kwa sababu kanuni zilizngatiwa ata anavyopokonywa point tatu ni hizo hizo kanuni zinezingatiwa pia maana kama ushindi wa walopewa na kamati ya SAA 72 ni wa kikanuni na ata haki waloipata kagera ni ya kikanuni.. Sasa turudia kwenye sheria ambapo inaonekana ni yenye mapungufu hasa unapojiulza je, unapochelewa kukata rufaa na ushaid unaonesha kuna jambo limekiukwa haki yako unaipataje?
Hapo ndio utata, kanuni zipo wazi rufaa ya masaa 72 ya nini? Hapo suala je mchezaji alikuwa na card 3? Kama yes simba anapewa point kama sio basi. Ikiwa ni yes hapo kagera ndio wa kukata rufaa kama hawaamini ana card 3. Sasa jana unamsikia Mkwasa anasema sheria zibadilishwe ok lakini kubadili sheria karibia league inaisha
 
Mimi nakubaliana na wewe ila kana kanuni ziko sasa rufaa ya nini? Kama kanuni ziko sheria ichukue nafasi yake suala la rufaa kama unapinga huyo kanuni au hukuridhika na maamuzi. Kanuni kwanza rufaa baadae

Kama sheria zitatumika Mtibwa na Majimaji nao wapewe point maana walicheza na Kagera kabla kucheza na Simba na wote walifungwa
 
Simba buana! Hata kuandika hawajui...
 
Sasa ndugu yangu mimi sisemi simba tu ni team yoyote imevunja kanuni adhabu ni sawa tu kama huyo mchezaji alicheza mechi hizo na majimaji na hakutakiwa kucheza kanuni zifwate tatizo hapa team ikivunja kanuni basi kama hakuna rufaa inakuwa halali? Narudia tena kanuni haisubiri rufaa
 
Simba buana! Hata kuandika hawajui...
Tunarudi kulekule usimba na Yanga ndio maana hatufiki kokote tunaishia vichapo tu. Sasa kwa taarifa yako mimi mipira ya bongo hata hainiumizi kichwa hapa ni sheria za sika lazima ziheshimiwe. Halafu ndugu yangu mtu msomi hata akiona mtu katype error anaelewa tu huyu mtu ana maanisha kitu gani.
 
Simba buana! Hata kuandika hawajui...
Huwa sishangilii ubingwa wa Yanga wa Simba maana najuwa mipango mingi tu ni kama ile mechi ya simba na mbao ni wazi yule kipa kauza game sasa unategemea mimi nishangilie wakati na mashaka na uwezo wao. Mimi naamini yes ile mechi kuna mchezo.
 
Mimi nakubaliana na wewe ila kana kanuni ziko sasa rufaa ya nini? Kama kanuni ziko sheria ichukue nafasi yake suala la rufaa kama unapinga huyo kanuni au hukuridhika na maamuzi. Kanuni kwanza rufaa baadae
Kipi kuliwafanya mkate rufaa kwanza kabla ya kuiacha TFF ushughulie na kanuni kwenye hilo suala.?
 
Hakuna kitu kibaya kama ushindi wa mezani ila hapa hoja iwe je sheria inasemaje mtu kuwa na card 3 na je ni kweli alikuwa na card 3? Baada ya hapa haki ichukue mkondo wake. Na kama tunadhani card 3 ni sheria mbovu basi vikao halali vifanye kazi kuzifuta ijulikane tu card sio issue.
Hapo kwenye sheria, Je taratibu za kukata rufaa hiyo ya kadi 3 zilifuatwa sawa sawa?
 
Back
Top Bottom