Simba ubingwa wa point za rushwa haunogi chezeni mpira

Mjasiria Akili

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
823
371
20acd89a36cb40c1167c92bbb3f809c1.jpg


Simba wamemkatia rufaa mchezaji muhamed fakhi wakidai alicheza akiwa na kadi tatu za njano baada ya kupigwa miwa miwili kule kagera hivyo wanataka wapewe point 3.

Mechi imechezwa jumapili lkn wakatiwa rufaa wamejua wamekatiwa rufaa alhamisi tena kwa siri kuvuja sbb simba wakishirikiana kamati ya saa 72 ambayo imejaza watu wa simba na kila wakutanapo kufanya maamuzi yanayoihusu simba huitana wenyewe kwa kisingizio akidi imetimia na kila kunapokua na mahudhurio ya watu ambao sio simba mwenyekiti huahirisha kutoa maamuzi hata kama ukweli umebainika na wataendelea kupiga kalenda mpaka siku watakayofanikiwa kukutana watu wa simba pekee.

Kwa mujibu wa kocha wa kagera anakataa fakhi hana kadi tatu, mratibu wa kagera anakataa mchezaji mwenyewe anakataa na kuanisha mechi alizoadhibiwa kwa kadi za njano.
Sarakasi nyingine mechi simba wanayosema alipata kadi haikuonyeshwa hivyo mashahidi pekee ni maafisa walioisimamia wakati huo huo refa aliochezesha hiyo mechi ndio aliochezesha mechi simba wanayodai point.

Kubwa kuliko eti maamuzi yameshindwa kufanyika baada ya kuwahoji maafisa watatu waliosimamia hiyo mechi na kutofautiana hivyo wanataka kupata majibu ya afisa wa 4 ambae ni kamishina swali hawa watatu walipatijanaje huyu mmoja ashindwe kupatikana?
Hapa ndio rushwa inapoanzia huyu kamishina anaetakiwa ndio awe shahidi wa mwisho kupenyezewa mlungula tu.

Ajabu lingine kamati wanatuambia hakuna ripoti zozote wanazopeleka bodi ya ligi baada ya mechi? Zile ripoti wanazosemaga zinawasilishwa bodi baada ya mechi ni zipi kama zipo kwa nini zisitumike?

Rushwa nyingine anatoa malinzi kwa simba sbb simba ndio waliomuweka malinzi tff na bahati mbaya anamaliza muda bila simba kuwa bingwa huku akikabiliwa na uchaguzi, ili arudi tena tff lazima awape simba rushwa ya ubingwa sbb 80% kama si 90% ya wenyeviti wa mikoa ni simba zaidi ya 60% ya viongozi wa vilabu vingine vya vpl ni simba hivyo hakuna namna lazima awalambe miguu kwa rushwa ya ubingwa.

Kama mkijinadi kwa mbwembwe nyie mabingwa wa kutandaza soka basi chukueni ubingwa kwa kutandaza soka sio rushwa

Mfurukutwa wa soka......
 
Ukichaa sio lazima uvue nguo Malinzi si alikua mwenyekiti wenu Yanga iweje Leo aibebe Simba
kumbuka kuwa hata Tambwe alikuwa mchezaji wa simba.. Ila amewachomeka mara nyingi kuliko mchezaji Yeyote Yule wa Yanga SC hivi sasa.

Soma hapo juu uone deni analo daiwa na wale waliomuweka madarakani...
 
kumbuka kuwa hata Tambwe alikuwa mchezaji wa simba.. Ila amewachomeka mara nyingi kuliko mchezaji Yeyote Yule wa Yanga SC hivi sasa.

Soma hapo juu uone deni analo daiwa na wale waliomuweka madarakani...
Kama vile kichuya alivowakojolea
 
Malinzi anajiandaa kuwapa SIMBA Ubingwa wa mezani.... Baada ya kuona uwanjani hawataweza...
Malinzi ndy kikwazo namba moja kwenye ubingwa wa simba....ila wana simba tunasema MBELE...NYUMA kote ni KUGEGEDWA tu..
 
Back
Top Bottom