Simba tuikumbuke na kuienzi siku kama ya leo...

Simba tuikumbuke na kuienzi siku kama ya leo...

Gang Chomba

Platinum Member
Joined
Feb 29, 2008
Posts
20,734
Reaction score
4,871
Tujikumbushe kidogo.....
Tarehe kama ya leo 13 novemba 1991 katika uwanja wa taifa timu ya dar yanga africans waliingia uwanjani na basi la sharuksy, lililokuwa linamilikiwa na mfadhilli wao wa kipindi hicho marehemu abasi gulamali.
Timu ya simba ya dar iliweka mpira kwapani wakati wa mapumziko na kutokomea kusikojulikana,kuweka mpira kwapani kulitokana na vipigo mfululizo vya august 31, octobar 9, lakini ilitanguliwa na kipigo cha said sued "scud" cha mei 18...
"Yanga daima mbele nyuma mwiko"
 
kuna Gazeti likaandika Lunyasi akimbia Gesti na kusahau Gagulo...
Heh heh heh heh heh
 
mkuu mpaka wanatokomea matokeo yalikuwa ngapi ngapi?
 
kumbe JF napo wapo akina Mbwiga Mbwiguke aya mzee tukumbushe ya zamani. Mi nakumbuka kombe la tusker YANGA WALIVYOTESWA NA MARK SIRENGO, SHAMBA LA BIBI
 
Mbona huongelei habari ya okwi kumstaafisha nsajigwa FUSO?
Acha kuwa biased kiasi hicho
 
nakumbuka watangazaji wetu walikuwa ni Charles Hillary na Omary Jongo...
Wakati Msimamizi wa Matangazo alikuwa Nadhiri Mayoka...
Na tuliporudishwa Studio kwa ajili ya matangazo mengine tulipokelewa na Eda Sanga...

Je unakumbuka nani alikuwa fundi Mitambo?
 
nakumbuka watangazaji wetu walikuwa ni charles hillary na omary jongo...
Wakati msimamizi wa matangazo alikuwa nadhiri mayoka...
Na tuliporudishwa studio kwa ajili ya matangazo mengine tulipokelewa na eda sanga...

Je unakumbuka nani alikuwa fundi mitambo?
ilikuwa ngapi ngapi wakati wanaweka mpira kwapani??
 
nakumbuka watangazaji wetu walikuwa ni Charles Hillary na Omary Jongo...
Wakati Msimamizi wa Matangazo alikuwa Nadhiri Mayoka...
Na tuliporudishwa Studio kwa ajili ya matangazo mengine tulipokelewa na Eda Sanga...

Je unakumbuka nani alikuwa fundi Mitambo?

Nakumbuka ila nilikuwa mdogo sana std 1 .. Neno la kutia mpira kwapani lilinitatiza sana; Usiku nilimuuliza baba kutia mpira kwapani ni nini? Lakini tayari nilikuwa na mapenzi na Simba..
 
Mzee kwa kumbukumbu uko juu! Mi nakumbuka wazee wa yanga walivyovua vile vibarakhashia kwa pamoja mbele ya waandishi wa habari!!kumsusia Nchunga. Loo kilichofuatia hapo ni kumbukumbu isiyosahaulika!!Yule kijana wenu anayelialia alilia siku hiyo machozi yakamkauka masikini!!!Nikumbushe mwaka na mwezi basi!!!
 
SIMBA: Iddi Pazi, Raphael Paul, Azizi Nyoni, Method Mogella, Frank Kassanga 'Bwalya', Iddi Selemani, Itutu Kigi/Jamhuri Kihwelu, Khalfan Ngassa, Bakari Iddi/Issa Kihange, Hamisi Gaga, Zamoyoni Mogella/Ayoub Mzee. Kocha: Hassan Affif. KIKOSI CHA YANGA SIKUKUMBUKI,ILA REFA ALIKUWA TAJI BAKARI WA DODOMA
 
Tujikumbushe kidogo.....
Tarehe kama ya leo 13 novemba 1991 katika uwanja wa taifa timu ya dar yanga africans waliingia uwanjani na basi la sharuksy, lililokuwa linamilikiwa na mfadhilli wao wa kipindi hicho marehemu abasi gulamali.
Timu ya simba ya dar iliweka mpira kwapani wakati wa mapumziko na kutokomea kusikojulikana,kuweka mpira kwapani kulitokana na vipigo mfululizo vya august 31, octobar 9, lakini ilitanguliwa na kipigo cha said sued "scud" cha mei 18...
"Yanga daima mbele nyuma mwiko"

kwa mujibu wa kumbukumbu zangu game ambayo simba waliweka mpira kwapani ilikuwa ni August 31,1991 SIKU YA JUMAMOSI!! GOLI PEKEE LA MAPEMA LILIFUNGWA NA SUED SAID SCUD, HIVYO HALF TIME JAMAA HAWAKULETA TIMU!!
 
Back
Top Bottom