Leo nimeamka na wazo jipya,nafikiri iko haja ya mimi kwenda kugombea 1 ya nafasi za juu kabisa za uongozi wa team ya Simba,labda (nasema tena,labda) kosa langu ni kujipambanua mapema hapa JF kuwa moyo wangu umelalia wapi lkn No....nitakwenda, wengi (naomba nieleweke vizuri hapa,wengi) wa Wanachama na Mashabiki wa Simba ni Mazuzu hapana shaka watanichagua tu.
Waliambiwa Mwenyekiti amekamilisha kazi ya Twite na angetambulishwa kwenye Mkutano mkuu,siku ya mkutano inafika hola...wakaambiwa tena angekipiga siku ya Simba day,siku ya Simba Day ikafika hola,sasa imethibitishwa kuwa atakipiga Jangwani lkn bado Wapenzi na Wanachama wa Simba despite longolongo zote za Viongozi wao wanawaona TFF na kuongeza muda wa usajili kuwa ndo Mchawi wa kumtorosha Twite wao.
Haya kwenye Simba day pale Mh MahaRage akawahakikishia Wana Simba(kama ambavyo amewahi kuwahakikishia hapo nyuma kumsajili Asamoah,Nizar na Yondani kutochezea Yanga Kagame) kuwanYondani huyohuyo hatacheza Ligi kuu na kama Yanga watataka imtumie mchezaji huyu basi watatakiwa watoe Mill 60 fedha za kitanzania,Wanachama wa Simba wakashangillllliaa,wakiamini kuwa hivi karibuni team yao itavuna mahela mengine kwa kuuza mchezaji,eh.....
Kuna nini huko Simba?, unajua hali hii ya kuchezewa akili mchana kweupee inanifanya nianze kuamini kuwa inawezekana katika Dunia hii ushirikina upo kweli,naanza kuhisi siyo bure......
Wapenzi na wanachama wa Simba tafakarini na kuchukua hatua,hao viongozi wenu wameshawaona "MABOYA"