Simba Sport Club: Taarifa kwa umma

Lamkyeku

JF-Expert Member
Apr 18, 2014
494
661
SIMBA SPORTS CLUB
DAR ES SALAAM
2-10-2016

TAARIFA KWA UMMA

Kwa masikitiko makubwa klabu ya Simba imesikitishwa sana na vitendo vilivyofanywa na baadhi ya washabiki wetu,cha kuvunja sehemu ya viti vya Uwanja wa Taifa.kitendo kilichotokea jana kwenye mchezo wetu wa Ligi kuu dhidi ya Timu ya Yanga.

Tungependa kuomba radhi kwa kadhia hii na klabu imekubali kulipia gharama za uharibifu huu.
Klabu itazungumza na wamiliki wa Uwanja huu kuona inalipaje gharama hizo.
Ni mategemeo yeti kuona jambo hili halitajikoze tena.

Lakini mbali na hayo klabu kesho Jumatatu itawasilisha malalamiko rasmi juu ya uchezeshaji mbovu wa waamuzi wa mchezo wa jana,hususan Mwamuzi wa kati Martin Sanya.

Sisi tunaamini vitendo viovu vilivyofanywa na washabiki wetu vilisababishwa na uamuzi wa hovyo kupita kiasi uliosababishwa na waamuzi hao.

Haieleweki ni kigezo gani mwamuzi huyo alitumia kulikubali goli la 'mpira wa pete'la mshambuliaji wa Yanga Amisi Tambwe na kulikataa goli halali la mshambuliaji wetu Ibrahim Ajibu.

Pia tumeshangazwa na kitendo cha kumpa kadi nyekundu nahodha wetu Jonas Mkude.ilhali kama nahodha alimfata kwenda kumlalamikia kitendo chake cha kukubali goli la 'hovyo 'la Tambwe.
Sote tumeona Sanya alijikwaa wakati anarudi nyuma na kuanguka,kisha kuanguka na kutoa kadi nyekundu kwa Mkude.

Kimsingi huyu mwamuzi ana historia ovu ya kuwabeba Yanga.
Hakuna asiyesahau msimu uliopita kwenye kombe la Shirikisho,Yanga walipocheza na Coastal Union kule Mkwakwani Tanga.nini kilitokea!

Tunajua safari hii Tff na bodi ya Ligi zitatoa adhabu kali kwa waamuzi hawa ili iwe fundisho kwa maamuzi ya hovyo ya aina hii.

Pia klabu italalamika kitendo cha vyumba vyetu vya kubadilishia nguo(dressing room)kupuliziwa dawa zilizokuwa na nia ya kuwaathiri wachezaji wetu kabla ya mechi kuanza.

Tutaziomba mamlaka zifanye uchunguzi wa kina kubaini kitendo hiki kisicho cha kiungwana kinachosadikiwa kufanywa na wapinzani wetu.
Tunajua dhamira yao ni kuwafanya wachezaji wetu wachoke,lakini timu yetu ya Matabibu ilichukua hatua sahihi za kuwafanya wachezaji wetu waweze kumaliza dakika Tisini za mchezo kwa uwezo na weledi mkubwa.

Na mwisho klabu itoe malalamiko yake kwa Waziri wa mambo ya nchi,Mh Mwigulu Nchemba.

Waziri huyu bila shaka amesahau majukumu yake yake ya kazi na kugeuka kiongozi wa klabu ya Yanga.

Tunajua ni haki yake kuwa na mapenzi kwa klabu aliyoichagua.lakini vitendo vyake anavyovifanya vinaacha maswali mengi kuliko majibu.ukizingatia nafasi yake kama Waziri mwenye dhamana ya kuongoza Wizara nyeti.

Itakumbukwa majuzi waziri huyu alifanya ziara Mkoani Morogoro kuzungumza na vikosi anavyoviongoza.
Na inajulikana pia Refarii wa mchezo wa jana Martin Sanya ni mwajiriwa wa Jeshi la Magereza mkoani Morogoro

Sote tulishuhudia Jana Mwigulu alishangilia goli la hovyo la mwajiriwa wake Sanya.

Pia waziri huyu alitoa kauli tata kuwa angetamani siku moja klabu inayoshangilia wapinzani wa Yanga wakipigwa mabomu ya machozi na Askari wa jeshi la Polisi.
Kauli hii aliitoa wakati wa sherehe za kukabidhi zawadi kwa timu zilizoshinda msimu uliopita zilizoandaliwa na wadhamini wa ligi.kampuni ya Vodacom.

Tunajiuliza yale mabomu ya jana pale Uwanja wa Taifa ndio utekelezaji wa maagizo ya boss Mwigulu?

Lakini pia matumizi ya rasilimali za umma yakiwemo magari ya serikali ktk shughuli za mara kwa mara za klabu ya Yanga napo kunaacha maswali mengi mno.

Wanasimba wanauliza kila Waziri anayeshabikia Simba akiwepo Waziri Mkuu akifanya vitendo hivi kutakuwa na utawala gani serikalini?

Imani yetu viongozi wakuu wa nchi watamuonya mh Mwigulu,vingenevyo atatengeneza chuki baina ya washabiki wa Simba dhidi ya serikali yao.
Mwigulu atambue klabu ya Simba ina mamilioni ya washabiki kama ilivyo klabu yake anayoishabikia.

Hatutarajii kuona 'mahaba'yake yasio na staha yanachochea jambo ovu kwa wanasimba na serikali yao wanayoiamini na kuipenda sana.

IMETOLEWA NA
KLABU YA SIMBA

SIMBA NGUVU MOJA
 
Taarifa imeharibiwa na maneno mengi yasiyo na miguu wala mikono. Kuhusu kushangilia goli hata mtangazaji mmoja alisema 'anaweka mpira kifuni anageuka na kuiandikia yanga bao' Kwamba mpira ulimbabatiza mkononi ilionekana zaidi kwenye replay. Hata world cup haya makosa yapo.
 
Taarifa imeharibiwa na maneno mengi yasiyo na miguu wala mikono. Kuhusu kushangilia goli hata mtangazaji mmoja alisema 'anaweka mpira kifuni anageuka na kuiandikia yanga bao' Kwamba mpira ulimbabatiza mkononi ilionekana zaidi kwenye replay. Hata world cup haya makosa yapo.
Hahahahahaaaa
 
Taarifa imeharibiwa na maneno mengi yasiyo na miguu wala mikono. Kuhusu kushangilia goli hata mtangazaji mmoja alisema 'anaweka mpira kifuni anageuka na kuiandikia yanga bao' Kwamba mpira ulimbabatiza mkononi ilionekana zaidi kwenye replay. Hata world cup haya makosa yapo.
Unajua issue ya Goli LA Tambwe inakuja baada ya kukataa Goli sahihi kabisa la ajib. Angekubali Goli ya Ajib hata yote yasingetokea. Unakataa goli mzuri tu lisilo na kasoro wala wa lakini unakubali goli ya Kijinga namna ile unategemea nn?
 
unajua watz tuna shida snki ukweli coz kuna uhusiano gani kati ya goli la Tambwe na viti?? hivi ni mara ya kwanza goli kufungwa tena kwa mkono katika ulimwengu wa soka??hivi tunawezaje kumlaumu refa kwa kila jambo kwani yeye si binadamu??mfano golila Ajibu aliyesema sio goli ni mshika kibendera wa upande ule kuwaaliotea kitu ambacho kinasadikika haikuwa ameotea sasa kwanini tumlaumu sanya??Afu goli la Tambwe refa alikuwa karibu lkn kwa alivyogeuka Tambwe ni sekunde ilikuwa so kuona moja kwa moja kama aliunawa ule mpira ilikuwa ngumu so tusilaumu sana tukashindwa kufanya mambo ya maendeleo.
Isitoshe jiulizeni ile ilikuwa ni.mpira kufuata mkono au mkono ulifuata mpira???
so tuache kulalamika lalamika tujipange kisoka matokeo hayabadiliki tutabaki tunalalamika tuuu hata maradona alifunga kwa mkono na kombe la dunia kabeba.
 
kulipa tutalipa tu lakini muungwana ni vitendo wenzetu wana yanga bundi ndo anaanza kuingiza kichwa chake kaeni chini muanze kuutafuta ugonjwa kwa sasa ni mkuki kwa nguruwe pia tff kwa kuzuiliwa kuutumia uwanja wa taifa nao wanakosa kipato na wala siyo kuziumiza timu ila nao ni ujumbe tosha kuwa hawawezi kuongoza mpira wa tanzania ndiyo maana tunaajiri makocha kila leo na hatufiki mbali kutokana na viongozi kuwa na unazi wa uyanga yanga.Kwa upande wa serikali naomba ukipewa jukumu la kitaifa basi simamia utaifa pia naiomba serikali iiadhibu pia na tff kwa kushindwa kusoma alama za nyakati kwani si mara ya kwanza kwa tff kufanya makosa haya na badala yake wanaadhibiwa timu kwa makosa ya tff nafikiri pia wadau walishauri kuwa kwa mechi kama hizi waje marefarii kutoka nje wasiojua simba wala yanga
 
Taarifa imeharibiwa na maneno mengi yasiyo na miguu wala mikono. Kuhusu kushangilia goli hata mtangazaji mmoja alisema 'anaweka mpira kifuni anageuka na kuiandikia yanga bao' Kwamba mpira ulimbabatiza mkononi ilionekana zaidi kwenye replay. Hata world cup haya makosa yapo.
Acha ushabiki uchwara wewe ule mpira alitumia mkono Ku control ndio maana alikunja mkono na kushika mpira huko sio kubabatiza
 
kuhusu viti kuharibiwa inahitajika tuende mbele zaidi katika upeo wa akilo zetu na tusiwe wa kutoa majibu kwa kuropoka .Ukweli mimi nasema nijibu la tatizo lililokosa ufumbuzi kwani tatizo ni tff kushindwa kukisikoa kilio cha mashabiki kwa uonevu na matumizi mabaya ya madaraka kwa viongozi wa tff kwani imeundwa kwa mfumo wa ushabiki wa timu fulani . mi nashauri hata wao wapewe gharama ya kulipa ujaribifu huu.mimi naamini kuwa kuvunjwa viti si mara ya kwanza hivyo tff ilipaswa kusoma alama za nyakati kwa kuchagua refa sahihi wa kuchezesha mpambano wa jadi.Pia ijulikane kuwa watanzania wote tunakaelementi ka usimba na uyanga hivyo yanayo jitokeza ni majibu ya kutokuwaza tumezoea kubebana tu ni aibu naomba tff iazibiwe vikali sana kuanzia malinzi mpaka afisa habari wake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom