Simba SC yashinda 2-0 dhidi ya Kahraba FC kwenye Mechi ya Kirafiki

Simba SC yashinda 2-0 dhidi ya Kahraba FC kwenye Mechi ya Kirafiki

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
1754986087590.png

Kikosi cha Simba kilichopo Misri, katika maandalizi ya msimu mpya wa NBC Premier League na mashindano ya kimataifa, kimecheza mchezo wa kwanza wa kirafiki wa kujipima nguvu na timu ya Carabat FC, ambapo Mnyama ameshinda magoli 2-0.

Bao la Mohamed Bajaber katika mechi ya kirafiki dhidi ya Kahraba Ismailia katika uwanja wa Suez Canal Authority.

Kahraba Ismailia SC, inacheza Ligi Kuu ya Egypt na imeshacheza mchezo mmoja wa ligi ya Egypt dhidi ya El Gouna ambayo walifungwa pia bao 1-0.

Goli la kwanza lilifungwa kipindi cha kwanza na mchezaji Mohammed Bajaber huku goli la pili likifugwa kipindi cha pili na Jonathan Sowah.

Jonathan Sowah akifunga bao la pili katika mechi ya kirafiki dhidi ya Kahraba Ismailia

Wikiendi ijayo Kikosi cha Simba SC kitahamisha kambi yao kutoka Ismailia kwenda Cairo ambako watacheza michezo mingine ya kirafiki kabla ya kurejea Tanzania.

1754978036458.png
 
Kikosi cha Simba kilichopo Misri, katika maandalizi ya msimu mpya wa NBC Premier League na mashindano ya kimataifa, kimecheza mchezo wa kwanza wa kirafiki wa kujipima nguvu na timu ya Carabat FC, ambapo Mnyama ameshinda magoli 2-0.

Goli la kwanza lilifungwa kipindi cha kwanza na mchezaji Mohammed Bajaber huku goli la pili likifugwa kipindi cha pili na Jonathan Sowah.

Ndugu mwandishi ungetuambia pia hiyo Kahraba ni timu ya daraja la ngapi. Natambua fika ni kipindi cha pre season.
 
Ngoja utopolo na wenyewe wajibu mapigo kwa kucheza na Kimbiji Kombaini
Utopolo siku zote hucheza na wakina kimbiji kombaini, mbagara market, n k lakini mataji anabeba na Simba inayocheza mechi za kirafiki ughaibuni anatandakwa na utopolo inayocheza na kimbiji kombaini.
 
Back
Top Bottom