Simba SC yabebwa Mapinduzi Cup

Mwanagandila

Senior Member
Oct 9, 2011
182
100
Timu ya Simba Sports Club jana usiku imeshindwa kutamba mbele ya timu ya Miembeni United inayomilikiwa na Aman Makungu.
Katika mchezo wa jana usiku katika uwanja wa Amani mpaka dakika ya 90 timu zote zilikuwa 3-3 hali iliyomfanya mmiliki wa timu ya Miembeni ashuke chini kwenye benchi la ufundi kwenda kumuambia kocha awaambie wachezaji wawaachie Simba wapate bao la nne.
Dakika moja baada ya kutoa maagizo hayo baadhi ya wachezaji wa Miembeni waliendelea kuwa imara na hasa golikipa wao Abbas alikuwa kikwazo kwao, dakika ya 92 Kocha wa Miembeni alimuita Uhuru Selemani wa Simba na kumuambia mbona hamfungi wewe ingia mpaka golini mabeki hawatakukaba, na sekende baadaye Uhuru alifanya hivyo mabeki hawakumkaba na kwenda kufunga bao la nne na ushindi, baada ya kufunga bao hilo tu refarii alimaliza mchezo.
Mashabiki wa soka mjini hapa walikerwa na kitendo cha Amani Makungu kuwaambia timu yake iwaachie bao Simba amabapo washabiki hao walipokwenda kumuuliza kwa nini amefanya hivyo akasema Simba ingetoka yeye atakosa hela!
Hayo ndo mambo ya soka la Tanzania mwenye timu ana amri
Hongera Simba kwa kubebwa
 
aiseee... bongo kila kitu mbona shaghala naghala......
 
Mleta habari hii ni nani?

.....Kocha wa Miembeni?
......shabiki wa Miembeni?
.....Refa wa mchezo huo?

Nadhani hii ingefaa zaidi kuwa kwenye jukwaa la udaku.

Simba Hoyeeeee..!!!!!!!
 
Jamani kama hali ya mechi hiyo ilikuwa hivyo then kwanini timu husika zisitolewe kwenye mashindano hayo, coz sioni watakwepa wapi adhabu kama ushahidi upo wazi kama ulivyo semwa hapo juu.
 
Alafu tunabaki kulalamika timu ya taifa haifanyi vizuri.kwa soka hii afadhali tukacheze soka ya mchangani
 
Mpaka sasa Yanga na Azam keshapigwa tatu bila kipindi cha pili.

Kocha wa Azam atatoa maelekezo kwa wachezaji wake wawaachie Yanga wasawazishe li waende wote semi final!

Ha ha haaa...!!!
 
duuuuuu! nimecheka hadi baasi. mkuu inaonekana una hasira sana
 
Yanga kapigwa 3-0 na azam,hao viongozi wa yanga ndio wajue umuhimu wakuwalipa wachezaji mishahara yao,kwa mwendo huu zamalek watawafunga yanga hata goli 20 wakipenda.
 
hahahahahahaha...huyo ndio Aman Makungu...na Hiyo ndio Simba Sc...

hapo ndipo nilipogundua ubovu wa timu inapokuwa ya mtu mmoja, hakuna wa kupinga wala kumbishiaaa... malengo yake yametimia baada ya jana Simba kushinda na timu yake ya miembeni kutolewa, hivyo simba inacheza na Azam jumatatu nusu fainali
 
Back
Top Bottom