Linguistic
JF-Expert Member
- Mar 16, 2021
- 3,671
- 8,237
Unapokuwa mwamba wa soka nchini kwa miaka minne mfululizo, na unapojenga sifa na heshima Afrika kwa miaka mitano, na kuwa timu pekee ya Tanzania inayojulikana huko duniani, unapokuja mwaka mmoja ukajikwaa ukihuzunika unamkufuru Mungu.
Kwa Ligi yenye figisu na siasa za “ku-balance” kati ya watani wa jadi, kuchukua ubingwa kwa miaka minne mfululizo na Kombe la FA kwa miaka mitatu mfululizo ni jambo lisilowezekana. Bayern Munich ni timu inayotamba Ujerumani lakini kuna miaka wanakosa Kombe. Tukubali kwa roho safi kwamba mwaka huu haukuwa wetu. Sababu:
.
1. Tumekumbwa na jinamizi la majeruhi kuliko ilivyo kawaida, kwani hakuna mchezaji hata mmoja ambaye hakukaa nje ya uwanja;
2. Tumebadilisha makocha katikati ya misimu mara mbili mfululizo.
3. Tumekuwa kwenye kipindi cha mpito kwa kuingiza wachezaji wapya vijana kwa mpigo.
4. Huku tukiwa na majeruhi, timu yetu imecheza mechi 12 zaidi ya timu nyingine za Ligi Kuu (mechi za Confederation na Mapinduzi).
5. Wenzetu waliutaka Ubingwa kwa kufa na kupona kuliko sisi. Kwa tajiri wa Yanga, ubingwa wa Yanga ni shughuli ya kujijenga kwenye jamii. Kwa tajiri yetu, mpira ni hobby
6. Viongozi wa soka na Bodi ya Ligi walikuwa kwenye vita dhidi yetu kutokana na siasa za “ku-balance”.
Tufanyeje kuanzia hapa tulipo?
1. Tutulie. Tusipaniki. Tutataniwa sana na watani wetu na wanayo haki kwani kukosa Ubingwa kwa muda mrefu ukiupata lazima ukimbie uchi mji mzima kwa furara. Lakini tuvumilie. Masikini akipata matako hulia mbwata.
2. Tuachane na benchi la sasa la ufundi. Kocha tuliye naye hatoshi. Hajaleta falsafa mpya ya uchezaji. Fitness coach hatoshi kwani majeraha mengi ni ya misuli ambayo chanzo ni fitness. Physio wa timu hatoshi. Tusitafute kocha wa muda mfupi mfupi.
3. Tuachane na wachezaji wazee wasioongeza chochote kwenye timu. Tuangalie mbele badala ya kuangalia nyuma. Future ya Simba ni Mwinuke, Israel Mwenda, Peter Banda, Sakho, Kanute, Kibu, Duchu (arudishwe kutoka kwenye mkopo). Wana umri mzuri. Waaminiwe na wapewe nafasi. Tusijenge timu ya msimu mmoja au miwili kama wenzetu.
4. Msimu ujao tutacheza round moja kabla ya kuingia group stage ya Klabu Bingwa Afrika, na tutapangiwa timu ndogo. Watani zetu watalazimika kucheza round mbili na watapangiwa timu ngumu. Wao watabaki, sisi tutavuka. Tusajili kwa ajili ya Klabu Bingwa Afrika. Hiyo ndio Ligi yetu kila mwaka inayotutambulisha duniani. Mchezaji yoyote mzuri Afrika atapenda kuchezea Simba. Tunayo sifa na uwezo wa kuvutia wachezaji bora kabisa kwenye Bara hili.
5. Tukamilishe miradi ya kuendeleza timu tuliyoipanga…kituo cha mazoezi, uwanja na masuala mengine ya mapato kwa Klabu.
Simba bado ni timu bora Tanzania. Ni timu inayocheza mpira bora zaidi. Ni timu iliyo na mafanikio zaidi kwa miaka ya karibuni.
Ni timu inayoibeba nchi barani Afrika kwa kuitangaza nchi lakini pia kwa kuifanya ipeleke timu nne kwenye mashindano ya Afrika kila mwaka.
Ni timu inayoongozwa kwa weledi zaidi. Tusimkufuru Mungu kwa kuhuzunika sana na matokeo ya mwaka huu.
Tuwapongeze na kuwatia moyo wachezaji na viongozi kwa jitihada waliyoiweka mwaka huu. Simba Nguvu Moja.
Ndimi
Edwin Silayo
Moshi
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app