Last emperor
JF-Expert Member
- Mar 22, 2015
- 10,346
- 9,889
Nawasalimia wana Msimbazi wenzangu!
Nimesikitishwa na mpira unaochezwa na timu yetu pendwa ya Simba (Lunyasi), timu siku hizi inacheza mpira mbaya sana, mpira makande, magoli yetu yenyewe yanapatikana kipapatupapatu kama ya utopolo. Leo nimeona takwimu eti Simba katika mechi 2 za ligi ndo tunaongoza kwa kupiga cross (cross 34!) Tangu lini Simba ikaongoza kwa kupiga cross na sio kupiga pass?
Kuna watu watakuja na utetezi kuwa timu Ina wachezaji wapya wengi, hivyo hawajaingia kwenye mfumo wetu wa Lunyasi. Hii sio kweli, maana ukiangalia kwenye timu iliyoanza (first eleven) ni wachezaji wawili tu ndo wageni ambao ni Inonga na Kanoute, lakin wengine wote ni walewale wapo zaidi ya misimu miwili. Na hata wanaosema kuondoka kwa Luis na Chama ni sababu ya timu kucheza hovyo siku hizi, nayo sio kweli, kuondoka kwa wachezaji wawili hakuwazuii watu kupiga pass na kucheza mpira uliozoeleka, maana hata hao wachezaji wawili walikuja waliikuta timu inacheza mpira biriani.
Tatizo kubwa ninaloliona ni kocha. Gomez ni kocha anaejali zaidi matokeo (results oriented) kuliko kujali namna ya hayo matokeo yanapatikanaje. Wana msimbazi tumezoea mpira biriani, Gomez alikuja akaikuta timu imetengenezwa na Uchebe na Kishingoo, na yeye akatembelea humo. Na zaidi ni Uchebe ndo aliitengeneza timu iliyocheza mpira biriani tunavyotaka.
Ombi langu kwa uongozi wanatakiwa wamuambie kocha sisi tunataka timu icheze mpira unaoeleweka, na sio mradi kupata ushindi wa style ya utopolo. Magoli ya kona na cross ya piga nikupige. Kama Gomez hawezi kutupa mpira tunaotaka atimuliwe!
Sio siku hizi...huyu kocha hana uwezo wa kufundisha mpira biriani.Kocha lazima ajali matokeo, na matokeo mazuri ni mandalizi n uhodari wa team.
Ukitaka kujua uwezo wa Simba na upate entertainment wacheze na azam.
Azam wana mchezo wa kitaalam ambao unawapa Simba fursa ya kuonyesha uwezo wao.
Sasa kama unaitwa mjinga..Mimi nitakuita Nani?Wewe utakuwa utopolo tu.
Ila unajificha.
Rivers United wanakupa hi
Tunataka vyote. Mbona zamani tulikuwa tunacheza na tunapata matokeo? Tunataka vyote. Msimu wa 2017/2018 tulichukua ubingwa baada ya kuletwa yule kocha aliyetupa ubingwa kwa kandarasi ya miezi 6 Pierre Lechantre, lakin hakuongezwa mkataba kwasababu alikuwa anatupa matokeo lakin mpira mbovu. Ndo akaja Uchebe akatengeneza hii timu, ikawa inacheza mpira mzuri na ubingwa tunachukua. Sasa huyu Gomez anaturudisha kwenye mpira makande. HatukubaliKwani mkuu kipi Bora Kati ya Timu icheze vizuri na isipate matokeo chanya VS Timu icheze hovyo ila ipate matokeo chanya,hakika hata Mungu tunamchanganya sana
Pirre lechantre alikuwa anacheza mpira mbovu?Tunataka vyote. Mbona zamani tulikuwa tunacheza na tunapata matokeo? Tunataka vyote. Msimu wa 2017/2018 tulichukua ubingwa baada ya kuletwa yule kocha aliyetupa ubingwa kwa kandarasi ya miezi 6 Pierre Lechantre, lakin hakuongezwa mkataba kwasababu alikuwa anatupa matokeo lakin mpira mbovu. Ndo akaja Uchebe akatengeneza hii timu, ikawa inacheza mpira mzuri na ubingwa tunachukua. Sasa huyu Gomez anaturudisha kwenye mpira makande. Hatukubali
Hahaahah!Tunataka vyote. Mbona zamani tulikuwa tunacheza na tunapata matokeo? Tunataka vyote. Msimu wa 2017/2018 tulichukua ubingwa baada ya kuletwa yule kocha aliyetupa ubingwa kwa kandarasi ya miezi 6 Pierre Lechantre, lakin hakuongezwa mkataba kwasababu alikuwa anatupa matokeo lakin mpira mbovu. Ndo akaja Uchebe akatengeneza hii timu, ikawa inacheza mpira mzuri na ubingwa tunachukua. Sasa huyu Gomez anaturudisha kwenye mpira makande. Hatukubali
Huyo ni uto, yeye anazani klabu bingwa kuna ubiriani hasa hizi hatua za mtoanoTimu imeshinda bado unalalamika,Utopolo wamepigwa nje ndani na faini juu.
Wakati timu ikiandaa biriani acha kwanza ushindi upatikane alafu biriani ikiiva utakula.
Hatua za mtoano zina presha zake, ni tofauti na hatua ya ligi ndefu au makundi ambapo unakuwa na muda wa kujaribu hivi na vile kwa kusahihisha makosa na kuendelea na mazuri. Katika mtoano, ukikosea tu ukakosa goli ugenini au ukaruhusu goli nyumbani, kuna hatari hata ya kukosa fursa ya kuja kuonyesha biriani lako kwenye makundi. Mfano mwepesi ni jinsi tulivyoshindwa kupata goli la ugenini katika mechi za mtoano za UD Songo na ile ya Kaizer Chiefs. Mechi hizo mbili kwa miaka miwili tofauti, kama tungepata goli moja ugenini basi tungesonga hatua inayofuataNimesikitishwa na mpira unaochezwa na timu yetu pendwa ya Simba (Lunyasi), timu siku hizi inacheza mpira mbaya sana, mpira makande, magoli yetu yenyewe yanapatikana kipapatupapatu kama ya utopolo.
Andaa timu yako tafuta kocha wako halafu baada ya miezi sita njoo ufufue huu uzi wakoTunataka vyote. Mbona zamani tulikuwa tunacheza na tunapata matokeo? Tunataka vyote. Msimu wa 2017/2018 tulichukua ubingwa baada ya kuletwa yule kocha aliyetupa ubingwa kwa kandarasi ya miezi 6 Pierre Lechantre, lakin hakuongezwa mkataba kwasababu alikuwa anatupa matokeo lakin mpira mbovu. Ndo akaja Uchebe akatengeneza hii timu, ikawa inacheza mpira mzuri na ubingwa tunachukua. Sasa huyu Gomez anaturudisha kwenye mpira makande. Hatukubali
UtopoloSasa kama unaitwa mjinga..Mimi nitakuita Nani?