Kichwa kikikosa akili mwili upo taabuni
vipi simba sasa mnataka kufungua tawi la ze comedy?nacheka kweli kweli hapa nilipo,yanga wanaenda uturuki mmoja wenu aombe lifti kwenye dege linalowapeleka angalao atasimama muifuate ile ramani ya uwanja.Ningemuelewa kama wangemtenda vyema Mafisango other wise ni usanii tu, inamaana msiba wa mtunga nyimbo ya club unauma sana kuliko mchezaji? Tuachie Simba yetu tupumue.
Niaje KubwaJinga?
Hebu nipe tathmini yako kisoka, wakati huu ambapo uongozi wa Munyama una mengi ya kuwaeleza washabiki wake; ombwe la uongozi, sakata la familia ya Petit Mafisango, ugomvi kati ya Rage (sio uongozi) na tawi la Mpira Pesa, matokeo mabovu kwenye ligi na kadhalika, kuna haja ya kujipendekeza kutuma salamu za rambirambi kwa marehemu Hussein? Basis waliyoitoa eti Sharo alikuwa anataka kufanya nyimbo yao ya timu, kwa hiyo wanatuma rambirambi kwa mshauri wao wa kibiashara.
Ptuuuuuh...
Kwa maoni yangu huku ni kujibaraguza, kutafuta huruma-au kuwasahaulisha washabiki wa Simba wasizingatie matatizo ya klabu kwa sasa, mchanga wa macho huu.
Sijasahau uwanja wa Bunju ambao kiuhalisia haupo...
Heshima mbele Mphamvu...
Ishu hapo ni ndogo mno.
Rage anataka kuiongoza timu kama vile anaongoza jimbo.
Anatumbukiza Siasa kwenye maswala ya Soka.
Anatumbukiza bla bla za siasa katika mambo ya Soka.
Hayo mambo ya kwenda kuandika waraka mrefu kama huo wakati timu iko katika wakati mgumu ni mbinu ya kuwasahaulisha wanachama wa Simba zile jazba walizonazo juu ya uozo wa timu yao uliojitokeza hivi karibuni.
Tumeshashuhudia wanasiasa wa Tanzania kujificha nyuma ya tukio flani ili kukwepa majukumu waliyonayo.
Mfano wanasiasa kuushadadia msiba wa Marehemu Kanumba wakati wana mengi ya kujieleza na kuyajibu kwa wananchi waliowachagua.
So wanachama wa Simba amkeni, msidanganywe na hio ujinga.
Mnachezewa akili na huyo Baniani
Wakati uchaguzi wa Simba unafanyika miaka mitatu nyuma, niliwashangaa wanachama wa Simba kumchagua ex-mwenyekiti wa Moro United kuwa mwenyekiti wao mpya, lau kama ingekuwa ni nafasi ya kuajiriwa isingenishangaza, ila ilikuwa nafasi ya kuchaguliwa ambayo kwa uzoefu wangu mdogo inawahusu wanachama tu.
Sasa Ismail Aden alikuwa mwanachama wa timu mbili kwa wakati mmoja?
Kujificha nyuma ya matukio huyu ex-konvict hakuanza leo, mwaka ule aliporejesha umeme jengo la Simba ilikuwa ndio habari ya mjini, wakati kiuhalisia sio big issue kivile, mara ngapi watu huwa tunarudisha umeme majumbani kwetu?
Unazi ndo umetufikisha hapa, tunapokutana washabiki wa Sunche na Kapeto na kuanza kubishana kila mtu anatetea upande wake hata kama maji matupu, na hapo ndipo washabiki wa Simba wanapolazimika kumbeba mtu ambaye amewahi kukaa jela kwa tuhuma za ubadhilifu ndani ya soka.
Shall we make it? Chambilecha Hamza Kassongo...
Na huyohuyo mla Mirungi alisemaje vile endapo Yondani atachezea Yanga?
Alitishia kuishtaki Yanga na TFF kwa kumsaini mchezaji usiku tena kwa kumuiba kambini.
Hata kwenye sakata la Twite, nilishangaa kwanini wanachama wa Lunyasi walishindwa kumwajibisha mwenyekiti wao kwa kutumia resources za timu kwenda Rwanda kusajali mchezaji kwa magumashi, badala yake wakaungana nae kuwalaumu kina Bin Kleb kwa kuwachezea rafu.
Leo hii Mpira Pesa wametumia haki yao kikatiba kuita mkutano halali, wametokea wanachama walioshikwa masikio kumuunga mkono Rage.
Ni kwamba hata maneno aliyoyatamka Rage au Simba kuhusu misiba ya wasanii au wachezaji yawe mabaya au mazuri namna gani, at the end of the day kazi kuu ya klabu ya soka ni kuwa na timu inayoshinda mechi muhimu na vikombe muhimu, na mfano ni huo wa 5 - 0. That's the context !Whats the context?