Simba naona mnakuja kivingine rage mbaya weweeeeeeeeeeee!!hapo watatulia tu

Ni kwamba hata maneno aliyoyatamka Rage au Simba kuhusu misiba ya wasanii au wachezaji yawe mabaya au mazuri namna gani, at the end of the day kazi kuu ya klabu ya soka ni kuwa na timu inayoshinda mechi muhimu na vikombe muhimu, na mfano ni huo wa 5 - 0. That's the context !

Kekundu.
Kama hii ndio aina ya wanachama tulionao basi kazi ipo...
Kama kazi ya mwenyekiti ni kuhakikisha ushindi unapatikana kazi ya kocha na benchi lake la ufundi itakuwa nini sasa?
 
Kekundu.
Kama hii ndio aina ya wanachama tulionao basi kazi ipo...
Kama kazi ya mwenyekiti ni kuhakikisha ushindi unapatikana kazi ya kocha na benchi lake la ufundi itakuwa nini sasa?
... Ni kushirikiana na wachezaji katika implementation ya mipango ya mwenyekiti/timu inayohusiana na pale dimbani.
 
... Ni kushirikiana na wachezaji katika implementation ya mipango ya mwenyekiti/timu inayohusiana na pale dimbani.

Sijui huelewi au unafanya makusudi?
Soka lina pande mbili, technical side na administrative side. Hata kama timu inashinda mechi (ingawa Simba haishindi) kuna mambo ya kiutawala ambayo lazima yasonge vizuri ingawa sio mchezo wenyewe.
Lazima timu isafiri, uwanja uhudumiwe (kama upo), jezi ziuzwe, televisheni ya timu ifanye kazi na kadhalika na kadhalika. Technical aspect inamhusu kocha, kamati yake ya ufundi na wachezaji na wanaripoti kwa mkurugenzi wa ufundi (Kwa Simba huyu ni Ibrahim Maestro), mambo mengine ya kiutawala yanasimamiwa na hili jopo linalobaki linalosukumwa na Rage.
Ukiwa kama mnazi mpofu wa Simba hautakiwi kushikilia kuwa 5-0 (of which matatu yalikuwa ya penati za zawadi toka kwa Nsajigwa) ndio kipimo cha ubora wa Rage.
Hapa ni kwa GT's na sio gogo vivu pale Msimbazi, lazima tujadili vitu juu ya ukawaida kama tuna nia ya kuikwamua timu yetu.
Behave...
 
Ni kwamba hata maneno aliyoyatamka Rage au Simba kuhusu misiba ya wasanii au wachezaji yawe mabaya au mazuri namna gani, at the end of the day kazi kuu ya klabu ya soka ni kuwa na timu inayoshinda mechi muhimu na vikombe muhimu, na mfano ni huo wa 5 - 0. That's the context !

Kwa hiyo ameifunga YANGA 5 ata ule uwanja wa BUNJU asijenge? ata akifungwa na Mtibwa,Toto halafu awe wa 3 kwenye msimamo ni sawa sababu kaifunga YANGA 5...ndio unachomaanisha wewe mwenyewe akili kama za GOZI.
 
…
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MWENYEKITI wa klabu ya Simba, Mhe; Ismail Aden Rage, amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa aliyekuwa msanii maarufu wa muziki na filamu, Hussein Ramadhani Mkiety, maarufu kwa jina la Sharo Milionea, kilichotokea jana usiku mkoani Tanga.
Kwa niaba ya klabu ya Simba na kwa niaba yake binafsi, Mwenyekiti anapenda kutuma salamu za pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki wote wa marehemu kutokana na msiba huu mkubwa sana si kwao pekee bali kwa taifa zima la Tanzania.
Sharo Milionea hakuwa msanii wa kawaida. Yeye ni miongoni mwa kizazi kipya cha vijana wa Kitanzania walioamua kutafuta maisha kwa kutumia vipaji walivyopewa na Mungu. Yeye alijitumbukiza zaidi katika uchekeshaji na baadaye akaonyesha uwezo mkubwa katika fani ya muziki.
Sharo alikuwa maarufu kiasi kwamba makampuni makubwa yalikuwa yameanza kumtumia kwenye matangazo yao ya kibiashara. Hii ilionyesha kwamba makampuni yalibaini faida itakayopatikana kwao kwa kumtumia msanii huyu ambaye bado alikuwa na heshima kubwa kwenye jamii kutokana na haiba yake na uwezo wake kwenye kazi alizokuwa akifanya.
Msiba huu umekuwa pigo kubwa kwa tasnia ya filamu ambayo bado inaomboleza vifo vya wasanii kama Steven Kanumba, Mlopelo na John Steven Maganga, waliofariki dunia mwaka huu pia.
"Ifahamike kwamba Sharo Milionea alikuwa miongoni mwa wasanii wa Kitanzania waliotuma maombi Simba ya kutaka kushiriki kwenye mchakato wa kutengeneza wimbo rasmi wa klabu ya Simba. Yeye alikuwa miongoni mwa wasanii waliokuwa wakiumizwa na ukweli kwamba klabu kama Simba inashindwa kufanya biashara ya kuuza nyimbo zake ilhali wanunuaji wapo," alisema Rage.
Kwa klabu ya Simba, namna pekee ya kumuenzi marehemu ni kufanyia kazi mambo ambayo alikuwa akitushauri kwenye eneo la biashara. Ni matumaini yetu kwamba iwapo tutafanya lile alilokuwa akitushauri, atakuwa mwenye amani huko alikotangulia mbele ya haki.
Rage amewaomba wasanii wa tasnia ya filamu na muziki kuwa watulivu na wenye subra kwenye kipindi hiki kigumu kwao. Kila kitu katika maisha ya wanadamu kinapangwa na Mwenyezi Mungu na ndiyo maana Waswahili wana msemo kuwa Kazi ya Mungu haina makosa.
Mola na ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Hussein Ramadhani Mkeity (Sharo Milionea).
Imetolewa na
Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC.

ndo nini sasa?nahis umetumia 0713.....
 
Back
Top Bottom