SIMBA NA YANGA DUUUUUUH

mahunduhamza

Member
Joined
Aug 25, 2021
Posts
19
Reaction score
46
Klabu ya Yanga imewachapa watani wao wa jadi Simba SC na kuizuia klabu hiyo kutangazwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania kwa msimu wa 2020/2021.
Mabingwa watetezi Simba walihitaji kupata alama tatu ili kutawazwa mabingwa kwa msimu wa nne mfululizo.
Hata hivyo goli la dakika ya 13 lililofungwa na Zawadi Mauya liliitosha Yanga kuifunga mdomo Simba na kulinda hadhi yake. Laiti Yanga ingelifungwa, maana yake watani wao wangetangazwa mabingwa kupitia mgongo wao.
Hata hivyo licha ya kufungwa bado Simba wapo katika nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa. Simba sasa inahitaji kushinda michezo miwili kati ya minne aliyosalia nayo ili kuchukua ubingwa. Hata hivyo, ubingwa huo utakosa kionjjo muhimu cha kumfunga Yanga katika mechi zote mbili za msimu huu. Mechi ya raundi ya kwanza Simba na Yanga zilitoka sare ya goli 1-1.
 
Mkuu uko ndotoni! Au mwenzetu memory card ya kichwa chako iliingia vairasi!! Na sasa ndiyo imeanza ku process outdated news!!
 
Watu wanaishi kwenye caves nawaambia.

Mi sifatilii mpira ila hao majamaa wakicheza nitajua tu.
 
Chanjo hiyo
😁😁😁 Jamaa memory ya kichwa imepoteza kabisa mwelekeo! Yaani tukio limetokea miezi miwili nyuma, ndiyo leo analianzishia uzi!

Kama chanjo yenyewe iko hivi, bora tu niahirishe aisee!!
 
Dishi limeyumbaaaaa likarudi!
Likayumbaaaaaa likarudi lilipoyumba Tena na kurudi automatic jamaa akajiona yupo mwaka 2006

Milembe mjeni muuchukue msukule wenu huku!
 
Miezi miwili ijayo jamaa atakuja na uzi wa Haji kuhamia Utopolo...

🀭🀭🀭😁😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…