Simba na Rufaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simba na Rufaa

Discussion in 'Sports' started by Makoye Matale, Jun 20, 2011.

 1. Makoye Matale

  Makoye Matale JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 6,480
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Ni dhahiri kuwa kwenye utawala bora mtu asiporidhishwa na jambo fulani anayo haki kukata rufaa kwa chombo cha juu cha maamuzi.
  Simba SC ilikata rufaa dhidi ya Bw. Kabangu kuchezeshwa na TP Mazembe isivyo halali na CAF wakaipa Simba haki yake. Ushindi huo wa rufaa uliisaidia Simba kukutana na Wydad Casablanca kule Misri na kubugizwa bao 3 ndani ya dk. 3 za mwisho. Hata hivyo kichapo hicho hakikuwa na maumivu sana kwa vile mnyama alikuwa amejihakikishia nafasi ya kukutana na DC Motema Pembe katika kombe la Shirkisho. Furaha ililipuka pale Msimbazi baada ya Mnyama kuibuka kidedea 1-0 katika uwanja wa taifa.

  Loo! la kuvunda halina ubani, matokeo ya jana yamemfanya mnyama aishiwe nguvu na aone haya mbele za uso wa dunia hii. Hata hivyo zipo habari kwamba Mnyama alinyanyasika sana na waamuzi wa mchezo huo kwa mfano inadaiwa goli la kwanza halikuwa halali, Kaseja alidaka na refa akaamuru mpira uwekwe kati. Kwa vile mimi sikuwepo uwanjani, siwezi kusema chochote kuhusu bao hili.

  Nashauri Rage mwenyekiti makini asiyekuwa Garasa kama yule mzee mweupe, akate rufaa tena ili aivushe Simba isiyokuwa na Msemaji Mkuu. Nimekuwa nikimsikia Mbassa akizungumzia mambo ya Simba nje ya nchi hivi yule naye ni msemaji wenu? Kama sivyo, mbona hivyo?
   
Loading...