Simba mwaka huu marefa wanatuonea

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,129
2,918
Kila tupojitahidi kuweka mikakati ya ushindi, lakini marefa wamekuwa wakiwabeba kwa mbeleko timu pinzani. Nahisi kuna njama ya kutuhujumu.

Na inawezekana hata kutumia baadhi ya wachezaji wasio waaminifu kuhujumu timu.
 
Nyie si mnamchezaji anaitwa sijui HAJI MANARA yeye huwa anacheza kwenye media tu,
Technically Simba haikosawa, forward line na midfield haiko sawa, fanyeni tena usajili wa kifundi, mnawachezaji ambao hawana Hadhi ya kuchezea Simba..
 
Mara marefa wanaibeba yanga nara yanga wananunua mechi sasa marefa wanawaonea sasa tushike lipi katika haya matatu au ndio mfa maji aishi kutapatapa maana wakati mnaongoza ligi mlikuwa mnasema ubingwa mwaka huu msimbazi sasa mbona mumepoteza kumbukumbu na mumekuwa mnaongea vitu vya ajabu kama mafundi wa mnara wa babeli
 
Infact simba kwa sasa haina wachezaji wenye uwezo wa kuchezea simba kama mdau alivyosema.Simba ni timu kubwa haiwezi kujaza timu B tu bila kuwa na stricker wenye kipaji.
 
Viwango vya timu zetu zote ni mdogo nimeiona hata Yanga na Toto mpira ulikuwa si kama wa timu Bingwa. Kwa ujumla viwango vyetu ni majanga
 
Utalaumu dobi tu kaniki ndio rangi yake ukitizama timu yenu kama wadau hapo juu wameandika wengi hawana kiwango cha kuchezea simba pia hata hao wenye viwango unaona hawajitumi ipasavyo matokeo yake inaonekana timu ya kawaida mkikutana na coastal au toto wana dindisha mnaanza lawama.
Kama game ya jana wachezaji wenu kama vile waliridhika na sare huoni watu wakijituma hata usoni unamuona mtu kapoteza mpira anaona kawaida.
 
Hooo ndugu jitahidi kuwa mkweli simba tatizo siyo marefa sasa hivi wanasimba wanacha kulia na uongozi kujipanga next year mnalalamika tu!!! Wewe Jana wachezaji wanabaki na kipa wana piga nje sasa ulitaka refa hawaingizie mpira golini? Ngoma na Tambwe wakipata nafasi kama zenu goli mnalalamika offside jipangeni
 
Infact simba kwa sasa haina wachezaji wenye uwezo wa kuchezea simba kama mdau alivyosema.Simba ni timu kubwa haiwezi kujaza timu B tu bila kuwa na stricker wenye kipaji.
Eti Mbadala wa Dany Lyanga ni Hajji Ugando!!!!!!! Huu sasa utani.
Halafu unataka timu ichukue ubingwa
 
Kila tupojitahidi kuweka mikakati ya ushindi, lakini marefa wamekuwa wakiwabeba kwa mbeleko timu pinzani. Nahisi kuna njama ya kutuhujumu.

Na inawezekana hata kutumia baadhi ya wachezaji wasio waaminifu kuhujumu timu.
Hapa ndipo unapogundua udhaifu wa wapenda mpira wa bongo, ina maana hauoni udhaifu wa kikosi cha Simba!!! Hivi kweli mbadala wa Dany Lyanga ni Hajji Ugando!!! Mbadala wa Kiiza ni Paul Kiongela!!!!
Huu ndio udhaifu wa Mashabiki wanaoutumia viongozi wetu kutusajiliwa wachezaji wabovu halafu mwisho wa siku mtu anatumia Media kuwaaminisha mashabiki wa timu yao kuwa Yanga inabebwa ili kupunguza kasi ya mashabiki wanaoitaka Simba yao.
 
Kila tupojitahidi kuweka mikakati ya ushindi, lakini marefa wamekuwa wakiwabeba kwa mbeleko timu pinzani. Nahisi kuna njama ya kutuhujumu.

Na inawezekana hata kutumia baadhi ya wachezaji wasio waaminifu kuhujumu timu.
jiahidi kuweka data mkuu,ILA kwa kifupi timu yenu haiko na balance nzuri ya wachezaji ,mmoja Tu akikosekana tatizo pia uwezo WA kocha wenu kuhamasisha hana Jana walikua kama wapo zoezini
 
ha ha ha ha ha ha ha ha ha SIMBA bwana majanga tu ''shirikisho hawapo,hata club bingwa hawapo daah hata dk mwaka ndondo hawapo !!!
 
Back
Top Bottom