Simba kujitoa Ligi kuu, yasema kuonewa sasa basi.

Gumzo

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
211
7
DSC04735.jpg

KAMATI ya Utendaji ya Simba SC inatarajiwa kukutana kesho katika kikao cha dharula, kupanga tarahe ya Mkutano Mkuu kwa lengo la kuomba Baraka za wachama wake kujitoa kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kutokuwa na kutokuwa na imani na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Zacharia Hans Poppe, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, amekiambia Chanzo chetu usiku huu kwamba, kutokana na mwenendo huo wa TFF wameona hawatendewi haki na sasa wanaona bora tu wajitoe ili shirikisho hilo licheze ligi na timu inazozipenda.
Hatua hiyo inafuatia Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF, chini ya Mwenyekiti wake, Alex Mgongolwa, kuwaidhinisha Mbuyu Twite na Kevin Yondan kuchezea Yanga katika msimu ujao wa Ligi Kuu, unaoanza mwishoni mwa wiki.
Kikao cha Kamati hiyo, kilichomalizika hivi karibuni, pamoja na maamuzi hayo, kimeipa Yanga siku 21 kulipa dola 32,000 ambazo Simba SC ilimlipa Twite ili ajiunge nao, lakini baadaye akaghairi na kusaini na kuhamia Yanga.
“Kanuni zipo wazi, klabu inapotaka kumsajili mchezaji lazima kwanza izungumze na klabu yake, lakini katika usajili wa Yondan, Yanga hawakufanya hivyo,”alisema Hans Poppe.

Uamuzi wa Kamati hiyo leo, unafuatia kikao cha pamoja baina ya Simba na Yanga Jumatatu iliyopita kuvunjika bila kufikia makubaliano kuhusu mustakabali wa wachezaji hao.

CHANZO: GUMZO LA JIJI
 
Safi sana saafii hyo tumezidi kuonewa wachezaji wetu mwaka jana wamefungiwa na kupigwa faini, wakanyang'anywa point 3 walizopata kwa kuifunga azam, hi kweli kamati ya ligi imezidi kutwonea kwa sababu wao yanga wamejaa,
 
Naona YANGA imewashika pabaya sa mnaanza kutafuta visingizio vya kujisafisha kwa wanachama na mashabiki wenu ili kufunika madudu na mauvundo yenu mnayoyafanya...eniew kila lakheri myama uelekeako kwenye hiyo ligi unayoijua...kuna timu nyingi sana mfano pamba zinataman japo nafasi ya kucheza ligi kuu lakin hazipati pamoja na kugangamala kila mwaka!
 
simba lazima ionyeshe wao ni timu kubwa kuna kipindi serikali ya Brazil ilikuwa inachunguza kuhusu kampuni ya nike ambao ni wadhamini wa timu yao ya taifa kulazimisha Ronaldo del lima ambaye hakuwa fit kucheza mechi ya fainali shirikisho la fifa lilitishia kuwafungia brazil kwa hatua ya serikali yao na wao wakamjibu bila sisi hakuna mpira duniani na fifa wakafyata mkia hatuwezi kuvumilia tff wakivunja sheria kila siku simba igome tuone kama ligi itachezeka
 
Jamani! Lakini si tuliambiwa kuwa Twite kakatiwa RB akitia mguu tu nchini anakamatwa? Sasa hiyo RB imeyeyukia wapi tena? Vile vile yule msomali si alisema lazima Simba walipwe milioni 100 vinginevyo hao wachezaji hawatachezea Yanga, imekuwaje tena?

Simba, hiyo ndio faida ya kuwa na viongozi wasanii sampuli ya Rage. Sasa anadai anawatafutia nafasi mkacheze na kina Vikokotoni ligi ya Zanzibar!
 
hawa simba wakati yanga wananyang'anywa pointi mwaka jana walikuwa wakirukaruka
 
Siasa! wakijitoa nani atawlipa mishahara wachezaji wao wakti wameshasainishana mikataba!
 
Itabidi wote Simba na Yanga wajitoe na zife kabisa maana hawana faida katika soka la Tanzania kwani ndo wao wanaoua vipaji na mpira wa Tanzania kwa uchawi. Watu wanakwenda kwa tecknology na vipaji wao toka uhuru mpaka sasa ni uchawi tu na ndiyo maana mpira wa Tanzania haukuwi. Tunapigwa hata na Uganda?
 
juzi juzi kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ilishutumiwa kwa kuweka ushabiki badala ya kufata kanuni.Maamuzi yaliyotolewa kuhusu utata wa usajili wa wachezaji kelvin yondani na Mbuyi Twite kwa kiasi kikubwa yameonyesha huenda madai hayo yana ukweli ndani yake.Kelvin aliidhinishwa kuchezea yanga na simba kuambiwa waende polisi ili kuthibitisha uhalali wa sahihi yake lakini wakati wa mashindano ya kagame Tff walimuidhinisha kuchezea yanga kwa madai mkataba aliosaini simba unaonyesha unaanza kutumika desemba 2012 kwanini tff wanakuwa na kauli mbili tofauti lakini kama wamewaambia simba waende polisi wao wamethibitishaje kwamba sahihi iliyopo siyo ya yondani.Pia yanga wameambiwa walipe pesa ambazo simba ilimpatia mbuyi twite wakati inajulikana kabisa aliyepokea pesa ni Twite wala siyo yanga hii inazidi kuishushia heshima kamati za tff na kuwafanya wapenzi wa soka wapoteze imani na chombo hicho
 
simba lazima ionyeshe wao ni timu kubwa kuna kipindi serikali ya Brazil ilikuwa inachunguza kuhusu kampuni ya nike ambao ni wadhamini wa timu yao ya taifa kulazimisha Ronaldo del lima ambaye hakuwa fit kucheza mechi ya fainali shirikisho la fifa lilitishia kuwafungia brazil kwa hatua ya serikali yao na wao wakamjibu bila sisi hakuna mpira duniani na fifa wakafyata mkia hatuwezi kuvumilia tff wakivunja sheria kila siku simba igome tuone kama ligi itachezeka

kwani tanzania kuna ligi au vituko mfano mzuri ni mwaka jana wametwaribia sana ligi wache waondoke
 
DSC04735.jpg

KAMATI ya Utendaji ya Simba SC inatarajiwa kukutana kesho katika kikao cha dharula, kupanga tarahe ya Mkutano Mkuu kwa lengo la kuomba Baraka za wachama wake kujitoa kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kutokuwa na kutokuwa na imani na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Zacharia Hans Poppe, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, amekiambia Chanzo chetu usiku huu kwamba, kutokana na mwenendo huo wa TFF wameona hawatendewi haki na sasa wanaona bora tu wajitoe ili shirikisho hilo licheze ligi na timu inazozipenda.
Hatua hiyo inafuatia Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF, chini ya Mwenyekiti wake, Alex Mgongolwa, kuwaidhinisha Mbuyu Twite na Kevin Yondan kuchezea Yanga katika msimu ujao wa Ligi Kuu, unaoanza mwishoni mwa wiki.
Kikao cha Kamati hiyo, kilichomalizika hivi karibuni, pamoja na maamuzi hayo, kimeipa Yanga siku 21 kulipa dola 32,000 ambazo Simba SC ilimlipa Twite ili ajiunge nao, lakini baadaye akaghairi na kusaini na kuhamia Yanga.
“Kanuni zipo wazi, klabu inapotaka kumsajili mchezaji lazima kwanza izungumze na klabu yake, lakini katika usajili wa Yondan, Yanga hawakufanya hivyo,”alisema Hans Poppe.

Uamuzi wa Kamati hiyo leo, unafuatia kikao cha pamoja baina ya Simba na Yanga Jumatatu iliyopita kuvunjika bila kufikia makubaliano kuhusu mustakabali wa wachezaji hao.

CHANZO: GUMZO LA JIJI

haya ni maneno ya bin zubeiry mnazi wa yanga na kwa kuwa wanaamua kujitoa tubaki kwenye ligi nasie tujigambe vizuri tu..

Hala Azam FC
 
Hakuna kitu hapo. Huu ni ukigwangwalla tu, watashiriki ligi kama kawa, hichi ni kisilani cha kike.
 
... Kususia ligi ni utoto tu. Wanachama wanachagua viongozi ili viongozi waweze kufanya maamuzi kwa niaba ya wanachama, kulipeleka suala hili kwa wanachama ni udhaifu wa kiuongozi maana kutatokea fujo tu. Kuna ngazi za juu zaidi za maamuzi kama hawajaridhika na maamuzi ya TFF, kwanin wasiende huko? Au ndo kutaka sympathy ya mashabiki baada ya kuvurunda kwenye usajili? Shule muhimu!
 
nilisema toka siku ya kwanza kuwa Manji Yusuph ni mtu hatari sana kwa mambo ya michezo ya Tanzania.ni Jambazi la kutupwa ni jangili la kupoka haki za watu ..haya yanatokea sasa
 
nilisema toka siku ya kwanza kuwa manji yusuph ni mtu hatari sana kwa mambo ya michezo ya tanzania.ni jambazi la kutupwa ni jangili la kupoka haki za watu ..haya yanatokea sasa
huna lolote unaona sasa enzi za simba zimeisha unaanza kulalamika sisi wanayanga tumemchagua na tunamuheshimu kama unaushahidi na uongealo nenda mahakamani sio unachafua jina la mnyekiti wetu kwaheri na utapotea kama simba tv ilivyopotea.
 
Back
Top Bottom